EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Bongo Movies. Show all posts
Showing posts with label Bongo Movies. Show all posts

Wednesday, April 22, 2015

HIVI WASANII MTAKUWA NA UCHUMBA‭, ‬NDOA ZA MAIGIZO MPAKA LINI‭?‬


Kwenu mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo‭, ‬habari zenu bwana‭. ‬Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa‭.‬
Mkitaka kujua afya yangu‭, ‬mimi ni mzima‭, ‬namshukuru Mungu naendelea kutimiza majukumu yangu‭, ‬likiwemo hili la kuwaandikia barua‭.‬
Nimewakumbuka leo kupitia barua‭, ‬nataka kuwaambia kwamba mimi pamoja na mashabiki wengine wa sanaa yenu tumewachoka‭. ‬Tumechoka kuona na kusikia kila siku mkifanya maigizo kwenye maisha yenu halisi‭.‬
Hivi ni kwa nini kila kukicha tunasikia mnaachana‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye uhusiano wa mapenzi‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye ndoa kama mashabiki wenu wanavyowategemea‭?‬
Penzi linapoanza kushamiri‭, ‬mnalinadi kwenye mitandao na vyombo vya habari‭. ‬Mnawaaminisha mashabiki wenu kuwa mnapendana kwa kauli zenu motomoto lakini ndani ya miezi miwili mitatu penzi chali‭.‬Wengine mnaonesha kwamba mmedhamiria na kuamua kufunga ndoa kabisa‭, ‬lakini kumbe moyoni bado mnakuwa mna lenu jambo‭. ‬Mashabiki wenu wanafurahia kuona mmeoana lakini ndoa nayo haidumu‭, ‬mnaachana‭.‬
Mbaya zaidi mnapoachana mnapeana maneno ya kashfa‭, ‬mnaumbuana kiasi ambacho kinadhihirisha kabisa mlikuwa hamna mapenzi ya dhati‭ ‬au hamkudhamiria kabisa kuingia kwenye ndoa‭.‬Hivi kama kweli mlipendana‭, ‬nini kinawafanya muanze kuumbuana‭? ‬Badilikeni‭, ‬mashabiki wenu wamechoka kusikia kila kukicha ndoa ya‭ ‬staa fulani imevunjika‭, ‬wachumba fulani wameachana‭, ‬ni aibu‭.‬
Watu hawapendi kuona Nay wa Mitego na Siwema mkiwa mmeachana‭. ‬Tena mnaachana kwa kupeana maneno yanayoonesha kwamba mlikuwa hamna nia ya dhati ya kuwa wapenzi‭.‬Shamsa Ford na Dick‭, ‬kapo yenu ilikuwa nzuri‭. ‬Mlipamba vyombo vya habari‭, ‬uhusiano wenu ukazaa matunda ya mtoto mmoja lakini ndoto ya kuishi kama mume na mke imeyeyuka‭.‬
Nasibu Abdul‭ ‬‮!‬٪Diamond‮!&‬‭ ‬na Wema Sepetu penzi lenu lilikuwa likipendwa‭  ‬na wengi‭, ‬likaishia njiani‭. ‬Rose Ndauka na Malick Bandawe mlioishi na kubahatika kupata mtoto mmoja‭, ‬nini kiliwakuta‭? ‬Inasikitisha‭.‬Wolper na Dallas nao walipamba sana vyombo vya habari lakini mwisho wa siku chali‭. ‬Ndugu zangu‭, ‬mnapaswa kubadilika‭. ‬Msiigize maisha yenu‭. ‬Igizeni kwenye filamu‭, ‬mkirudi nyumbani mjitambue kwamba heshima‭, ‬upendo‭, ‬busara vinahitajika ili kuishi na mwenzako‭.‬
Mbona wapo wasanii wengi tu maarufu duniani na wamedumu kwenye uhusiano‭? ‬Kwa nini msiige mfano kwa mastaa kama Marlaw na mkewe‭, ‬Jay Z na Beyonce ambao wanaheshimu penzi lao hadi sasa‭?‬Jamani‭, ‬cha msingi mnapaswa kuheshimu suala la uhusiano‭, ‬msifanye masihara katika maisha ya ukweli‭.  ‬Vitu vingine vinapaswa kufanyika kwenye filamu pekee na siyo kuvihamishia katika maisha halisi‭.‬
Bila shaka mtakuwa mmenielewa na mtabadilika‭, ‬kila la kheri‭.‬

Wednesday, January 7, 2015

FRANK: RIYAMA ANANIZIBIA!


Nyota wa filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank.
Stori: Hamida Hassan na Shani Ramadhani
NYOTA wa filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank, amedai kuwa msanii mwenzie Riyama Ally anamzibia riziki kiasi kwamba sasa anamsaka ili amweleze kitu gani aliwahi kumkosea.
Akizungumza jijini hivi karibuni, Frank alisema anamtafuta Riyama ili aweze kumwambia ni kwa nini inakuwa hivyo kwa sababu katika filamu zote ambazo yeye anatakiwa kucheza, mwenzake huyo huwepo na ndiye anayependekeza watu watakaohusika na filamu hiyo.

Saturday, January 3, 2015

JOKATE: SIPENDI ‘SINI’ ZA KUTOMASWA!

Mwanamitindo ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo.

MWANAMITINDO ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo amesema kuwa hapendi kuigiza sini za mapenzi hasa zile anazotakiwa kushikwashikwa na mwanaume hasa asiyemjua.

Jokate Mwegelo akipozi.
Jokate alifunguka hayo wakati paparazi wetu alipotaka kujua namna ambavyo wazazi na mpenzi wake wanavyolipokea suala la yeye kuigiza sini za kushikwashikwa na wanaume tofauti katika filamu ndipo alipofunguka kuwa suala hilo limekuwa likipigwa vita na wazazi wake lakini analazimika kufanya kwa sababu ndiyo kazi aliyoichagua.
“Wazazi wangu wanachukia sana jambo hili na huwa wanasema bora niache filamu, hata mimi mwenyewe huwa sipendi ila huwa navumilia kwa kuwa ni kazi, sina jinsi,” alisema Jokate.

Monday, October 13, 2014

NORA: WEMA, LULU, WOLPER WANAWEZA, BATULLI, AUNT EZEKIEL, CHUCHU HANS HAMNA KITU!



Muigizaji wa filamu nchini, Nuru Nassoro maarufu kama Nora anaweza akawa ameshaongeza matatizo mengi kuyazidi 99 ya Jay Z.
Kwenye kipindi cha hivi karibuni cha Mkasi, Salama Jabir alimuuliza swali gumu kwake la kuwataja wasanii wa filamu wanaofaa na wasiofaa. Nora alikataa kutaja akijitetea kuwa hataki beef na mtu lakini watangazaji wa show hiyo walimrahisishia kazi na kuanza kuwataja ‘randomly’ waigizaji mbalimbali na kumtaka aseme tu kama wanafaa ama hawafai.
Hivyo ndivyo alivyojibu na kuwapa makavu live anaohisi wanafaa kurudi ‘kuflip burger’ na kuacha kuigiza.
Kajala – Hapana
Batulli – Hamna kitu
Steve Nyerere – Hapana
Wema Sepetu – Yeah anafaa
Rose Ndauka – Anafaa vibaya mno
Wolper – anajaribu… anafaa
Aunt Ezekiel – Hamna Kitu
JB – Anaweza
Hemed – Anaweza
Mlela – Hapana
Lulu – Ndiyo
Irene Paul – Anaweza
Chuchu Hans – Hamna Kitu
Unakubaliana na Nora?

Wednesday, September 10, 2014

BI MWENDA AMEMTAKA RAIS WA BONGO MOVIE UNITY AJIUZULU

MKONGWE wa uigizaji Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ amemtaka Mwenyekiti  wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ asijiuzulu kwani kazi aliyoifanya hadi sasa ni kubwa na nzuri.
Mkongwe wa uigizaji Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’
“Mimi nashangaa haya maneno yanatokea wapi sijui, lakini sipendi kusikia Steve Nyerere amejiuzulu na kama akijiuzulu, atakayekuja hawezi kuwa kama yeye ni mtu wa watu, hachagui habagui,” alisema.Mwenyekiti  wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Aidha alisema katika kipindi cha uongozi wake, klabu yao imekuwa na maendeleo makubwa.
“Katika viongozi waliopita hakuna hata aliyeleta maendeleo ya klabu yetu zaidi ya majungu tu, hata hivyo mimi naona Steve yuko sahihi sielewi wenyewe wanajifikiriaje,” alisema.

Thursday, September 4, 2014

IDD AZZAN, MAMA TUNU PINDA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA ‘MATESO YANGU UGHAIBUNI’

 
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda.
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan,  na mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda, ni miongoni mwa wageni watakaohudhuria uzinduzi rasmi wa filamu ya ‘Mateso Yangu Ughaibuni’ unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Leaders klabu vilivyopo Kinondoni jijini Dar.
Filamu hiyo imerekodiwa na kutengezewa na kampuni inayomilikiwa na Mtanzania  iitwayo Didas Fashion yenye maskani yake nchini Uingereza ambapo ndani yake kuna waigizaji Wastara Juma, Riyama Ally, Monalisa na Issa Musa ‘Cloud 112’
(Habari na Shakoor Jongo/GPL)

Wednesday, August 27, 2014

URAIS 2015 WAIBOMOA BONGO MUVI

KUMEKUCHA! Baada ya kuwepo kwa misuguano ya chini kwa chini kati ya viongozi na wanachama wa kundi la waigizaji wa filamu la Bongo Movie Unity, sasa siri imefichuka kuwa baadhi ya watu wanaotajwa kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wagombee urais mwakani, ndiyo wanaolibomoa kundi hilo kutokana na fedha wanazodaiwa kuzitoa.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Baadhi ya waigizaji wenye ushawishi katika kundi hilo waliliambia gazeti hili juzi kwamba, dhambi kubwa inayolitafuna kundi hilo ni kambi za kisiasa zinazoratibiwa na makada wawili wanaoonekana kuwa na ushawishi ndani ya CCM ambao wanatajwa kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu.

Wednesday, March 12, 2014

BONGO MUVI KUNA MASHOGA!

IMEBAINIKA kuwa ndani ya tasnia ya filamu Bongo kuna baadhi ya wasanii wanaofanya mapenzi ya jinsia moja yaani mashoga, Risasi Mchanganyiko limenyetishwa.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museven, kupitisha sheria nchini mwake ya kupiga marufuku mavazi yasiyo na staha, uvunjifu wa maadili na mapenzi ya jinsia moja.
Uganda ipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiunganishwa na nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda yenyewe.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo ndani ya kundi hilo, baadhi ya wasanii wa kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga, ingawa wanajifanya vidume vya mbegu.
“Wapo mashoga na mabwana zao tunawajua ila sema sasa kwa sababu huna ushahidi wa moja kwa moja na hujamfuma kwenye tukio, unashindwa kumtaja,” alisema msanii mmoja wa kike, Bongo.
“Yule…(analitaja jina la msanii mkubwa) bwana’ke alifariki na sasa ana mwingine lakini ndani ya Bongo Muvi anaonekana kiwembe kwa sababu ana msururu wa wanawake,” alisema.
AMSHAURI JK

Wednesday, February 5, 2014

BONGO MOVIES VIPANDEVIPANDE!

MPASUKO mkubwa umeikumba tasnia ya filamu Bongo baada ya baadhi ya wasanii wanaong’ara kuchukua kadi rasmi za kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wasanii walojiunga CCM wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
Tukio hilo lilitokea juzi, Jumapili jijini Mbeya kulipokuwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Mashabiki mbalimbali wa sinema za Kibongo, waliingia kwenye mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, mara baada ya wasanii hao kuonesha uamuzi wao, kila mmoja akieleza mtazamo wake.

WASANII WENYEWE
Baadhi ya wasanii waliochukua kadi za CCM ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Irene Uwoya, Haji Salum ‘Mboto’, Tamrina Posh ‘Amanda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Wastara Juma na Haji Adam ‘Baba Haji’.

MIJADALA
Watoa maoni walikuwa na mawazo tofauti kuhusiana na uamuzi wa wasanii hao wenye mashabiki wengi, wengine wakiwapongeza huku upande wa pili ukiwashutumu kwa maelezo kuwa wanawagawa mashabiki wao.

Wednesday, January 8, 2014

HOFU YA KIFO YATAWALA MASTAA BONGO

HOFU ya kifo imetawala kwa mastaa Bongo ikiwa ni siku chache baada ya gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita kutoka na habari ya utabiri wa Hussein Yahaya, ikieleza kuwa mwaka huu vifo zaidi vitaendelea kwa wasanii wa filamu, muziki, waandishi wa habari, viongozi wa dini na wanasiasa.
Aunt Ezekiel.
Baadhi ya wasanii wa sanaa mbalimbali Bongo na kueleza maoni yao kuhusiana na utabiri huo. Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Single Mtambalike ‘Richie’ aliye msanii wa filamu ambaye alisema:
“Namwamini Mungu kwa asilimia zote, hata kama kitatokea kifo mbele yetu nina imani kitakuwa na sababu kama ugonjwa na kadhalika, siyo ghafla."

Thursday, November 7, 2013

WEMA AIPASUA BONGO MUVI

KLABU ya mastaa wa filamu jijini Dar es Salaam, Bongo Movie ‘Bongo Muvi’ imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Honorati Lasasi Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilio asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria mazishi ya baba'ke Wema Visiwani Zanziabar.

Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
LAWAMA ZOTE KWA RAY
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.
Wema Sepetu (katikati) baada ya kuwasili Zanzibar. Kushoto ni rafiki yake Kajala Masanja.

Saturday, September 14, 2013

Jacob Steven ‘JB’ awachana Uwoya, Wema.

MSANII maarufu wa filamu hapa nchini, Jacob Steven ‘JB’, amewataka wasanii wakongwe na wenye majina kufuata nyayo za chipukizi wasio na majina ili waweze kumudu soko la sasa.

JB, aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano na kipindi cha Take One cha Clouds FM kuwa, wasanii wa zamani wenye majina, wamebakia kubaki na majina yao na kushindwa kuendana na chipukizi ambao wanakuja kwa kasi na kutikisa tasnia hiyo.

Aliwataja baadhi ya wasanii ambao wanamsikitisha kupotea katika ‘game’ licha ya kuwa na majina makubwa kuwa ni Wema Sepetu, Irene Uwoya, Blandina Chagula ‘Johari’ pamoja na Aunt Ezekiel.

Alisema wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu na kushindwa kuendana na hali halisi ya sasa na kuwa wakati umebadilika, huku akiwashauri kama wanahitaji kutoka, wanatakiwa kwenda na wakati wa sasa na kufanya kazi pamoja na chipukizi ambao wanakuja kwa kasi na kuwazidi wao na ukongwe wao.

“Mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada zetu wamepotea na kubaki na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka kwa sasa, waendane na mazingira ya sasa,” alisema.

Alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi wasanii hao wanaigiza, yeye alikuwa akicheza kama baba na kutokana na juhudi zake za hali na mali, ndiyo sababu ya kufikia alipo sasa na kujitegemea mwenyewe katika sanaa.

“Mimi kusema kweli nilikuwa kila filamu naigiza kama baba, lakini nikawa najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini na ndiyo maana nikajichanganya na nimetoka,” alisema JB.

Wednesday, September 11, 2013

HII NDIYO SAFARI YA MWISHO YA MSANII WA FILAMU MELISA

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likishushwa kwa ajili ya kuingizwa ndani.

 Siku ya jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Zuhura Maftah ‘Melisa’ aliyefariki dunia Jumapili iliyopita katika hospitali ya Hindu Mandal ambapo majonzi yalitawala nyumbani kwa dada yake Mikocheni ulikokuwa ukiagwa mwili wake na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar.
  Mtoto wa marehemu, Sabrina akiuaga mwili wa mama yake.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili.

Monday, September 9, 2013

MSIBA BONGOMOVIES: Mwanadada Zuhura Maftah (Malisa) hatunaye tena!

Habari zilizotufikia  zinasema kuwa mwigizaji wa bongo movies Zuhura Maftah  ama  Malisa (Pichani) amefariki dunia lsiku ya jana.
Bado hatujaweza kupata taarifa kamili za chanzo cha  kifo chake ila tnafanya juhudi kuweza kuzipata na tutawaletea hivi punde zitakapokuwa tayari.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Monday, September 2, 2013

TASWIRA ZAIDI WAKATI WA UZINDUZI WA FILAMU YA LULU IITWAYO FOOLISH AGE- SASA IPO MADUKANI.

 
Fetty Akiwa katika Mapozi tofauti tofauti wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uzinduzi uliofunika na kufana sana hadi kuacha Gumzo Jijini Dar, uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa iliyopita Chini ya Kampuni Mpya Kabisa ya Proin Promotions Limited.
Tino akiwafanyiwa mahojiano na Ceaser Daniel wakati wa Uzinduzi wa Filamu Mpya ya Elizabeth Michael aka Lulu iitwayo Foolish Age
Wadau wakijiachia
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakifuatilia Uzinduzi huo Kwa Makini
 JB akito tabasamu zito wakati akiwasili kwenye uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions limited ndani ya Ukumbi wa Mlimani City siku ya Ijumaa
 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliowahi kuingia Kwenye Ukumbi kabla ya Uzinduzi kuanza
Wadau wakiserebuka wakati Lady Jay Dee aka Anaconda, Aka Komandoo akitoa burudani ya kibao chake kipya Cha Yahaya..
Credit: Lukaza blog

Saturday, August 31, 2013

YAHAYA YA LADY JAY DEE YAMJAZA MAHELA LULU WAKATI WA UZINDUZI WA MY FOOLISH AGE.

UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.

Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.

“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.

Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City
 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...

LULU MICHAEL ALIVYO TOKELEZEA KATIKA UZINDUZI WA MUVI YAKE YA FOOLISH AGE - MLIMANI CITY.

1

Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti wake Jonson
Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki Lady Jay Dee aka Komando aka Anaconda akituzwa wakati akitoa burudani safi sana katika Uzinduzi wa Lulu ndani  ya Ukumbi wa Mlimani city.
8Elizaberth Michael (Lulu) akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti  wake Jonson Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku wa kuamkia leo.1aLulu akilakiwa kwa mbwembwe na vijana walioandaliwa kwa kazi hiyo. 2.Mwenyekiti wa kampuni ya Proin Promotion Bw. Jonson Lukaza katikati akizungumza na baadhi ya waigizaji wa filamu Rich Rich na mwenzake

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate