EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Jacob Steven ‘JB’. Show all posts
Showing posts with label Jacob Steven ‘JB’. Show all posts

Saturday, May 23, 2015

JB: NILILELEWA ‘KI-MAMA’ MAMA SANA!

Msanii nguli kwa sasa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven Mbura ‘JB’.
MKONO mmoja ulikuwa shavuni nikiendelea kusoma kitabu kipya cha ujasiriamali kilichoandikwa na mhamasishaji nguli barani Afrika wa watu kujikomboa na umasikini, Eric Shigongo kiitwacho Jinsi ya Kutoka Kwenye Umasikini Hadi Mafanikio kinachopatikana mitaani kwa bei nafuu, nikiinua kichwa mara kwa mara na kuangaza macho huku na kule nikimsubiri mtu aliyenifanya niwe katika eneo hilo. Ndiyo, sikuwa nimechelewa wala kuwahi sana, nilikuwa hapo kwa wakati.
Nilikuwa ndani ya viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, nikimngoja kwa hamu msanii nguli kwa sasa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven Mbura ‘JB’. Lengo likiwa ni moja tu. Kupata simulizi ya maisha yake tangu anazaliwa hadi alipo sasa.

Sikujishughulisha sana na magari yaliyokuwa yakiingia uwanjani hapo, lakini ghafla nililazimika kusitisha kila kitu baada ya kuingia gari ambalo kila aliyekuwa maeneo hayo alilikazia macho.
Ndiyo, ilikuwa ni Toyota, Land Cruiser VX-V8. Halikushangaza wengi kwa aina yake, bali kwa rangi ya mng’aro lililonakshiwa.
Baada ya salamu, mazungumzo yakachukua nafasi huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua maisha halisi ya gwiji huyu wa sanaa kwa sasa! Haraka sana naikamata na kuikaza vyema kalamu yangu na kuanza kudondosha wino kwa kila elezo alilolisema. Ungana nami katika simulizi hii tamu ya maisha halisi ya JB.

Monday, December 8, 2014

JB BETHIDEI YANGU NI KANISANI TU!

LEGENDARY wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ amesema kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo vimemkalia kushoto ni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya sherehe, yeye siku zote hufanyia kanisani kwa kufanya maombi.
Legendary wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’
Msanii huyo ambaye siku chache zilizopita alitimiza miaka kadhaa ambayo hakuwa tayari kuiweka wazi, alisema haoni umuhimu wa kupoteza fedha kwa kufanya sherehe kubwa katika siku yake ya kuzaliwa zaidi huwa anasali na kumshukuru Mungu.

Saturday, September 27, 2014

RAY, JB WAMPIGIA SALUTI KAJALA

Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti muigizaji mwenzao,  Kajala Masanja kutokana na filamu fupi aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na waandishi wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa  Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.

Tuesday, March 25, 2014

Msanii JB na Timu ya EATV Nirvana wauvamia mji wa LUSHOTO

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani,iliyoadhimishwa Duniani kote mnamo Machi 5, kampeni ya Grow ikiongozana na mmoja wa mabalozi wake muigizaji Jacob Stephen ‘JB’ iliungana na kipindi cha EATV Nirvana na kuutembelea mji wa Lushoto,Jijini Tanga.

Kampeni ya GROW, inayoendeshwa na Oxfam, inahamasisha mabadiliko kwenye mifumo iliyopo ili iwafanufaishe wakulima na wafugaji/wavuvi wadogo wadogo hususani wanawake wawe na maisha endelevu! Inawasherekea kwa mchango wao mkubwa wa kulisha nchi huku wakipambana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa masoko, pembejeo na miundo mbinu. Katika harakati hizi, mnamo mwaka 2011, shindano la "Mama Shujaa wa Chakula " lilizinduliwa rasmi hapa nchini. Lengo la tuzo hii ni kutambua mchango wa wanawake hasa waishio vijijini.

Huko Lushoto hali ilikuwa kama picha zinavyoonyesha...
Alfajiri ya Machi 6, timu ya Nirvana, Grow, pamoja na JB walielekea soko kuu la Lushoto ambapo walikutana na wakulima ili kusikia hadithi zao za mafanikio pamoja na changamoto. Nirvana na Kampeni ya GROW wanahamasisha lifestyle njema! Lakini tunavyokula vyakula bora, vyenye virutubisho tunajua vinatoka wapi!
Akizungumza kutoka katika sehemu yake ya biashara, Zinira Ally (kushoto aliyekaa) alishuhudia jinsi ambavyo anasomesha watoto na kulisha familia yake kwa pesa inayotokana na biashara yake ya uuzaji wa mbogamboga na matunda.
"Nzenze"... Salaam na wapenzi wa filamu zikiendelea.
JB, Lotus na Deo wakitizama mazao mbalimbali katika soko kuu la Lushoto.
Veronica Joseph ambaye ni muuzaji wa mboga mboga sokoni Lushoto anasema angependa kuona mabadiliko katika miundombinu ya soko ili kulinda ubora wa mazao, “soko halina ubora, watu wananunua vyakula hivi hivi kwa bei ghali kwenye supermarket kwa sababu ya ubora, sie tunauza tu bora tunauza, tunaogopa vyakula kuoza, tungekuwa na mafriji ya kuhifadhia mboga mboga na sisi tungeweza kuuza bei sawa na supermarket.”Akiendelea kutaja changamoto, Veronica ambaye ni mama wa watoto wawili, alionyesha kusikitishwa kwake na maisha duni wanayoishi wakulima, “mkulima analima chakula ambacho wengine wanakula hadi kutupa lakini yeye hawezi hata kula mlo kamili kwa sababu kipato anachopata ni kidogo” Veronica anaamini kama, “masoko yangeboreshwa, tungeuza bidhaa kwa bei nzuri ili na sisi tusomeshe watoto wetu na kujikimu kimaisha.”

Wednesday, December 4, 2013

Leo ni siku ya kuzaliwa ya muigizaji JB (Jacob Steven) , huu ndio ujumbe aliouandika kwa fans wake wote.


"...Namshukuru sana Mungu kwa kunilinda mpk kufika siku ya leo. Kwa akili na uwezo wangu nisongeweza ila kwa uwezo wake Mungu hata leo hii nipo salama.Ni mengi nimepitia lakn mkono wa Mungu u juu yangu ndio maana leo nipo kaama nilivyo.Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunizaa,mke wangu kipenzi Irene Makeula kwa kunilea kwa kila hali asante sana moyo wangu queen irene nakupenda sana.Pia kwa nafasi ya kipekee sana nawashukuru sana mashabiki wangu wote kwa kufatilia kazi zangu na kuwa pampja nami begakwabega ktk shughuli zote zinazofanya nathamini sana mchango wenu Mungu wangu awabariki sana.Asanteni wote ambao kwa namna moja au nyingine mmechukua nafasi yenu kunitakia kheri kwa siku yangu hii ya kuzaliwa Mkono wa bwana usiwapungukie..."

Happy birthday JB, Mungu akupe maisha marefu yenye mafanikio

Saturday, September 14, 2013

Jacob Steven ‘JB’ awachana Uwoya, Wema.

MSANII maarufu wa filamu hapa nchini, Jacob Steven ‘JB’, amewataka wasanii wakongwe na wenye majina kufuata nyayo za chipukizi wasio na majina ili waweze kumudu soko la sasa.

JB, aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano na kipindi cha Take One cha Clouds FM kuwa, wasanii wa zamani wenye majina, wamebakia kubaki na majina yao na kushindwa kuendana na chipukizi ambao wanakuja kwa kasi na kutikisa tasnia hiyo.

Aliwataja baadhi ya wasanii ambao wanamsikitisha kupotea katika ‘game’ licha ya kuwa na majina makubwa kuwa ni Wema Sepetu, Irene Uwoya, Blandina Chagula ‘Johari’ pamoja na Aunt Ezekiel.

Alisema wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu na kushindwa kuendana na hali halisi ya sasa na kuwa wakati umebadilika, huku akiwashauri kama wanahitaji kutoka, wanatakiwa kwenda na wakati wa sasa na kufanya kazi pamoja na chipukizi ambao wanakuja kwa kasi na kuwazidi wao na ukongwe wao.

“Mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada zetu wamepotea na kubaki na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka kwa sasa, waendane na mazingira ya sasa,” alisema.

Alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi wasanii hao wanaigiza, yeye alikuwa akicheza kama baba na kutokana na juhudi zake za hali na mali, ndiyo sababu ya kufikia alipo sasa na kujitegemea mwenyewe katika sanaa.

“Mimi kusema kweli nilikuwa kila filamu naigiza kama baba, lakini nikawa najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini na ndiyo maana nikajichanganya na nimetoka,” alisema JB.

Thursday, August 22, 2013

MASTAA HAWA... MAJINA YAO YA ASILI ‘YAMEKUFA’

KWA kawaida binadamu yeyote huzaliwa na kubatizwa jina ambalo hulitumia katika masomo na hata kazi yake.
 

Tofauti na ilivyo katika fani nyingine, wasanii wamekuwa wakijibatiza majina ya ziada (a.k.a). Mbaya zaidi, majina hayo huwa yanaanza kama utani lakini inafika wakati msanii husika analizoea jina hilo jipya na kulifanya kuwa kama rasmi.
Leo Amani linakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao majina waliyopewa na wazazi wao ‘yamekufa’, hawayatumii kabisa:
LULU
Jina lake halisi ni Elizabeth Michael, Lulu lilizoeleka kupitia tasnia ya uigizaji. Alianza kulitumia wakati alipojiunga na Kundi la Sanaa la Kaole.
Hadi leo hii, siyo rahisi kabisa mtu kutokea na kumuita jina la Elizabeth, wengi wanamfahamu kwa jina la Lulu.

RAY
Ray ndiyo jina ambalo limezoeleka na wengi. Vincent Kigosi alilopewa na wazazi wake ni kama limekufa. Kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu alipokuwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole hadi sasa.
Jina la Ray ndiyo watu wanalolifahamu zaidi ingawa hivi karibuni baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakijaribu kumuita Vincent ili kurudisha uhai wa jina hilo.

JOHARI
Jina lake halisi ni Blandina Chagula. Johari lilizaliwa kwenye Tamthiliya iliyobeba taito ya jina hilo. Akiwa katika Kundi la Kaole, alianza kujiita Blandy, baadaye alibadilisha jina hilo na kuwa Johari walipoingiza tamthiliya hiyo ambayo pia ilizaa filamu.
“Kuna wakati huwa najuta kutumia jina la a.k.a ambalo limefunika kabisa jina langu la asili,” anasema Johari.

DK. CHENI
Ameanza gemu kitambo, tangu Kundi la Splended.  Jina alilopewa na wazazi wake ni Mahsein Awadhi, kwa sasa limekufa. Hakuna anayelitumia, hata yeye mwenyewe.
Jina hilo lilizaliwa baada ya mazoea yake ya kupenda kuvaa cheni kubwa kwenye michezo iliyokuwa ikirushwa Runingani, kwa sasa wengi wanashindwa hata kulitamka jina lake.

Tuesday, August 6, 2013

AUNT EZEKIEL AFUNGA DIMBA LA KUFUTURISHA


 
Irene Uwoya ‘Mama Krrish’ akipata msosi wakati wa futari hiyo.
    Aunt Ezekiel akiongea jamba na marafiki zake wakati wa futari.
  Mcheza filamu mahiri Jacob Steven 'JB' akipata futari.
Yvonne Cherry 'Monalisa' akifurahia jambo wakati wa futari.
Chuchu Hans (kushoto) na Devota Mbaga wakipata msosi.
  
Kajala akiwa na mtoto wake Paula wakipata futari.
Aunt Ezekiel akiwa na marafiki zake.
   Beautiful Onyinye Wema Sepetu akiwa na shosti wake Kajala katika futari hiyo.
    Wema, Kajala na Sajenti katia pozi.
  
Kajala akiwa na Chuchu Hancs muda mfupi kabla ya kufuturu.
 
Kajala akiwa na mtoto wake katika picha ya pozi.
STAA mahiri wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel jana alifunga dimba la kufuturisha kwa mastaa baada ya kuwaalika watu mbalimbali nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kupata futari pamoja. Pichani juu ni baadhi ya taswira wakati wa zoezi hilo.
(PICHA NA IMELDA MTEMA / GPL)

Wednesday, July 3, 2013

MUIGIZAJI JB AMUONYA IDD AZZAN DHIDI YA KIPIGO KITAKATIFU ATAKACHOMPATIA KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI.

Jacob Steven 'JB' akijifua kwa ajili ya mpambano wake na Idd Azzan utakaofanyika katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013.
Jb akipiga pushapu kadhaa wakati wa maandalizi hayo.

Monday, July 1, 2013

JB AFUATWA NA MASTAA WAZUNGU KUTOKA ULAYA



MWIGIZAJI Bora wa Kiume Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amefuatwa na mastaa Wazungu kutoka Ulaya nchini Norway.

Hivi karibuni, Ijumaa Wikienda lilimnasa JB akipigwa na baridi usiku wa manane kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar ambapo alipoulizwa kulikoni alisema kuna waigizaji kutoka Norway wanaokuja kumfuata hivyo anawasubiri.
 
Alisema: “Kuna waigizaji Wazungu kutoka Norway wanakuja kunifuata, nimekuwa nikiwasiliana nao kwa muda mrefu, mwanzoni nilisita kwa kuwa nilikuwa siwajui. Baadaye nilijiwa na mawazo kwamba kwa nini nisiwatafute mtandaoni? Kweli nilipoingia mtandaoni na kutafuta majina yao niliwapata.
 
“Wapo wawili, majina yao ni Bard Yuvis Akir na Vega Uvisakir, waliniambia wanakuja kunichukua nikafanye nao kazi za filamu kwao, nikimaliza Tamasha la Matumaini tutarekodi filamu moja hapa nchini ndiyo tuondoke.”
wakati mazungumzo yakiendelea, JB aliitwa kwenye mlango wa kutokea uwanja wa ndege na kuwapokea wageni wake kisha kutimua eneo hilo.
CREDIT:GLP

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate