EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Ray C. Show all posts
Showing posts with label Ray C. Show all posts

Monday, March 16, 2015

RAY C: MAMA YANGU ANAUMWA SANA

Musa Mateja STAA wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ambaye anatumia dozi ya kumwezesha kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, amesema kuwa mama yake mzazi yu mgonjwa sana, akisumbuliwa na maumivu makali, Ijumaa Wikienda lina mkasa kamili.
Mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, staa huyo alisema kwa zaidi ya siku tatu mfululizo, mama yake alishindwa kupata usingizi kutokana na maumivu ya mifupa ya miguu yaliyomfanya avimbe miguu, kitendo kilichosababisha ajikute akilia kama mtoto mdogo.
Rehema Chalamila 'Ray C'.
“Ujue mara ya kwanza aliuguaga na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, baadaye Mungu alimjalia akapona lakini naona ugonjwa wake umerudi tena. Anasumbuliwa na mifupa ambayo inamfanya wakati mwingine avimbe miguu hadi anashindwa kutembea,” alisema nyota huyo maarufu kama Kiuno Bila Mfupa.
Alisema mama yake amekuwa akipata shida kutembea kiasi kwamba Ijumaa iliyopita, alimpeleka hospitali ya Wachina iliyopo Sinza ili kupata vipimo na dawa, lakini haikusaidia.
“Hapa ninapoongea na wewe leo Jumamosi Machi 14, nipo kwenye Hospitali ya Misheni hapa Tegeta tumekuja kupata matibabu na kalazwa kwa muda ili afanyiwe vipimo vya MRI, maana leo usiku hajalala kabisa kwani muda wote alikuwa akilalamika tu miguu inamuuma.
“Imefikia wakati hadi nahisi maumivu yake na nabaki nalia tu, nampenda sana mama yangu kiasi kwamba natamani hata ningekuwa na fedha za kutosha kama zamani, hivi sasa ningekuwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi, anateseka usiku na mchana,” alisema Ray C.

Friday, February 13, 2015

RAY C, BABA MWENYE NYUMBA WAKE KIMEUKA

Stori:Waandishi wetu/Ijumaa
Inadaiwa kuwa kimenuka kati ya msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ na baba mwenye nyumba wake, Hussein Kassim baada ya mdada huyo kudaiwa kugoma kutoa vyombo vyake kwenye mgahawa aliopangishwa na mkataba kuisha.
Msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Ray C aliyekuwa akitoa huduma ya chakula na vinywaji kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kupitia mgahawa wake maarufu kwa jina la Ray C Restaurant, alifikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa na yeye alipwe fidia ya shilingi laki moja kwa ajili ya ukarabati alioufanya.
Akizungumza na gazeti hili, baba mwenye nyumba hiyo alisema baada ya Ray C kugoma kutoa vitu vyake, aliamua kwenda kumshtaki kwa mabosi wao wa kitengo cha Methadone ambacho kinamtibu Ray C na yeye mwenyewe kwani wote ni waathirika wa madawa ya kulevya.
Baba mwenye nyumba huyo alidai baada ya kumshtaki katika kitengo hicho, Ray C aliahidi kwenda kuvunja ukuta ambao aliujenga na kuchukua vitu vyake hivyo baada ya siku mbili na angepeleka ufunguo kwa mkuu wa kitengo cha Methadone.

Friday, February 6, 2015

RAY C AAPA KUMSAIDIA DAZ BABA

Na Hamida Hassan
Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Chanzo chetu cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
Staa wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C, alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie walipofikia kwa sasa.

Monday, September 29, 2014

RAY C SASA ATAKA KUOLEWA NA MZEE!

 
Utu uzima dawa! Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atamlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza kulea  mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
 Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya/GPL

Saturday, July 12, 2014

CHID BENZ AMPIGA RAY C

CHANZO NI GLOBAL PUBLISHERS Uonevu! Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.
TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.

Wednesday, March 5, 2014

Ray C amtaka Lord Eyez kubadilika

 
Staa nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’amemtaka aliyekuwa mpenzi wake, Lord Eyez kubadilika kutokana na changamoto za maisha zinazomkuta hasa ya kutuhumiwa mara kwa mara kuiba mali za watu. 
Msanii huyo wa hip hop kutoka kundi la Weusi,Lord Eyez anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kuvunja gari na kuiba laptop huko Arusha,ambapo Kundi lake la Weusi limetoa tamko kuhusu msanii huyo kutoka na natukio hilo.Kupitia account yake ya Instagram aliandika hivi…Badilika babaa......Nakuombea sana ujitambue na ubadili mwendo wa Maisha yako...Wewe bado ni kijana mdogo sana na una kipaji cha pekee.....Kila Mtu Ana changamoto yake ya maisha,angalia wapi ulipokosea,litambue tatizo halafu kubali kwamba una tatizo then rekebisha Hilo tatizo.

Thursday, December 19, 2013

RAY C AANIKA VIGEZO VYA MUMEWE MTARAJIWA

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi.
Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.
“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.
“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka  meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.

Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.
“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.
Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.

Friday, September 20, 2013

STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’ ameamua kuianika gari yake ambayo anatembelea kwa sasa ...


Gari hilo ni aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajilihazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… J aguar don'tcare...CHL means Chalamila Family.....Pongezi za kutosha zikufikie Ray C popote ulipo. Huoni  mwanzo mzuri  baada  ya mateso ya madawa  yakulevya yaliyokufanya  uwe teja

Saturday, September 7, 2013

RAY C: SIJAPATA UKIMWI, SIJAOKOKA

MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.

Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.

