WAKATI tukiwa
tunakaribia kumaliza mwaka 2014, msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’,
amedai kuwa hakuna jambo ambalo mastaa wa Bongo wamelifanya zaidi ya
kuchuma dhambi na kutumia muda mwingi kupigana majungu kuliko kumcha
Mungu kwa matendo mema.
Msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na gazeti hili, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya
filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo
ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi
kuchafuana kwa kupigana majungu.