Mwigizaji wa bongo movies na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamedi ama shilole ameingia katika beef la hatari na mwigizaji, blogger na mtangazaji wa kituo cha DTV Christine Sintah “Sintah”
CHANZO NINI?
Habari zinasema kuwa tatizo limeanza baada ya Sintah kuandika
kwenye blog yake kuwa mwanadada Shilole kuwa hana Kipaji cha kuimba kama
tunavyonukuu maneno yake hapa chini…
“…sasa J wake Lo na Shilole jamani hebu tuweni wakweli aiiiii
nimesema kidogo kwa Lina anyway tusubiri collabo nahisi nitaenda
kuingiza vocal maana my dada hatokosa kuniita nijionee mchiriku mix…”
SHILOLE AMJIBU…
“Nashangaa, sijawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama
Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani, ameshangaa
watu wa Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia
muziki wa Marekani wakati wenyewe hawana muda muziki wa hapa Bongo,
anamchukia Sintah kwa kuongea kitu asichojua na kumponda yeye na Snura…”
“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha
J-lo kuimba naye lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea
video za muziki wangu alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane
naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko
kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,”
anasema Shilole….