Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ akipozi.
Akizungumza na Kituo cha Radio Times FM cha jijini Dar, wikiendi
iliyopita, Jide alifunguka kuwa yeye ndiye aliyeamua kummwaga Gardner.Katika mahojiano hayo, Jide alisema kwamba alikuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gardner lakini alisema alikuwa akiteswa (hakuna mwanaume mwingine zaidi ya Gardner).