Wednesday, August 28, 2013

RAY C AMEBADILIKA SANA,SASA AINGIA GYM RASMI KUREJEA KWENYE MZIKI.

ray c 
Zaidi ya sauti yake na uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo zinazoshikika kiurahisi, umaarufu wake mwingine mkubwa toka enzi hizo ni kiuno bila mfupa kwa jinsi alivyokua akicheza nacho….. ni uwezo uliofanya mpaka maneno ya kiuno bila mfupa yakapata umaarufu kupitia yeye.
Siku kadhaa tu baada ya kutangaza kurudi kwenye muziki kama zamani, Ray C akiwa ametoka kwenye matibabu ya matumizi ya dawa za kulevya… ameanza kujipanga kupunguza unene alionao ili awe mwepesi zaidi ya alivyo sasa ili kila kitu kiende kama kilivyokua.
Ray C akipiga story na fans wake alisema “Mauno ni nyonga si manyama”, hii ni moja ya sababu za msingi sana zilizomfanya Rehema Chalamila kuingia gym kuanza mazoezi.
ray4 ray3

Saturday, August 24, 2013

MIDUME YAJITOKEZA KUTAKA KUMUOA RAY C.

Siku chache baada ya kupona madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’ midume kibao imejitokeza kuwania kumuoa staa mkubwa wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Risasi Jumamosi limeinyaka.

Ishu hiyo ilianza tangu mwanadada huyo maarufu kama Kiuno Bila Mfupa alipohojiwa kupitia CloudsTV ambapo alieleza jinsi alivyofiti kiafya.
 
“Unajua tangu aliposema anamshukuru Mungu kumuepusha na shetani wa madawa ya kulevya, wanaume kibao wamekuwa wakimfuatilia wakitangaza dau la kumuoa.
“Lakini pia kilichochochea zaidi wanaume kutaka kumuoa ni pale aliposema amepima Ukimwi na yupo fiti kabisa kiafya.

Thursday, August 8, 2013

HIKI NDICHO AICHOANDIKA RAY C ,LAWAMA ZOTE AMEZIELEKEZA KWA MPENZI WAKE ZA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.


 
Ray ameandika haya
"The New Ray C, Am a Strong Lady!!!!kila Nipewapo Mtihani mgumu wa Maisha napigana mpka nakuwa mshindi."

RAY C ASIMULIA KILICHOMFANYA AANZE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA........LAWAMA ZOTE AMEZIELEKEZA KWA MPENZI WAKE

Muimbaji wa ‘Niwe Nawe Milele’ Rehema Chalamila aka Ray C jana alifanya interview ya kwanza ya TV tangu takriban miezi 10 iliyopita baada ya kujichimbia kupata matibabu ya madhara aliyokuwa amepata kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akiwa na muonekano mpya, mchangamfu, aliyenawili, mrembo na mwenye afya njema, Ray C alizungumza kwa undani kwenye The Interview ya Clouds TV kuanzia namna alivyoingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, jinsi yalivyomwathiri na namna alivyosaidiwa hadi leo amekuwa hivyo.

Friday, July 5, 2013

UJUMBE WA RAY C KWA MASHABIKI WAKE SOMA HAPA.

BAADA ya kimya cha muda mrefu tangu alipogundulika kuwa hoi kwa madawa ya kulevya na kusaidiwa na Rais Jakaya Kikwete, msanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila a.k.a Ray C amewaandikia ujumbe na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa sasa yupo fiti.
Ujumbe aliouandika Ray C kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

Ray C ambaye kwa sasa haijulikani anaishi wapi alitupia picha ya muonekano wake mpya katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram na kuwatoa watu hofu huku akiwashukuru mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono tangu enzi hizo hadi sasa.
 
                                                                     Ray C.
Staa huyo aliandika: “Nipo fiti. “Nawapenda sana mashabiki wangu walionisapoti tangu miaka hiyo hadi leo! “Thank u so much for u’r support hugs and kisses! Ray C.”

Monday, June 3, 2013

MASTAA ‘UNGA’ UTAWAMALIZA

 
                                                     Rehema Chalamila ‘Ray C’.
LEO Michano haitaegemea kwa msanii au staa mmoja. Habari mbaya ni kwamba baadhi ya wasanii wetu wamejikita kwenye matumizi, usafirishaji na biashara haramu ya dawa za kulevya.
                                                                             Msafiri Diouf.
Wasanii mna mashabiki wengi. Sibishi katika hilo. Kama mlikuwa hamjui, mashabiki wanawapenda. Hawapendi kuwaona mkipoteza maisha mkiwa wadogo kwa sababu ya madawa ya kulevya.
Kama hamjui, madawa ya kulevya au unga au poda au baga kama mnavyoita limekuwa ni janga la kitaifa sasa.
                                                                 Aisha Madinda.
Mkitaka kuamini ninachokisema katizeni mitaa ya Kinondoni-Manyanya, Dar muone vijana wadogo wanavyovuja udenda wakiwa hawajiwezi kiafya. Hakika nguvu kazi ya taifa langu inapotea, familia nyingi na taifa vinaathirika kisa ni starehe inayopatikana katika kubwia unga, uvutaji bangi, unywaji pombe wa kutupwa, matumizi ya mirungi, shisha na vileo vingine.
 
Sawa, kila mtu anahitaji starehe lakini siyo hiyo ambayo kwa sasa mmetumbukia humo.
Kama mlimsikia Prodyuza wa Bongo Records, Paul Mathyasse ‘P-Funky Majani’ alisema kuwa 
 
Albert Mangwea ‘Ngwea’ aliyefariki wiki iliyopita aliingia kwenye matumizi ya unga kwa sababu ya ‘stress’ tangu mwaka 2006.

Monday, December 10, 2012

Hatimaye Ray C ameonekana na afya inayoridhisha.

 
Mh.Rais Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Rais kumshukuru kwa kumsaidia matibabu.mungu amsaidie asirudie jaman.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate