GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ,
lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya
Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.