EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 2, 2013

BABY MADAHA NA WOLPER WAMALIZA BIFU LAO.

WASANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ na Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ wamemaliza bifu lao lililokuwa likifukuta kama moto wa kifuu mwishoni mwa wiki mbili zilizopita.
Akizungumza na mwandishi  wetu katikati ya wiki hii, Baby alisema alikuwa Mkoani Geita kwa ziara ya kikazi lakini alipigiwa simu na Wolper akimuomba msamaha kutokana na tofauti zao zilizosababishwa na nyumba ya kupanga.
“Nimeona bora yaishe kwa sababu Wolper amekubali kosa na mimi siwezi kuendeleza bifu lakini kama asingeniomba msamaha tungefikishana mbali,’’ alisema Baby Madaha na kuongeza:
“Nimemalizana na Wolper ila kesi itabaki kwa mwenye nyumba, nitapambana naye hadi atakaporejesha mkwanja wangu japokuwa nimepata nyumba nyingine maeneo ya Mikocheni.”

FACEBOOK WAMEKUJA NA "VERIFIED ACCOUNT " NA RAIS UHURU AWA WA KWANZA.

Facebook imefuata mkondo Twitter kwa kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/accounts) ili kuwawezesha watu mashughuli kuthibitisha akaunti akaunti na fan page zao. Facebook wamesema wamefanya hivyo ili kusaidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za mastaa na watu wengine mashughuli wanaotumia mtandao huo, pia ikiwemo biashara zenye majina makubwa.

Kurasa zilizothibitishwa zitakua na alama ya blue ya pata “check-mark” kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Watu wataoruhusiwa kutumia huduma hiyo ni, viongozi wa serikali, waandishi wa habari maarufu, makampuni au bidhaa maarufu. Hivyo kuanzia sasa, utaweza kufahamu akaunti/pages zipi ni za kweli na zipi ni feki.

MABADILIKO: MWILI WA NGWEA UTALETWA JUMANNE NA SIYO LEO.


 Mwili wa ngwea  utaletwa Tanzania siku ya jumanne  na  siyo  LEO.

Taarifa hizi nikwa mujibu wa tweet alotweet Millard Ayo aliyeko nchini africa kusini ulipo mwili wa marehemu Ngwair

WANYARWANDA WANASWA BONGO WAKIJIUZA USIKU POLISI WAWAPA KIBANO.


Stori:Richard Bukosi
POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi, Risasi Jumamosi  lina cha kushika mkononi.
Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.

Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 2//06/2013

Saturday, June 1, 2013

ILLUMINATHA DOMINICK NDIYE REDD'S MISS MULEBA 2013 KUTOKA RUBYA.


Mshindi wa Redd's Miss Muleba Illuminatha Dominick akitabasamu mara baada ya kutangazwa usiku.( Habari na Bukobasports.com).
Mshindi wa pili kushoto Linah Mutayoba na kulia ni mshindi wa wa tatu Fransisca
                                                Kujificha kwa tabasamu ni vigum.
Babylove Kalalaa ndiye aliyekuwa ameshikilia taji na sasa ameliachia Illuminatha kwa mwaka huu 2013.

Kampuni zamneemesha Neymar

LONDON, ENGLAND
WAKATI nyota wa Brazil, Neymar, akisubiri kutambulishwa rasmi kwenye kikosi cha Barcelona keshokutwa Jumatatu, habari mpya ni kuwa nyota huyo ameshukiwa na neema baada ya kampuni inayomiliki matangazo ya David Beckham kuingia naye mkataba wa haki za picha.


Mkataba huo utamfanya kuwa nyota anayelipwa fedha nyingi kutoka Brazil.
Simon Oliveira ambaye ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya Doyen Group, alisema Neymar amesaini mkataba utakaodumu mpaka mwaka 2017. 
Oliveira alisema kampuni hiyo itakuwa na kazi ya kusaka wadhamini kwa ajili matangazo ya picha ya Neymar nje ya Brazil.

Neymar ambaye amesaini mkataba wa kujiunga na Barcelona ni mchezaji wa tano kwa kupata fedha nyingi miongoni mwa wanasoka ambapo anapata kiasi cha Euro 20 milioni kwa mwaka.

“Kazi yetu ya kwanza itakuwa ni kutengeneza jina la Neymar huko Asia, tunaamini tutapata mafanikio,” alisema Oliveira. 
Neymar tayari ana mikataba na kampuni kadhaa za Brazil ikiwa ni pamoja na kampuni ya Nike Inc.

Imefahamika kuwa kampuni zimemiminika kutaka kufanya naye kazi baada ya kubainika kuwa nyota huyo ana marafiki zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kitendo cha kuhamia Barcelona pia kimempa nafasi ya kusakwa na kampuni zaidi.

Anti Suzy: Haya ndiyo machungu ya ushoga.

Vitendo vya Ibrahim Mohamed Anti Suzy havikuwapendeza watu wengi hasa wanaume. Alipingwa mitaani, barabarani na maisha yake yakawa ya kujificha mithili ya panya.

“Niliwahi kupanga nyumba karibu na msikiti, majirani na viongozi wa msikiti wakaamua kunifukuza wakasema nitawafundisha watoto wao tabia mbaya. Wakanirudishia kodi yangu nikaenda kupanga chumba kingine”anasema

Si hivyo tu, bali anazomewa barabarani, kutukanwa, wakati mwingine watu kukataa kumpa mikono au hata kumsaidia anapougua.

Anti Suzy anasema, moja ya tabu zake kuu ni kuingiliwa na wanaume na kubakwa mara kwa mara jambo ambalo linamkosesha raha hasa ukizingatia nyumba yake ni chakavu.
“Juzi waliniingilia wanaume wanne, walifika usiku saa tisa, wakasukuma mlango kwa nguvu, wakanibaka wote,” anasema.

Kijana huyu anasema pamoja na kuwa na tabia za ushoga, mwendo wake, sauti na jinsi alivyo havifichi kubaini kuwa ni mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Anasema anapovaa mavazi ya kiume, ndipo watu humshangaa kwani anakuwa na sura ya kike, mwendo wa kike, sauti ya kike kasoro mavazi tu.
“Lakini nikivaa khanga au sketi ndefu, hakuna mtu anayejua kuwa mimi ni mwanamume na nimeshawahi kupata mwanaume alidhani mimi ni mwanamke alipofika chumbani alitimua mbio” anasema.

Mwaka 2010 Anti Suzy alikwenda kupima virusi Vya Ukimwi na hapo alipewa majibu yaliyomshtua ambayo hata hivyo hakuyaamini majibu hayo.
Anasema hakuweza kuamini majibu ya kuwa ana VVU kwa sababu alikuwa na afya njema, alikuwa haumwi chochote kile.
“Nilipima hospitali zaidi ya tatu, Bugando, Muhimbili na Kilimahewa na majibu yalikuwa yaleyale kuwa ni nimeathirika” anasema
Anti Suzy hata hivyo hakuacha tabia hiyo, aliendelea akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kujipatia kipato chake cha kila siku, hadi mwaka jana hali yake ilipokuwa mbaya zaidi.

BASATA yatoa salamu kifo cha Ngwair.

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeelezea kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya muziki nchini, Albert Mangwea ‘Ngwair’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, baraza limeshtushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo cha Ngwair, ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.

Materego alisema baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
“Tunaomba Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu,” alisema Materego.

Mwalimu mbaroni kwa kumtorosha mwanafunzi

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia Mwalimu  Ased Job (31) kwa  kumtorosha  mwanafunzi  wa  kike mwenye umri wa miaka 17  kisha kuishi naye kinyumba kwa zaidi ya miezi  miwili sasa.

Mwalimu  huyo  ambaye  anafanya  kazi  katika Idara  ya Elimu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga  anatuhumiwa kuishi  na  mwanafunzi  huyo  anayesoma  kidato  cha pili  kama  mkewe  kwa kipindi  hicho  chote.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Peter Ngusa,  akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alisema lilitokea  Februari  mwaka  huu  baada ya mtuhumiwa kumtorosha  mwanafunzi  huyo na kumpeleka  mkoani Mbeya kisha kufanya taratibu za uhamisho kwa lengo la kumhamishia mkoani Mbeya ili akaishi naye huko.

“Baada ya kukamilisha uhamisho  huo mwanafunzi huyo alihamia mkoani Mbeya kisha akaanza kuishi  na mwalimu  huyo  kinyumba  hadi  mwisho  mwa  Mei  mwaka huu  alipomrejesha  mjini  Sumbawanga  na kuendelea  kuishi  naye kinyumba kisha baadaye kukamatwa,” alisema.

Mwili wa Mangwea sasa kesho

MWILI wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ sasa unatarajiwa kuwasili nchini kesho badala ya leo kama ilivyotaarifiwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya mipango ya mazishi ya msanii huyo iliyotolewa jana inayoongozwa na Kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea, mwili huo utawasili Jumapili majira ya saa 8, mchana na kisha kufuata taratibu zingine.

“Mwili utafika nchini siku ya Jumapili majira ya saa nane mchana na sio Jumamosi (leo), kama ilivyotaarifiwa hapo awali,” ilieleza taarifa hiyo.
Sababu za mabadiliko hayo, imeelezwa ni kutokana na Watanzania waishio Afrika Kusini, kuomba kutoa heshima za mwisho, Jumapili.

Kwa hatua hiyo, kamati ilibainisha kuwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani, watapata nafasi ya kuuaga mwili Jumatatu majira ya saa 2 asubuhi hadi 6 mchana na baada ya hapo, wataelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi, Jumanne.
Aidha, kamati iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, huku ikiomba wadau kuendelea kuwaombea kufanikisha salama shughuli hizo za mazishi.

Kesi yaiweka pabaya TFF

KESI iliyofunguliwa mkoani Pwani dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeonekana kuliweka pabaya shirikisho hilo, ambalo hivi sasa linahaha ifutwe.

TFF imeburuzwa mahakamani mjini Kibaha na mdau wa soka, anayejulikana kama Babu Adam ambaye alifungua kesi Mei 30 mwaka huu, na kusimamiwa na Daniel Ngasa wakitaka haki dhidi ya Kiluvya United, iliyopokwa ubingwa wa mkoa wa Pwani.
Kamati hiyo, iliamua kuivua ubingwa Kiluvya United, baada ya kupokea malalamiko kutoka timu ya Al Etihad ya Mafia, ambayo ilikuwa mshindi wa pili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni, alisema wamekitaka Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (Corefa), kifute kesi hiyo kwa manufaa ya soka la Tanzania.
Kayuni ambaye pia ni Mkutugenzi wa Ufundi wa Shirikisho hilo, alisema, tayari amekiandikia barua chama hicho, kukiagiza kishirikiane na mdau huyo kufuta kesi hiyo kabla ya saa 11 jioni ya jana ili kuondoa uvunjwaji na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za katiba ya Corefa na TFF.

Wengi wafaulu kidato cha sita

Dar es Salaam.
Baraza la Mitihani Nchini (Necta), limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo asilimia 87.85 wamefaulu huku kundi la shule 20 za mwisho likitawaliwa na shule kongwe nchini na zile za Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde, alisema watahiniwa 50,611 walifanya mtihani huo na kati yao 44,366 sawa na asilimia 87.85, wamefaulu.
Mwaka 2012 wanafunzi waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.


Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2013, kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Watahiniwa wa shule
Dk Msonde alisema kuwa, watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani huo.
“Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana 26,956 sawa na asilimia 93.03,” alisema.
Mwaka 2012 watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 walifaulu mtihani huo.
Watahiniwa wa kujitegemea
Alisema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani huo walikuwa ni 7,659 na waliofaulu ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.
Ufaulu katika kundi hili umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 5,883 sawa na asilimia 64.96 ya wote waliofanya mitihani hiyo.
Ufaulu kwa madaraja
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, watahiniwa 325 sawa na asilimia 0.76 ya wote waliofanya mtihani huo walipata daraja la kwanza, kati yao wavulana wakiwa ni 188 sawa na asilimia 0.65 na wasichana 137 sawa na asilimia 0.99.

Waliopata daraja la pili ni 5,372 sawa na asilimia 12.54 wavulana wakiwa ni 3,142 sawa na asilimia 10.84 na wasichana 2,230 sawa na asilimia 16.08. Waliopata daraja la tatu ni 30,183 sawa na asilimia 70.45 wavulana wakiwa ni 20,442 sawa na asilimia 70.55 na wasichana 9,741 sawa na asilimia 70.24.
Watahiniwa waliopata daraja la nne 4,362 sawa na asilimia 10.18 ya wote waliofanya mtihani huo huku wavulana wakiwa ni 3,184 sawa na asilimia 10.99 na wasichana 1,178 sawa na asilimia 8.49.
Waliofeli ni 2,604 sawa na asilimia 6.08 wavulana wakiwa 2,021 sawa na asilimia 6.97 na wasichana 583 sawa na asilimia 4.20.

Shule za Zanzibar zaboronga
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, shule kutoka Zanzibar zimefanya vibaya ambapo katika kundi la shule 10 za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 30, saba zinatoka kwenye visiwa hivyo.
Kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 30, nne zinatoka Unguja huku shule nyingine kongwe zilizokuwa zikifanya vizuri mwaka huu zimevuta mkia.

Kwa upande wa shule 10 za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 30 ya kwanza kutoka mwisho ni Pemba Islamic College (Pemba), Mazizini (Unguja), Bariadi (Simiyu), Hamamni (Unguja), Dunga (Unguja), Lumumba (Unguja), Osward Mang’ombe (Mara), Green Acres (Dar es Salaam), High View International (Unguja) na Mwanakwerekwe (Unguja).

Shule zilizofanya vizuri zenye watahiniwa chini ya 30, ya kwanza kutoka mwisho ni Mbarali Preparatory (Unguja), Philter Federal (Unguja), St Mary’s (Dar es Salaam, Mzizima (Dar es Salaam), Hijra Seminary (Dodoma), Tweyambe (Kagera), Mpapa (Unguja), Al-Falaah Muslim (Unguja), Presbyterian Seminary (Morogoro) na Nianjema (Morogoro).
 
Shule zilizofanya vizuri
Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa chini ya 30, ya kwanza ni Palloti Girls (Singida), St. James Seminary, Parane na Sangiti (zote Kilimanjaro), Itamba (Njombe), Masama (Kilimanjaro), Kibara (Mara), St.Luise Mbinga Girls (Ruvuma), St. Peters Seminary (Morogoro) na Peramiho Girls (Ruvuma).

Shule 10 bora katika kundi lenye watahiniwa zaidi ya 30, ya Kwanza ni Mariani Girls (Pwani), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), Iliboru na Kisimiri (zote kutoka Arusha), St Mary’s Mazinde juu (Tanga), Tabora Girls (Tabora), Igowole (Iringa), Kibaha (Pwani) na Kifungilo Girls (Tanga).
Waliofaulu Sayansi

Waliofaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi na michepuo yao kwenye mabano ni Erasmi Inyanse kutoka Iliboru (PCM), Maige Majuto kutoka Kisimiri Arusha (PCM), Gasper Mung’ong’o kutoka Feza boys Dar es Salaam (PCM), Gasper Setus kutoka St. James Seminary Kilimanjaro (PCM) na msichana pekee kwenye kundi hili aliyeshika nafasi ya tano ni Lucylight Mallya kutoka Marian Gils Pwani (PCM).
Waliofaulu Biashara
Kundi hili linaongozwa na Eric Robert Mulugo Tusiime Dar es Salaam (ECA), Alicia Filbert kutoka Shule ya Ngaza Mwanza (ECA), Evart Edward, Kibaha Pwani (ECA), Annastazia Renatus Tambaza Dar es Salaam (ECA), Peterson Meena Mbezi Beach Dar es Salaam (ECA).
Lugha na Sayansi ya Jamii
Wa kwanza ni Asia Idd Mti kutoka shule ya Barbro-Johansson ya Dar es Salaam (HGE), Godlove Geofrey Ngowo kutoka shule ya Majengo Kilimanjaro (EGM), Jonson Elimbizi Macha kutoka shule ya Njombe iliyopo Njombe (EGM), Hamisi Joseph Mwita Iliboru Arusha (HGL) na Sia Sand Marian Girls Pwani (EGM).
Matokeo yaliyozuiliwa na kufutwa
Dk Msonde alisema kuwa, Necta imezuia matokeo ya watahiniwa 116 kutoka na sababu mbalimbali, 93 hawakulipa ada ya mtihani, 10 walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya mitihani na 17 walipata matatizo ya kiafya na hawakufanya mtihani hata mmoja.
Alisema pia kuwa, baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa wanne kutokana na kubainika kufanya udanganyifu, kati yao mmoja akiwa ni mtahiniwa wa shule na watatu wa kujitegemea.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate