Limekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya mastaa wa Kibongo kuonesha
au kupiga picha anaponunua gari jipya huku suala la kuonesha kadi ya
gari likiwa gumu na ahadi zisizokwisha lakini mwigizaji ‘sexy’ mwenye
mvuto kwenye tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameandika
historia ya tofauti.
Mwigizaji ‘sexy’ mwenye mvuto kwenye tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KADI YA GARI
Ijumaa limenasa kadi ya gari jipya
la Lulu aina ya Toyota Rav4 New Model lenye rangi ya silva hivyo
kuthibitisha kuwa yeye si kama wale wanaohongwa magari bila kupewa kadi.
Habari zilidai kwamba Lulu ameamua kufanya hivyo ili kuwaziba midomo
baadhi ya mastaa waliozoea kutembelea magari ya kuhongwa na wanaume.
DONGO KWA WEMA?
Ilisemekana kwamba ni dongo kwa
mastaa wakubwa kama Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuhongwa gari la
kifahari aina ya Audi Q7 na yule kigogo wake maarufu kwa jina la CK,
kabla ya kunyang’anywa na kurudishwa kwa mwenyewe kwani lilikopwa.
Mfano wa Gari analomiliki Elizabeth Michael ‘Lulu’.
AU JACK WOLPER?
Kuna madai kwamba pia kijembe
hicho kilitupwa kwa Jacqueline Wolper Massawe ambaye naye aliwahi
kuhongwa gari la kifahari aina ya BMW X6 na yule aliyekuwa bwana’ke,
Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ambalo hadi leo linaozea Majembe Auction kwa
kuwa liliingizwa Bongo kimagumashi.
JE, NI AUNT AU KAJALA?
Kwa mujibu wa watu wake
wa karibu, pia dongo hilo huenda lilielekezwa kwa mastaa wengine kama
Aunt Ezekiel Grayson na Kajala Masanja ‘K’ waliowahi kuripotiwa kwa
skandali ya kuhongwa magari huku wengine wakitamba na magari ya
kukodisha wakidai ni yao.
Muonekano wa kadi ya Gari hilo.
LULU ATIRIRIKA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo
kutoka kwa chanzo makini, gazeti hili lilizungumza na staa huyo ambapo
alisema kwamba amechoka kila kukicha kutangaziwa sijui pedeshee gani
kamhonga gari, mara anakodisha magari atanulie mjini, jambo ambalo
halina ukweli wowote.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
LULU ANA HOJA
Lulu alitoa hoja kwamba ili
kuvunja kasumba hiyo, ameamua kuweka kadi ya gari hilo hadharani ili na
hao wenye kujitamba katika mitandao ya kijamii na magari yao ya
kifahari, waweke hadharani kadi zao zinazoonesha umiliki wao wa halali.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe.
“Mimi siyo Mswahili kama wengine ndiyo maana nimeonesha kadi yangu kutokana na maneno ya ajabu ya kila siku wanayonitangazia.
“Sasa nasema hivi, mimi nimeonesha kadi yangu na wao waweke hadharani
kadi zao za hayo magari yao ya kifahari wanayoringia mjini tuone
umiliki wao wa halali,” alisema Lulu ambaye ni staa wa kwanza Bongo
kuonesha kadi yake ya gari inayomuonesha kuwa ni mmiliki halali.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Kajala Masanja.
Mbali na gari hilo ambalo mwenyewe anadai amelinunua dola 27,000
(takriban shilingi milioni 44), pia Lulu anamiliki nyumba anayoendelea
kuijenga iliyopo maeneo ya Mbezi Shamba jijini Dar hivyo kuwafunika
mastaa wengi wakubwa wa tasnia ya filamu Bongo.
CHANZO NI GPL