EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, October 2, 2012

AMANDA POSHY ASEMA ANAPENDA KUKATA NYELE ZAKE KUFUGA NYELE KWAKE NI WAZIMU.

Alichosema Amanda Poshy katika wall yake ya Facebook yaani kati ya vitu uwa siviwezi na vinanitia wazimu ni kufuga nywele....kwanza nikisukwa naona kama msusi ananionea tu....me napenda kukata nywele kama hivi.....najivunia kuwa na kichwa kizuri...

Hizi ndio gharama mpya za huduma ya BlackBerry (BIS) kutoka Vodacom.


Kwa wiki ni Tsh 6000.
Kwa Mwezi ni Tsh 17500.
Furahia internet isiyo na kikomo na yenye spidi na huduma zote za BlackBerry bila kikomo kuanzia e-mail, kuperuzi mitandao na BBM!
Kazi ni kwako!

Monday, October 1, 2012

Mkurugenzi Jiji la Mwanza aingia matatani

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, ameingia matatani baada ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kumwandikia barua ya kumtaka atoe maelezo kwanini ameshindwa kuwalipa fidia wakazi tisa wa eneo la Kangae B kiwanja Na. 240 kitalu “EE” jijini humo waliobomolewa nyumba zao bila kuwapa taarifa.
                          Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe.
Barua ya wizara hiyo yenye kumbukumbu namba  LD/146519 Vol. V/23 iliyoandikwa Juni 23, mwaka huu na kusainiwa na Anna Mdemu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, ikimtaka Mkurugenzi huyo atoe maelezo ya kina ya suala hilo.

Barua hiyo ambayo NIPASHE imeiona, imeeleza kuwa kulikuwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu wakati wa ubomoaji na kumilikisha kiwanja hicho na hivyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilemela iliamulu wananchi hao walipwe fidia kutokana na hasara waliyoipata.“Wizara inahitaji kupata taarifa kamili juu ya mgogoro huo na kiini cha mgogoro na ni kwa nini hamjawalipa fidia wananchi hao kama ilivyoazimiwa kwenye kikao cha ulinzi na usalama cha wilaya,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.Naye Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kabwe alipoulizwa ni kwa nini amekaidi agizo la wizara la kuwalipa fidia wakazi hao, alijibu kwa kifupi kuwa wakazi hao walivamia eneo hilo na walijenga kinyume cha sheria kisha kukata simu.Kamishna wa Ardhi wa Wizara hiyo, Anna Mdemu, alithibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi hao na  kusema kuwa walimwandikia barua Kabwe kutaka kutolea ufafanuzi juu ya mgogoro huo.“Ni kweli tulipokea malalamiko hayo, lakini suala hilo kwa sasa lipo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi,” alisema Mdemu.Mmoja wa waathirika wa bomoabomoa hiyo, Mussa Maduka, alisema Juni 23, 2009 majira ya mchana, Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiongozwa na  Kabwe ilitumia mabavu ya kubomoa nyumba hizo bila kuwapa taarifa ya kuondoka eneo hilo wala kupewa fidia.Alisema kufuatia hali hiyo, walitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa naye akamwagiza Mkuu wa Wilaya ashughulikie suala hilo kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya na Novemba 13,2009 walisomewa na Mkuu wa Wilaya maamuzi yalioyotolewa na kamati hiyo mojawapo likiwa ni kuitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi ilipe fidia wanachi tisa waliobomolewa nyumba hizo.

Alisema maamuzi mengine ni  kuwa wananchi waliobomolewa warudishiwe eneo hilo na waliohusika na ubomoaji huo wawajibishwe mara moja maana haki na utawala bora haukuzingatiwa.Maduka alisema kipindi kirefu kilipita pasipo maamuzi hayo kufanyiwa kazi ndipo walimuandikia barua aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa wakati huo, John Chiligati, ili awasaidie kudai haki yao.Alisema tangu mwaka huo hakuna msaada wowote walioupata kutoka katika uongozi wa serikali badala yake walikuwa wanazungushwa huku mwafaka wa kumaliza kwa mgogoro huo ukikwama.Alisema Juni 6, mwaka huu waliamua kulifikisha suala hilo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, ambaye aliandika barua iliyosainiwa na Mdemu ya kumtaka Mkurugrnzi wa Jiji la Mwanza Kabwe awalipe fidia wakazi hao.
SOURCE: NIPASHE

Kuna utata mkubwa sana juu ya umri wa Wema Sepetu, Juzi ka-turn 22, kumbe alishiriki na kushinda Miss TZ akiwa under 18?

Obviously she is beautiful, she is a star, she makes headlines, lakini je is she really 22???
Ijumaa ya last week 28th Sept ilikuwa ni birthday ya Wema Sepetu, hakuna asiyemfahamu kutokana na kuandikwa kila kukicha katika magazeti pendwa kutokana na mambo mbali mbali yakiwemo ya mahusiano aliyokuwa nayo na star mwenzake Diamond Platnums na mengineyo.

Katika siku yake ya kuzaliwa hiyo Ijumaa ilisemekana Wema ame turn 22, kwa maana kwamba alizaliwa 28th Sept, 1990. Sawa hilo hata sisi kwetu lisingekuwa na tatizo kabisa sababu huwezi uka judge age ya mtu kama ni kutoka kwake mwenyewe.Lakini contoversial angle katika hili swala ikaanza kujileta yenyewe kutokana na records ambazo tayari zipo na zinazofanya issue hii iwe na mkanganyiko. Issue kubwa ni kwamba Wema tayari yupo katika orodha ya walimbwende walioisha wahi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World kutokana na yeye kufanikiwa kulinyakua taji la Miss Tanzania mwaka 2006.Sasa kama alishinda taji la miss Tanzania mwaka huo 2006 takriban miaka 6 kutoka leo, JE, hiyo inamaanisha mwaka huo alioshinda taji hilo alikuwa ana miaka 16?? Kama ndio, hili linawezekana vipi binti aliye chini ya miaka 18 kuruhusiwa kushiriki mashindano hayo? Na mbaya zaidi akashinda taji na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia?

Kama vile haitoshi mapema mwaka huu Wema alifanyiwa Interview na Salama Jabir katika show inayozidi kupata umaarufu kwa sasa ya MKASI. Moja ya maswali aliyoulizwa Wema ni kuhusu lini alianza kujihusisha na mambo ya mapenzi, na jibu lake lilikuwa alipofikisha miaka 18. Salama alionesha kutaka kujua zaidi na akamuuliza tena ni lini alifikisha miaka 18, mrembo wema alisita kidogo na kumwonesha Salama kama anaogopa kusema bt end of da day akasema ni kama miaka 5 iliyopita, jibu lililomshtua Salama kidogo lakini akalipotezea na kuendelea na mengine.

Hiyo ni Interview ya mwaka huu 2012, na kama alidai kaanza mahusiano miaka 5 iliyopita that means kwa mujibu wa jibu la wema basi aliturn 18 mwaka 2007, ambayo bado inathibitisha alishiriki mashindando ya Miss Tanzania 2006 akiwa under 18. Did she lie ili aweze kuruhusiwa kushiriki? We don'tknow.Sikilizahapachinimudahuu.Baada ya story hizo za wema kuturn 22 Ijumaa iliyopita watu mbalimbali walianza kuhoji maswali juu ya umri huo huku wakioanisha na mwaka alioshinda taji la miss Tanzania. haya ni baadhi ya maoni ya watu kuhusu swala hilo kupitia Jamii Forum siku ya jana.
                        Chanzo cha habari leotainment.blogspot.com

Basi la Adventure lawaka moto, abiria 10 wajeruhiwa

Zaidi ya abiria 10 akiwemo askari polisi mmoja wanahofiwa kufariki dunia huku wengine tisa wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Adventure lenye namba za usajiri T 294 ABD aina ya Scania walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto katika kijiji cha Nyantakala wilayan Biharamulo mkoani Kagera.Ajali hiyo imetokea jana saa 4:30 asubuhi wakati basi hilo likitokea mkoani Mwanza kwenda Kigoma. Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa kwenye hospitali Teule ya Wilaya ya Biharamulo wamejeruhiwa vibaya akiwemo wakala wa kukatisha tiketi wa basi hilo, Dotto Tryphone (30), ambaye amevunjika miguu wakati wakijinasua kutoka kwenye basi hilo. 


Kwa mujibu wa wakala huyo, basi hilo lilikuwa na abiria 54 waliokuwa wamekaa kwenye viti na abiria ambao hawakuweza kutambulika idadi yao waliokuwa wamesimama kutoka mwisho wa gari hadi mlangoni kutokana na basi hilo kujaza abiria zaidi ya uwezo wake.Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Paulo Alex Kalangi, alisema atatoa taarifa baadaye kwa kuwa alikuwa safarini kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo majeruhi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi hilo kufika kwenye tuta  la kuzuia mwendo kasi ambapo ghafra walianza kuona moshi ukitokea ndani ya basi kabla ya kushika moto na kuanza kuteketea. Dereva wa basi hilo ambaye hakutambulika jina lake haijajulikana kama alikimbia au aliteketea kwenye basi hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo.
    
Mganga Mkuu msaidizi wa hospitali hiyo, Dk. Gabriel Mashauri, alisema amepokea majeruhi tisa na kwamba saba kati yao walikuwa katika hali mbaya, lakini bado wanaendelea kupatiwa matibabu. Aliwataja majeruhi waliolazwa kuwa ni Phinihas Elias (37), Pius John(21), Msigwa Isaya (18), Johary Chapa (23),Josephina Ngereza (46), Rashidi Mahonda (48) na Eles Ngereza(60).Waliovunjika miguu wametambulika kwa majina ya Dotto Tryphone (30) mkazi wa Nyakanazi na Zainabu Issa, wote wamevunjika miguu ya kushoto.

Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee.


                    Mwonekano wa nje wa kasri la Mch. Mh. Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).
Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuguswa.Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, nyumba hiyo haikubomolewa kutokana na pingamizi la mahakama.Nyumba inayotajwa kuwa mali ya Mchungaji Lwakatare, imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za bahari ya Hindi.

Viwanja hivyo vinadaiwa kupatikana kwa ushirikiano wa Mchungaji Lwakatare na Frank Mushi.Mdee alisema wakati kigogo huyo (Lwakatare) amehamia kwenye nyumba yake kwa matangazo na mbwembwe, mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa, lakini zaidi kuwepo raia waliobomolewa kwa mujibu wa sheria hizo.

Mdee alinukuu Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004, fungu 57(1), inasema hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60.Mita hizi ni ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri ulinzi na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa bahari, kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili wa ziwa.Sheria nyingine ni ya ardhi, namba 4 ya mwaka 1999, sura 113, fungu la 7 (1) (d), ikieleza kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka kingo ya mto na bahari, linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa.

Na pale inapotokea kuwa masharti ya sheria moja yanapingana na masharti ya Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa mazingira, sheria hiyo inatumika, kwa mujibu wa fungu 232 la sheria ya mazingira sura 191 ya mwaka 2004, “Kutokana na hali hii, serikali inatakiwa kujinasua katika mwendelezo wa tafsiri wanayoipata wananchi kuwa imetekwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache wenye uwezo,” alisema na kuongeza, “maana wanaona kuwa huu ni mwendelezo wa serikali kuwa na kigugumizi pale sheria zinapovunjwa na vigogo serikalini, au watu wenye fedha wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala kufanya ufisadi.”

Alisema hali ilivyo sahihi inadhihirika kuwepo kundi la wanaojiona wapo juu ya sheria, huku wanyonge wakishughulikiwa, “Ni wakati kwa mawaziri wanaohusika na masuala ya ardhi na mazingira kuwaeleza Watanzania kulikoni wananchi wa hali ya chini kuvunjiwa nyumba wakati Mchungaji Lwakatare, ambaye uharibifu wake ni wa hatari kuliko waliovunjiwa akitamba mtaani, ” alidai.

Mdee alitafsiri kitendo hicho kama ni Mchungaji Lwakatare kutamba kuwa yuko juu ya sheria na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kumzuia kufanya alichofanya, ”Ni aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa aina hii! Viongozi ambao wako tayari kutumia fedha, hila, mamlaka na dhamana za uongozi walizopewa, kuhalalisha haramu, ni janga kwa mstakabali wa taifa letu,” alisema.Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Huvisa, hawakupatikana kuelezea juu ya tamko la Mdee.

Mawaziri hao walikaririwa kwa nyakati tofauti wakisema nyumba zote zilizojengwa kando kando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa.
Habari via Nipashe Jumapili



WOLPER AHOFIA KUUAWA

SAKATA LA KUMLIPUA DALLAS SASA AISHI KAMA DIGIDIGI.

Na Erick Evarist
SIKU chache baada ya mwigizaji ‘classic’ Bongo, Jacqueline Wolper Masawe kumlipua mchumba’ke, Abdallah Mtoro ‘Dallas’, inadaiwa kuwa mwigizaji huyo anaishi kwa ‘machale’ akihofia kuuawa kutokana na ukweli wa maisha yao aliouanika gazetini, Ijumaa Wikienda limeelezwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Dallas hakufurahishwa na sentensi za Wolper ambazo alizielekeza kwake huku akidai amemdhalilisha aliposema kuwa jamaa huyo hana chake na anatembea na nguo zake katika gari ili muda wowote amkabidhi.

“Kusema kweli sasa hivi Wolper anaishi kama digidigi, haonekani hovyo kama zamani, kama huamini mtafute awaambie,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya madai hayo kufika mezani, mwanahabari wetu alimwendea hewani Wolper kupitia kilongalonga chake cha mkononi ambapo alisisitiza alichokisema gazetini na alipobanwa kuhusu madai ya kuhofia kuuawa, aliishia kuguna na kumuomba mwandishi kuwa atamtafuta baadaye, lakini hadi tunakwenda mtamboni hakuwa amepiga simu.

MAADUI NO. 1 WA MABAKA NA VIDOTI DOTI VYA USONI

KARIBU AK CLASSIC COSMETICS SASA WANAPATIKANA KINONDONI MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.CONTACT: 0753482909/0713468393..OPENING HOURS: MON-SUN 900AM 
MABINGWA WA VIPODOZI VYA UKWELI
AK CLASSIC COSMETICS SASA WANAPATIKANA KINONDONI MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.CONTACT: 0753482909/0713468393..OPENING HOURS: MON-SUN 900AM -900PM.http://akclassic.blogspot.com/

WAFANYAKAZI WA BARCLAYS WAFANYA BONANZA LA MICHEZO

Wacheza  mpira kikapu  wa Benki ya Barclays Tanzania wakichuana ili kumpata mshindi  wakati wa bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Barclays Tanzania, wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Wasakata kabumbu wa Benki ya Barclays Tanzania, Paul Abduel (kushoto) na Stanslaus Mkondya (kulia) wakigombea mpira katika bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barclays wakiselebuka katika bonanza la Siku ya Michezo katika Viwanja vya UDSM jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina (katikati) akipozi kwa picha na timu iliyoibuka kidedea katika mchezo wa soka wakati  bonanza la Siku ya Michezo katika Viwanja vya UDSM jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akizungumza wakati wa bonanza hilo ambapo wafanyakazi hao walishiriki michezo ya kuvuta kamba, kabumbu, wavu, kikapu na kusakata dansi. 

3 held over two bombs found in bus headed to Nairobi

Police suspect that these recent bomb attacks are the work of the Islamic group of the Al- Shabaab
Monday 1st October 2012 - Police are holding three people in connection with the seizure of two bombs in a bus headed to Nairobi.


The officers handling the case said they are pursuing intelligence that the bombs were to be used in an attack at the Nairobi International ASK show that opens on Monday.

The bus was headed to Nairobi from Garissa when it was stopped at a roadblock in Matuu. All the 60 passengers on board disowned the luggage that had the two explosives. The suspects were arrested on Friday.

Yatta police commander Joel Sang said on Sunday that after interrogation, they zeroed in on the bus driver, conductor and a third man.

“They had hidden the explosives in tyre tubes. When we asked each passenger to pick his or her luggage, one bag remained unclaimed. It was opened and we discovered it had ingredients that, if assembled, could make two bombs,” said Sang.

He said the three are expected in court this morning. The police boss said investigation has shown that the home made bombs were loaded onto the bus in Mwingi town.

Yesterday a bomb exploded in ACK St Polycarp church along Juja road killing a child and seriously injuring eight others.


Kashfa nyingine yaibuka Tanesco

KASHFA mpya imeibuka ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya kubainika kuwa vikombe vya kufungia nyaya za umeme vyenye thamani ya mamilioni ya fedha vimetelekezwa kutokana na baadhi ya vigogo wa shirika hilo kushindwa kunufaika na mradi huo.
Habari kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa vigogo hao wanadaiwa kuvikataa vikombe hivyo kwa maelezo kuwa ni vibovu, baada ya mzabuni kushindwa kuwaona vigogo hao.Wakati vigogo hao wakivikataa vikombe hivyo kwa madai kuwa ni vibovu, taarifa zinaeleza kuwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamethibitisha kuwa vikombe hivyo ni vizuri na havina matatizo yoyote.Hatua ya Tanesco kupeleka vikombe hivyo kuthibitishwa na wataalamu wa Chuo Kikuu, Kitengo cha Uhandisi ilitokana na mvutano uliokuwapo baada ya vigogo walioshindwa kunufaika na mradi huo kutoa maelezo kuwa vikombe hivyo havina viwango bora.
Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa licha ya vigogo hao kuvikataa vikombe hivyo zaidi ya 40,000 vyenye thamani ya Sh900 milioni kwa madai kuwa vibovu, tayari shirika hilo limekuwa likivitumia katika nguzo zake zenye umeme mkubwa kwa miaka mingi.Mvutano wa viongozi hao ndani ya shirika hilo, umesababisha mradi wa kukarabati njia za umeme mkubwa bila ya kuzima umeme kwa kuondoa vikombe vilivyochakaa uliokuwa ukifanyika katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kusimamishwa mapema mwaka huu.Baadhi ya wataalamu wa Tanesco wanaeleza kuwa vikombe hivyo kama vitatumika vina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya kufunga vikombe vipya katika njia ya umeme mkubwa wa kutoka kwenye mtambo wa kuzalishia umeme wa Kidatu mkoani Morogoro hadi Ubungo jijini Dar es Salaam.Pia, kumalizia ukarabati wa njia ya umeme ya Arusha hadi Moshi mkoani Kilimanjaro iliyositishwa.   

Chanzo chetu kutoka ndani ya Tanesco kinaeleza kuwa vikombe vilivyopo katika njia ya umeme ya Kidatu hadi Ubungo  havijabadilishwa kwa miaka mingi hali ambayo inafanya umeme kupotea njiani kwa asilimia nyingi.Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Felschami Mramba alisema kuwa mikataba ndani ya shirika hilo ni mingi na kusisitiza kuwa hawezi kulijibu suala hilo mpaka atakapowasiliana na kitengo cha ununuzi cha shirika hilo.
“Kwa sasa sina maelezo ya kina ya mikataba, hasa kuhusu suala hilo unaloniuliza, lakini mpaka wiki ijayo nitakuwa nimefuatilia na kupata jibu sahihi,” alisema Mramba.Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulika Nishati, George  Simbachawene alisema suala hilo halijafika kwake.Simbachawene alisisitiza: “Mambo yanayofika katika ofisi yangu huwa kama malalamiko yanayoletwa na watu kutoka Tanesco na sehemu nyingine. Nikiyapata naanza kufuatilia ili kujua nini kinaendelea.”Alisema kuwa Tanesco ni shirika linalojitegemea katika utendaji wake wa kazi na ndiyo maana lina bodi yake, ambayo hukaa na kupanga mambo mbalimbali ya kufanya.“Wakati mwingine wizara inaingilia utendaji wa Tanesco kama tunaona kuna mambo hayaendi sawa, ila hili la ununuzi kwa kweli sijui kwa sababu halijafika ofisini kwangu kama lalamiko,” alisema Simbachawene na kushauri kuwa atafutwe Mramba.

Hoja ya kuvikataa vikombe hivyo ambayo imekuwa ikitolewa na baadhi ya vigogo hao wa Tanesco ni kwamba vikombe hivyo ni vizito na nguzo haziwezi kuvibeba, vibovu na kwamba havifai katika ule utaratibu wa kufanya matengenezo bila kuzima umeme. Tanesco imekuwa ikikumbwa na kashfa mbalimbali zikiwamo matumizi mabaya ya fedha za shirika kwa baadhi ya maofisa kutumia zabuni kujinufaisha.Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi William Mhando alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo.Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ilieleza kuwa Mhando alisimamishwa kazi pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. 

Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi wa Ununuzi, Haruni Mattambo.


Matatizo mengine ambayo yanadaiwa kuikumba Tanesco ni pamoja na uchakavu wa mitambo ya Tanesco, hujuma za miundombinu na kuingiwa kwa mikataba mibovu.Via www.mwananchi.co.tz

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate