Na Imelda Mtema
KILICHOMPATA Madam Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari.

Rita Poulsen ‘Madam’.
Akizungumza baada ya kuwa kimya muda mrefu
ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa
kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea
chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru
kwa kutoka salama.
Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo
aliipata katikati ya Jiji la Dar na kusababisha kuvunjika kwa kifundo
‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya
hospitali kumuwekea ‘hogo’.