Penzi matata linalowanyima usingizi baadhi ya watu mjini kwa sasa kati ya mwigizaji wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ limeibua tafrani kubwa huku waliokuwa wapenzi wa mastaa hao wakijikuta wakiangua vilio kweupe, Ijumaa limesheheni.
TATIZO MAHABA NIUE
Mara baada ya wawili hao kutangazwa rasmi kuwa sasa ni mahaba niue huku picha za ushahidi zikimwagwa, aliyekuwa mwandani wa Nay, Siwema a.k.a Wemalicious na aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’ wanadaiwa kujikuta kwenye hali mbaya kiasi cha kumwaga machozi.
TUJIUNGE NA CHANZO KWA SIWEMA
Habari kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Siwema jijini Mwanza zilidai kwamba, mara baada ya picha za wawili hao kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii aliumia roho hasa alipomuona Shamsa akijiachia kwenye nyumba ambayo alishirikiana na Nay kuijenga.
“Yaani Siwema ameumia hadi akajikuta akiangua kilio kwa uchungu. Sikukuu ya Pasaka ilikuwa mbaya kupita kiasi kwa Siwema. “Kinachomuuma zaidi ni kwamba hata nguo zake za mtoko Shamsa anavaa ‘gym’ na kufanyia mazoezi. Jamani kuna dharau zaidi ya hiyo? “Ukweli roho inamuuma vibaya mno,” kilisema chanzo hicho kwa ombi la kutochorwa jina gazetini.
Kabla ya kuhamia kwa chanzo cha mume wa Shamsa ili kupata ubuyu kamili, gazeti hili lilimsaka Siwema ili kujua anachukuliaje jambo hilo ambapo alifunguka ya moyoni.
SIWEMA AANIKA MAZITO
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Siwema mwenye mvuto wa kuvunja midume shingo alianika mazito kwamba, kitendo cha Nay kumuacha na muda si mrefu kwenda kwa Shamsa ni upuuzi.