EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 3, 2012

Uhakiki wa Vitambulisho vya Taifa waanza Ilala, Temeke

Uhakika wa majina ya walioomba kupatiwa vitambuliso vya taifa umeanza jijini Dar es Salaam katika wilaya za Temeke na Ilala.
                           Afisa Habari wa Nida, Thomas William
Mamlaka ya Taifa ya Utambuzi (Nida) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo waliendelea kufuatilia ripoti ya kuhakiki majina hayo kwa wale wasio na sifa za kupatiwa vitambulisho hivyo katika wilaya zote.Afisa Habari wa Nida, Thomas William, alisema jana kuwa Wilaya ya Kinondoni ndiyo haijaanza uhakiki huo.Alisema ripoti kamili ya vipingamizi mkoani humo itatolewa baada ya uhakiki kukamilika katika wilaya zote.Uandikishaji majina ya vitambulisho hivyo ulianza Juni, mwaka huu, mkoani humo, huku mikoa mingine ikisubiri.

UDSM yapokea fedha kutoka Bodi ya Mikopo

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimepokea fedha kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo chuoni hapo.Taarifa hiyo ilitolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utawala), Profesa Yunus Mgaya, wakati akizungumza  chuoni hapo jana.
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utawala), Profesa Yunus Mgaya
Alisema fedha za wanafunzi katika chuo hicho walianza kupokea kutoka HESLB tangu juzi na kwamba, kinachoshughulikiwa kwa sasa ni kukamilisha taratibu za hundi za fedha hizo.Profesa Mgaya alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza watawahi kupokea fedha zao endapo watawahi kusajiliwa mapema na kupewa kitambulisho cha chuo na Jumamosi wiki hii wataanza kupokelewa rasmi chuoni hapo.Alithibitisha kuwapo kwa uhaba wa hosteli kwa chuo hicho na kusababisha wanafunzi kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda, ambapo pia alidai ni makosa.Alisema kwa sasa chuo kina zaidi ya wanafunzi 14,000, wakati kina uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi wasiozidi 6, 849 sawa na asilimia 49 na kwamba, wanafunzi wa mwaka wa kwanza ndio wanaopewa kipaumbele.

Mkurugenzi wa Mawasaliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Rainfrida Ngatunga,
alisema fedha hizo hazijafika, lakini HESLB waliahidi wanazituma ndani ya wiki hii.Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Waisilamu, Sudi Mndeme, alisema fedha za malipo ya ada kwa wanafunzi zinapelekwa moja kwa moja katika uongozi wa chuo, lakini za kujikimu wanaingiziwa wanafunzi wenyewe, hivyo hana uhakika kama wameshapewa kwa kuwa chuo hicho kilifunguliwa jana.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Taaluma), Profesa Peter Gilla, alisema mpaka sasa kwao halijawa tatizo kwa kuwa chuo hicho hakijafunguliwa na wanatarajia kufungua Oktoba 15, mwaka huu.Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza kilisema kinao wanafunzi zaidi ya 1,000, ambao uwapo wao chuoni hapo unategemea upatikanaji wa mikopo kutoka HESLB.
Makamu Mkuu wa SAUT, Dk.Charles Kitima, alisema ingawa chuo hicho kimeshafungua, lakini HESLB iliahidi kupeleka fedha baada ya Oktoba Mosi, mwaka huu.“Ni kweli kwamba, serikali ilielekeza tusifungue vyuo kabla ya Oktoba Mosi, lakini sisi ni chuo binafsi tuna mipango yetu. Ndio sababu tulifungua tangu Septemba 25. Lakini kuhusu mikopo kwa wanafunzi, tuliambiwa tusubiri hadi baada ya Oktoba Mosi,” alisema.Hata hivyo, alisema ni mapema sana kuilaumu HESLB kwamba imechelewesha fedha za mikopo kwa wanafunzi kwa sababu iliahidi kufanya hivyo ndani ya mwezi mmoja baada ya Oktoba Mosi, mwaka huu.
Alisema kimsingi chuo hakiwezi kudai fedha hizo kutoka HESLB, badala yake chuo kitawadai wanafunzi, ambao kama watacheleweshewa fedha hizo ndio watakaoathirika.
“Tuna imani bodi itazingatia ahadi yake ili wanafunzi wasiathirike iwapo watacheleweshewa. Kimsingi wao ndio wanaopaswa kufuatilia sio sisi. Lakini tunaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema.Imeandikwa na Isaya Kisimbilu, Joyce Kakoko, Dar; George Ramadhan, Mwanza na Ashton Balaigwa, Morogoro.

Kesi ya Lema: Mawakili walumbana

Malumbano ya mawakili jana yalitawala kesi ya rufani iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema.Wakili wa Lema, Method Kimomogoro aliiambia mahakama kuwa iwapo madai ya wakili ya wajibu rufani, Alute Mughwai kwamba hati ya kukazia hukumu iliyomvua ubunge Lema, ni batili, basi mteja wake ni mbunge halali.
Kimomogoro alitoa madai hayo jana wakati akijibu pingamizi la awali lililotolewa na wakili Mughwai, aliyedai kwamba hati hiyo ina kasoro kubwa za kisheria ambazo inafanya rufani hiyo kuwa batili tangu mwanzo hadi mwisho wake.Kutokana na hoja hiyo, Kimomogoro aliiomba Mahakama ya Rufani ifute mapingamizi yaliyotolewa na Mughwai.Wakili Kimomogoro alitoa ombi hilo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na Jaji Mkuu, Mohammed Othman Chande, ambaye anasaidiana na majaji Natalia Kimaro na Salum Massati.

Pia, aliomba wajibu rufani walipe gharama za kuendesha kesi. “Tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na walioleta wawajibike kulipa gharama na kama mtaona inafaa basi kila upande ubebe mzigo wake iwapo hoja yao itazingatiwa,” alidai Kimomogoro.Rufani ya kesi hiyo iliyosikilizwa jana katika Mahakama Kuu Arusha,  ilikuwa ikisikilizwa pingamizi la awali, lililowasilishwa na wakili wa wajibu rufani, kwa niaba ya wateja wake, Musa Mkanga, Agnes Mollel na Hapines Kivuyo, ilivuta umati mkubwa wa watu kutoka karibu kila kona za jiji la Arusha.
Mapema wakili Mughwai alitaka rufani hiyo ifutwe kwa kuwa hati ya kukazia hukumu ilikuwa ina kasoro mbalimbali. Pia alitaka waomba rufani walipe gharama ya kesi hiyo pamoja na gharama za mawakili kwani wameihangaikia sana kesi hiyo.“Rufaa ambayo ipo mbele yenu ni batili kwa sababu imesimikwa kwa hati ya amri ya Mahakama Kuu ambayo ni batili, hiyo hati ni batili toka mwanzo hadi mwisho wake,” alidai.Aliendelea kuiambia mahakama kuwa kukosekana kwa muhuri wa mahakama katika hati hiyo ni hitilafu kubwa hata kama hati yenyewe ina saini ya jaji aliyeiandika.Alidai kuwa uwepo wa muhuri wa mahakama unaonyesha mamlaka na uhalali na nyaraka yenyewe na kwamba bila muhuri nyaraka hiyo ni karatasi ya bure.Mughwai hakukubaliana na hoja ya waleta rufaa kwamba hawahusiki na kasoro hizo isipokuwa  wanaohusika ni mahakama kwani wao walitakiwa kujiridhisha kwamba hati hiyo imekamilika.
Katika hoja nyingine ya pingamizi, Mughwai alidai kuwa hati hiyo haionyeshi tarehe iliyotolewa ingawa ipo tarehe iliyoandikwa.Aliieleza kuwa utaratibu huo unakwenda kinyume cha Kanuni ya 9 ya Masjala ya Mahakama Kuu na kuongeza kuwa hati hiyo haikuandikwa kwa muundo unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria.Akijibu mapingamizi hayo, Kimomogoro alidai kuwa mazingira ya shauri hilo yalikuwa ya kipekee baada ya kutolewa hukumu Mahakama Kuu na kwamba jalada la kesi lilipelekwa Dar es Salaam, kwa hiyo hawakuwa na nafasi ya kuangalia hati hiyo.Aliongeza kuwa wakili Mughwai katika pingamizi amekwepa au kuchenga kwa makusudi kuelezea kanuni mpya na uamuzi wa kesi zilizotolewa siku za hivi karibuni kwa kuzingatia kanuni hizo kuelezea haki za msingi.


Wakili Mwandamizi wa Serikali, Timon Vitalis, ambaye katika kesi hiyo anamwakilisha Mwanasheria Mkuu, lakini kama sehemu muhimu (necessary party) alimuunga mkono wakili Kimomogoro, kwa hoja kwamba hati ya kukazia hukumu inatolewa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (CPC) na  siyo chini ya Kanuni ya Masjala ya Mahakama Kuu, hivyo alitaka kama kuna mgongano basi CPC ndiyo itumike.Hata ukisema hati ya kukazia hukumu ina kasoro, basi anayepaswa kulaumiwa ni mamlaka iliyotoa hati hiyo na siyo wakili wa waomba rufani, hivyo mahakama ina jukumu la kutoa hati iliyo sahihi,” alidai.Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Jaji Mkuu Chande, aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine ambayo watapanga.


“Uamuzi utatolewa kwa tarehe ambayo mtaarifiwa,”  alisema Jaji Chande.
Aprili 5, mwaka huu, Mahakama Kuu Tanzania Kanda Arusha,  ilitengua matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi Lema baada ya kuridhika kuwa alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Dk. Batilda Burian.Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila, baada ya kumtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne aliyokuwa akikabiliwa nayo, huku akitupa mawili kwa kukosa ushahidi.Jaji Rwakibarila alimvua ubunge Lema baada ya kuridhika na ushahidi kuwa alitumia maneno ya kashfa na ubaguzi wa jinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Burian.Pia Jaji Rwakibarila katika hukumu yake hiyo, alimwamuru Lema kulipa gharama za kesi hiyo.Hata hivyo, alimweleza kuwa ana haki ya kukata rufaa ikiwa ataona hakuridhika na hukumu hiyo.
CHANZO: NIPASHE

Watanzania sasa kupata Bima kupitia huduma ya M–Pesa.


Picture
  • Ni ushirikiano kati ya Vodacom na Heritage Tanzania kuzindua bima ya Faraja, Bima ya mazishi na ajali.
  • Wateja kununua na kulipia Bima kupitia M-Pesa.
  • Huduma ya bure kutolewa kwa wateja watakaolipia huduma mara kumi kwa Mwezi.

Dar-es Salaam, Octoba 3, 2012--- Huduma ya Vodacom ya M-Pesa imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha Watanzania kufanya malipo yao ya bima kupitia huduma hiyo.

Hii inafuatia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania kuzindua Bima ya Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa kulipwa fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo ya kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza huduma ya vifo vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao. Ongezeko hili la ziada litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko dogo la malipo.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure kwa mwezi.“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa walau mara 10 kwa Mwezi watapata bima ya bure ya kiasi cha Shilingi laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna haja ya kujaza fomu ili kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia rahisi kwa kupiga *150*00# na kuchagua kipengele cha bima.Vodacom inahakikisha kuwa wateja wote wa M-pesa wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani ndani ya familia zao.

“Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa zako ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa zako zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza na kuongeza kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji na bajeti yako,”Bima hii ya Faraja pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza kiwango chake kwa ile enye faida zaidi kulingana na mahitaji yao na mabadiliko ya bajeti katika maisha yao.Kwa taarifa zaidi kuhusiana na huduma mteja atapiga 0764 300001 bure au vipeperushi kutoka kwa wakala wa M-Pesa nchini.

Ni nani kati ya Simba na Yanga atajichukulia points leo pale uwanja wa Taifa?

Watu kumi wa mwanzo watakao sema nani atashinda na kwa mabao mangapi watapata vocha ya elfu 50,000!!! Kila la kheri!

KAULI YA LEO: FERGUSON NDIO BOSI WA MAKOCHA WOTE - ASEMA JOSE MOURINHO

"Kitu kizuri kuhusu kuwepo pale (kwenye Premier league) ni kufundisha, kwa sababu nafikiri soka itapoteza vitu vingi sana mara Sir Alex Ferguson atakapoacha kufundisha na hakuna makocha wengi vijana wala wazee. 
Kwangu mimi, Fergie ndio boss. Namuita Sir Alex bosi kwa sababu ndio bosi wa makocha wote na ninatumaini kwamba nitakapoenda tena kwenye soka la England atakuwa bado anaifundisha Manchester United." 

Jose Mourinho, jana akimwelezea Sir Alex Ferguson wakati akihojiwa na CNN.

Ajali ya basi la Dar Express iliyotokea Segera, Tanga siku ya jana

Basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali ya kuungua na kuteketea kwa moto siku ya jana asubuhi katika eneo la Segera kwenye njia panda ya Dar es Salaam-Arusha-Tanga.Basi hilo lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam likiwa na abiria sitini na tano.

Imeripotiwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa au kupoteza uhai katika ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ambayo iliteketea.Basi hilo lilikuwa na wanafunzi. Askari usalama wa barabarani aliyekuwa zamu katika eneo hilo aliona moshi ukitoka na mara moja akawaamuru abiria wote kushuka. Muda mfupi baadaye gari hilo lilishika moto. Gari la zimamoto kutoka Korogwe lilikuwa likitarajiwa kufika katika eneo hilo kutoa msaada wa kudhibiti moto huo.
Picture
(picha hii moja, ni kutoka kwenye blogu ya TangaYetu)
Picture
Picture
Picture
Basi la Dar Express baada ya kuteketea kwa kuungua moto (picha hii moja imepatikana via Michuzi blog)

Tuesday, October 2, 2012

BREAKING NUUUZ; AJALI MBAYA IMETOKEA MUDA SI MREFU ENEO LA MBALIZI MBEYA, MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO .


WATU NANE WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO.


 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYE VAA SUTI YA BLUE MH. ABASS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI
 HIVI NDIVYO HILI GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI
 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI

WATU NANE WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO.

CHANZO CHA HABARI mbeyayetu.blogspot.com

Watoto Wa Wassira Kujiunga CHADEMA; Ufafanuzi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU 

Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. 

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. 

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. 

CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. 

Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1). Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira.

 Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Lilian Wasira 0719 604156 Esther Wasira 0655 048797

Mwendelezo wa kusikilizwa Rufaa ya Lema - Oktoba 02, 2012

Judge Chande: Amepokea hoja za pande zote mbili kwa ajili ya hoja za awali, uamuzi utatolewa kwa tarehe ambayo tutaarifiwa.

Tumefika mwisho wa kikao cha rufani. anashukuru wote. wamesikiliza shauri 36 za rufani hapa Arusha. 

Tunaahirisha mahakama panga tarehe itakayopangwa tena!
KESI IMEAHIRISHWA!


Chande: 
Leo waanasikiliza pingamizi za awali kwanza


Kabla hatujaanza kusikiliza, mawakili wote wawe na right of audience.


Kimomogoro: Upande wa rufani tuna uhalali wa kusimama mbele ya rufaa kwa zaidi ya miaka kumi


Alute: Nina uhalali tangu 1985


Lissu: Nimekuwa wakili tangu 2003, hivyo nina zaidi ya miaka mitano.


**************

Majaji naona wanashauriana baada ya kusikiliza maelezo ya TL kuwa ana haki ya kusikilizwa kwenye mahakama hii tukufu

Alute: Rufaa ni batili on a decree of the high court. Decree haikubaliani na hukumu.


Reference to page no 957/958 kifungu cha 14 sheria ya uchaguzi. Mkurugenzi wa uchaguzi azingatie sheria ya uchaguzi.

Decree haijaandikwa kama inavyotakiwa na sheria.Na katika hili tumeambatanisha hukumu ya mahakama hii tukufu iliyotolewa mwezi wa tano dhidi ya Gesud Bajuta.

*************

Kesi hii imeelekeza kuwa hii decree inatakiwa iwe na format ipi. Kwenye ukurasa wa sita hadi nane.

Kwenye hii kesi tar ya decree ilikuwa imekosewa. Haya ni maelezo ya Alute yanaendelea.


Mahakama ilikumbushia umuhimu wa kuzingatia decree.Kesi iliyopo mbele yetu decree imekosewa, haina baadhi ya maneno kama given under my hand in a seen of the court.

Decree haionyeshi ni lini imechukuliwa. Imekiuka kanuni ya tisa ya kanuni ya masijala ya mahakama.Kanuni ya tisa "All summons shall be seen of the court. And should show when the order was distracted"

*************

Alute: Hii decree ina hitilafu, amekiri kuwa ina saini ya jaji, lakini haina muhuri wa mahakama. Bila muhuri mheshimiwa, hii decree is like a piece of paper. Decree lazima iwe kwenye formalities, na moja ya hiyo formalities ni lazima decree iwe na muhuri to show the seen of the high court. Sign peke yake haina maana.Hii decree ni batili si makosa ya waleta rufaa bali makosa ya mahakama. Lakini pia waleta rufaa walitakiwa kuchunguza vizuri makaratasi kama yamekidhi rufaa.Kwakuwa hii decree ni batili, basi na rufaa nayo itakuwa batili.


Chande: Alute elewa kwamba mwisho wa siku ni mambo ya mamlaka. Na aliyetoa hukumu ni jaji Rwakibarila, rufani ilisainiwa na yeye. Bado unabisha kwamba siyo mamlaka ya ofisi ya mahakama?


Alute: Bila muhuri wa mahakama the answer is no!


Chande: Kuhusu kasoro ya muda, order twenty sect. 7 haionyeshi suala la muda. 


Alute: Lina uzito mheshimiwa, kwa sababu hakuna certificate of delay.


Chande anamwuliza Alute kwa maoni yake kama ameona ni batili, atoe ushauri wa adhabu mbadala.


Alute anasema kuna makosa huwa hayana adhabu mbadala.


Kweli hii kesi ya uchaguzi uchaguzi, lakini mahakama hii kwa kukosa decree of the court ilifuta kesi ya Fortunatus Machana, panga hilo hilo litumike kwenye rufaa hii.


***************

Kimomogoro: 

Ningeanzia alipoishia Alute. Anasema mwenyewe aliandika barua kuomba decree haikujibiwa. Kama yake haikujibiwa ya kwetu ingejibiwa vipi?Mtaona kwamba drawn order imekuwa sealed. You need circumstance kusikiliza shauri hili.arua alizoomba corrective decree iliomba point no 4, haikuzungumzia lingine.Msomi mwenzetu alisema marekebisho haya ili ayatumie kwenye shauri hili. Kwa bahati mbaya barua zote hazikunukuliwa kwetu.


Msomi mwenzangu amesema hakukuwa na wajibu wa kuensure the record proper. Wakati kanuni zinamwelekeza hivyo.Waheshimiwa tunaomba muelekeze kama mlivyomwelekeza msomi mwenzangu.Alute hajazungumzia authorities tulizoambatanisha zinazoelezea kusahihisha decree. Tunaamini amechenga kwa makusudi 


Kimomogoro:ukumu ni la jaji aliyetoa uamuzi kuhakikisha kuwa decree imetengenezwa. Tumetoa pia kesi ya mausi vs Arusha general store. Mahakama ilitoa mwongozo kuhusu aina ya kanuni, moja ni mandatory na directory.Mahakama ilisisitiza kwamba kanuni za mwongozo hazitaathiri muendelezo wa kesi. Kasoro zilizotajwa kwenye hiyo zote ni clerical error.Makosa mengine ni ya muundo 'given under my hand in a seal of the court' na date of extraction, imefutwa na GN no 6 ya mwaka janaMheshimiwa jaji aliridhika ni hii decree, akaweka mkono wake, kwahiyo imekamilika. Kama jaji aliridhika kimakosa, sisi hatuna makosa.Kuhusu reg. Rule inahusika na masijala. Decree ikishapata sign ya jaji kinachofuata ni kusikilizwa.Kama decree ni batili basi Mteja wetu bado ni mbunge wa Arusha, kwasababu hakuna kilichomtengua.

**************

AG rep. Anataja sifa za pingamizi la awali, na hii rufaa imekamilisha hilo katika hoja za maandishi ali refer kesi ya manufacturing limited na distributors ltd. ktk kesi hii iliyokuwa mahakma ya africa mashariki ilitoa mifano kuwa shauri ilikuwa nje ya muda, au kwamba wadai walitakiwa shauri ingepelekwa kwney arbitration.Mahakama ya rufani hapa ilizungumzia preliminary objection, hapa shauri linaamuliwa bila kulirudisha mahakamani. Kama alivyopendekeza Mughwai kuwa wakajipange upya.Anasema kuna pingamizi ambazo zinaongeza gharama, hivyo kama alivyopendekeza Alute kuwa wakajipange upya, ni kujiongezea gharama zingine.

Dar Express Lililokuwa Likitokea Arusha Kwenda Dar Es Salaam La Waka Moto.

Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema watu 65 wamenusurika kufa eneo la Segera Mkoani Tanga baada ya basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar Es Salaam kuteketezwa na Moto. Picha kwa Hisani ya Jamii Forums

MITIHANI YA KIDATO CHA SITA NA NNE YABADILISHWA TAREHE 2013

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mithihani la Tanzania (NECTA) anapenda kuwatangazia watahiniwa wote wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2013 kuwa, kufuatia mabadiliko ya mihula yaliyofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mtihani wa Kidato cha Sita uliokuwa ufanyike mwezi Februari 2013 sasa utafanyika mwezi Mei 2013. 


HIVI NDIO VIINGILIO VYA MECHI YA SIMBA NA YANGA SIKU YA KESHO

KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano kesho (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.
 
Release No. 159, TAARIFA YA TFF , Oktoba 1, 2012
Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni.
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
Wakati huo huo, mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Meli Mpya Ya Azam Yenye Uwezo Wa Kubeba Watu 1000 Na Magari 200 Yawasili Nchini.

Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake. 
                                         Azam sea link1
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali. Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika. Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari. Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba. 
                                         Muonekano wake ndani.
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara. 
Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.Habari na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate