EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Elizabeth Michael. Show all posts
Showing posts with label Elizabeth Michael. Show all posts

Thursday, August 27, 2015

Lulu amhenyesha Mboto ukumbini

IMG_1826
Haji Salum ‘Mboto akisaidia kulibeba gauni la Lulu.
DIVA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni amemhenyesha staa mwenzake wa filamu, Haji Salum ‘Mboto’ baada ya kumpa kibarua cha kulishika gauni lake lisiguse chini.
Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo Lulu na Mboto walikuwa washehereshaji.
IMG_1779Katika hali iliyoonesha Lulu alikuwa ‘siriaz’ stejini alimsisitizia Mboto kila mara ahakikishe amelishika gauni lake vizuri na asiliachie.
“Mboto hapa kazi yako ni kulishika gauni langu kwa nyuma kila nitakapokuwa nawe na ole wako uliachie,” alisikika Lulu ambapo Mboto alitekeleza ombi la Lulu.

Wednesday, August 19, 2015

Lulu amchokonoa Zari

lulu-na-diamondMwandishi Wetu
UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ëLuluí anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ëDiamond Platnumzí, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ëbethdeií ya DJ wa Diamond, Rommy Jones.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo.
rommmmILIANZA HIVI
Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí waliokuwa wakiwakodolea.
Kwa kuwa Diamond alikuwa host (mwendeshaji) wa shughuli hiyo, Lulu alikuwa akimwaga mauno huku akimshangilia Diamond kufuatia muziki wake wa nguvu uliokuwa unarindima ukumbini humo.

Monday, July 20, 2015

LULU AJIITA DEMU FEKI


Makubwa! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedai kwamba yeye ni ‘demu feki’ tena mwenye tabia za kitapeli huku kauli yake hiyo ikiacha baadhi ya watu midomo wazi na kutaka kujua kulikoni.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Lulu alisema kuwa ni kweli yeye ni demu feki lakini kama watu wanataka kujua kwa nini yeye ni feki na ana tabia za kitapeli wasubiri kujua kwa nini ameamua kujiita hivyo.
“Kama mtu anataka kujua ufeki wangu anisikilizie maana kuna kitu nimefanya kitathibitisha hilo,” alisema Lulu.

Monday, May 11, 2015

LULU AANIKA SIRI YA ‘KU-DATE’ NA WALIOMZIDI UMRI

Funguka! Sexy lady kunako sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anapenda kuminya ‘ku-date’      na wanaume wanaomzidi umri kwa sababu wanakuwa na nafasi nyingi katika maisha yake.
Elizabeth Michael ‘Lulu’
Akizungumza runingani juzikati, Lulu alisema anapenda kuwa na wanaume wanaomzidi kwa sababu wana nafasi tatu katika maisha yake ya kawaida, wanakuwa kama kaka, baba na mpenzi.
“Siwezi kuwa na mwanaume ambaye tunalingana kwa sababu atakuwa hana sifa hizo,” alisema Lulu.

Thursday, May 7, 2015

LULU: MIMI SINA JINI MAUTI JAMANI

MSANII nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’ amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea, Amani linakujuza.
Msanii nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’.
Akizungumza na gazeti hili juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana na matukio mengi yanayomtokea, muigizaji huyo wa filamu ya Foolish Age, alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana, hivyo anaamini kutokana na maombi yake, hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa anachokihitaji.
“Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa mwilini mwangu,” alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita, aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake.
Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake wa kimapenzi na binadamu.“Hapa nimshauri tu, achukue hatua ya matibabu haraka iwezekanavyo vinginevyo hali hiyo itaendelea, anatakiwa afanye kafara kwa kuchinja mnyama yoyote ili aondokane na matatizo haya,” alisema.

Wednesday, April 22, 2015

MAMA LULU ATAMANI MWANAYE AFE TU!

Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!

Lulu akiwa hoi nyumbani.
YOTE HAYA KISA MITANDAO
Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.
TUJIUNGE NA MAMA LULU
Akizungumza na gazeti hili, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.
MANENO KUNTU
“Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi.
“Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia.“Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?
“Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue,” alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Monday, April 20, 2015

LULU APATA KASHFA MPYA!

Waandishi wetu
WAKATI mwili wa bilionea Lusekelo Samson Mwandenga ‘Seki’ aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita ukitarajiwa kuzikwa leo mjini Dodoma, mitandao mbalimbali ya kijamii imempa kashfa staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa kumtaja kuwa alikuwa na uhusiano wa ‘kimalovee’ na marehemu huyo, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Seki ambaye alikuwa na urafiki mkubwa na mastaa mbalimbali wa Bongo Movies, alifariki dunia baada ya kuanguka nyumbani kwake Madale jijini Dar ikidaiwa kuwa alikuwa akitaka kumuokoa mwanaye aliyekuwa akianguka ndipo yeye akaangukia meza ya kioo na kumchana tumboni.
ALIKUFA AKIKIMBIZWA HOSPITALI
Hata hivyo, wakati akikimbizwa hospitalini jijini Dar, alivuja damu nyingi hali ambayo ilimsababishia umauti kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Saturday, April 18, 2015

LULU AFUTA AKAUNTI YAKE INSTAGRAM

Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ .
MUIGIZAJI wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyekuwa na wafuasi wengi kwenye Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na baadhi ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.
Kufuatia kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’, watu wengi walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku pia wakiweka picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu.
Msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.
Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga 'Secky' enzi za uhai wake.

Wednesday, March 25, 2015

LULU MASOMO YAMZUIA KUJIRUSHA

STAA wa filamu  Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekiri kuwa ubize wake katika masomo umemzuia kwa kiasi kikubwa kupata muda wa kufikiria mambo ya kijinga na hata kujirusha.
Staa wa filamu  Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akichonga na paparazi wetu juzikati, Lulu alisema mtu akisimamia kwenye masomo hawezi kuwa na mawazo mabovu kama ya kwenda kujirusha au kupata kilevi badala yake unajikuta ukifikiria masomo na mitihani tu.
“Jamani kama mimi sasa hivi sina hata ninachokiwaza zaidi ya masomo yangu na mitihani ninayokutana nayo yaani hata muda wa kusema utaenda Club, hakuna nafasi kabisa katika kichwa, hivyo nimeamini kuwa ukiwa bize na masomo akili za ajabu hazipo kabisa,” alisema Lulu.

Saturday, January 17, 2015

LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE


Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Stori: shani ramadhani
MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya kuigiza tu na si vinginevyo.
“Napenda kuwa msanii na ninaamini mimi ni msanii, niweke wazi kwamba mimi katika maisha yangu sitarajii kuja kuwa dairekta au script writer wala kuja kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuigiza.
“Asilimia kubwa ya wasanii hapa kwetu hatuwazi mbali, chochote tunachofanya tunaona ni sawa tu hatupo kibiashara kwa sababu bado ni masikini ndiyo maana wengine wanaigiza ili waonekane, tubadilike,” alisema Lulu.

Saturday, January 10, 2015

LULU APELEKEWA BARUA YA UCHUMBA

STAA ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.
Mshenga anayefahamika kwa jina moja la Isaya akipeleka posa kwa akina Lulu Elizabeth Michael.
MSHENGA NI MPAMBE
Kwa mujibu wa watonyaji wetu ambao waliwataarifu mapaparazi wetu wa Kitengo cha Kufichua Maovu (OFM) kuhusu barua hiyo na kutia timu nyumbani hapo, mtu aliyepewa kuifikisha kwenye familia hiyo ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam ambaye sasa amekuwa mshenga pia.

Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
MSHENGA GETINI KWA AKINA LULU
Ilikuwa saa tano asubuhi, mshenga huyo akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Corolla (namba hazikupatikana mara moja), alishuka nje ya geti kuu la nyumbani kwa akina Lulu ambapo anaishi na mama yake.

Thursday, January 8, 2015

PICHA ZA LULU ZATIKISA MITANDAO YA KIJAMII

Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta 'Lulu' akiwa katika mapozi tofauti baada ya kuachia picha hizi kupitia account yake ya Instagram siku ya jana na kupelekea kutikisa katika mitandao ya kijamii huku wapenzi wake wakimuita Kim Kardashian wa bongo.

Monday, January 5, 2015

LULU AMZAWADIA MAMA’KE NYUMBA

Imekaa poa sana! Taarifa tamu ikufikie kwamba sexy lady wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amemfanyia mama yake, Lucresia Karugila kufuru ya kufa mtu kisha kumzawadia ile nyumba yake anayoimalizia iliyopo Kimara jijini Dar.
Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Tukio hilo la kupongezwa lilichukua nafasi usiku wa Januari Mosi, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Great Wall iliyopo Masaki, Dar, ambapo Lulu alimfanyia mama yake pati ya bethidei akiwa anatimiza umri wa miaka 45.

Saturday, January 3, 2015

NDOA YA LULU YABUMA!


Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Stori: Musa Mateja
BAADA ya kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.
“Ndoa ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,” alisema Lulu.
Akizidi kupiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.
‘Lulu’ akipozi.
“Sina mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.
Alipotakiwa kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.

Saturday, December 20, 2014

LULU MAWIGI YANATUZEESHA JAMANI

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
“Nilijaribu kuweka mawigi pembeni na kujisukia tano kichwa changu kwa kweli naonekana katoto kabisa hapo ndipo nilipogundua kuwa mawigi kwa kipindi kingine siyo kabisa yanatuzeesha tu,” alisema Lulu.

Saturday, December 13, 2014

LULU: HAPPY AKISHINDA MISS WORLD NITAITWA LUPPY


Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu'.
Sehemu ya ujumbe wa Lulu katika Instagram.
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amendika katika Instagram kuwa mshiriki wa Tanzania kwenye Miss World, Happiness Watimanywa akishinda atabadilisha jina na kuitwa Luppy!

Friday, December 12, 2014

LULU AWATIKISA MAPEDESHEE BUKOBA

Staa wa Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mapedeshee wa Bukoba kumganda na kumzonga huku kila mmoja akitaka namba yake ya simu.
Staa wa Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisherehesha.
Lulu aliongozana na wasanii wengine akiwemo Kulwa Kikumba ‘Dude’ kwenye uzinduzi wa hoteli iitwayo Nalfin iliyozinduliwa juzikati wilayani Muleba ambapo staa huyo alionekana kuwaumiza vichwa wanaume wakware wenye fedha zao.

Thursday, December 11, 2014

LULU AMUWAHI IDRIS

ACHANA na watu kibao waliojitokeza mitandaoni na kudai wana undugu na mshindi wa Shindano la Bigbrother Hotshot (2014), Idris Sultan (21), mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ndiye mtu wa kwanza kabisa kujinadi kuwa na urafiki na mshindi huyo aliyejinyakulia zawadi ya shilingi milioni 510.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Idris.
Idris ambaye alinyakua kitita hicho nchini Afrika Kusini wikiendi iliyopita, aliwasili jana nchini na kupokelewa na Wabongo wengi ambao walimpongeza kutokana na ushindi huo alioupata baada ya kuwagaragaza washiriki saba wa nchi tofauti za Afrika.

Wednesday, November 19, 2014

KESI YA LULU YAWEKWA KIPORO

Stori: Musa Mateja KESI ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi za mauaji mahakamani, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
Mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa tena Februari mwakani kutokana na mlolongo mkubwa wa kesi za mauaji zilizopo Mahakama Kuu ya Tanzania.

Friday, October 17, 2014

LULU: BONGO MOVIES ISHABUMA


Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kwa mtazamo wake anaona Bongo Movies imebuma hivyo ameamua kukomaa na shule ili awe na kitu kingine tofauti na sanaa.
Staa wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate