EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 2, 2013

Utata manispaa ya Kinondoni baada ya kutakiwa kulipa sh 695,520,000 kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imejikuta njia panda baada ya kutakiwa kulipa sh 695,520,000 kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota ikiwa ni pango la kodi kuanzia Januari hadi Desemba mwaka huu.

Halmashauri hiyo iliingia mkataba na wakazi hao Septemba mwaka 2011 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ambapo ilikubali kuwalipia pango la chumba wakazi hao kuanzia mwaka huu hadi pale nyumba za eneo hilo zitakapokamilika.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, mmoja wa watendaji wa halmashauri hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alisema kuwa malipo hayo yamesababisha migongano baina ya viongozi wa manispaa na baraza la madiwani.

Alisema kuwa kuliibuka mvutano mkubwa katika kikao cha baraza la wadiwani ambapo baadhi walipinga mkataba huo na wameshauri malipo hayo yasitishwe ili hatua za kisheria zichukuliwe.

“Hivi ninavyokwambia kuna sintofahamu juu ya malipo hayo maana wakazi hao wana mkataba halali unaotambuliwa na mahakama na hata baraza la madiwani linafahamu hilo ndiyo linajaribu kupigania mkataba huo uvunjwe ili fedha hizo zitumike kwa shughuli nyingine,” alisema.

Serikali yazidi kuandama magazeti..Yakerwa na Mwananchi kuonekana mtandaoni.

KWA mara nyingine serikali imeendelea kuandama vyombo vya habari viwili ilivyovifungia wiki iliyopita, magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.
 
Jana ilitishia kuchukua hatua kali dhidi ya gazeti la Rai (dada wa Mtanzania) ikisema iko tayari kulifunga iwapo litaendelea kuchapishwa katika siku tofauti na Alhamisi.
Kupitia kwa Mkurugenzi wa Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, serikali jana ilisema haitaki kuliona gazeti la Mwananchi mtandaoni kama ambavyo hailitaki mitaani.
Mwambene alipiga marufuku magazeti hayo kuonekana popote, kwa njia yoyote, kabla hayajamaliza kifungo.

Mwambene alisema kuwa gazeti la Mwananchi baada ya kufungiwa limeendelea kutoa habari zake kupitia tovuti ya gazeti lao kinyume cha amri iliyotolewa na kwamba serikali imewaandikia kuwataka kuacha mara moja la sivyo watalazimika kuchukua hatua kali zaidi.
“Kampuni ya New Habari 2006 baada ya kufungiwa moja ya magazeti yake, imeanza  kuchapisha gazeti la ‘Rai’ kila siku tangu  Septemba 29, mwaka huu bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti,” alisema.

Hata hivyo, amri ya serikali ya kuzuia Rai kutoka kila siku hasa baada ya Mtanzania kufungiwa siku nne zilizopita, imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa New Habari.

IRENE UWOYA ATANGAZA RASMI KUACHA KUIGIZA MUVI.

Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.  

Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
 
Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.
 
Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.
 
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.

JOHN BARNES NA LUCAS RADEBE WAWASIHI VIJANA KUWA NA MAPENZI YA MCHEZO KABLA YA KUANZA KUWAZA PESA.

Wanasoka wa zamani John Barnes na Lucas Radebe wamesema siri kubwa ya mafanikio yao katika mchezo wa soka ilikuwa ni kutoweka mbele masilahi binafsi kama ilivyo kwa vijana wa sasa, wameyasema maneno hayo siku ya jana kwenye kongamano la SOCCEREX linalofanyika kwenye uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban.

Lucas Radebe na John Barnes walipokuwa wanahojiwa na mtangazaji wa Supersport Carol Tshabalala.

Beki wa zamani wa vilabu vya Kaizer Chiefs,Leeds Utd ya England pamoja na kikosi cha Bafana Bafana Lucas Radebe amesema wakati anachipkia kwenye mitaa ya Soweto yeye na vijana wenzake walikuwa wakiugombania mpira mmoja uliokuwa unamilikiwa na kijana mwenzao mtaani kwao, '' hatukuwa tunacheza ili tupate pesa pamoja na umaskini mkubwa uliokuwa unatukabili,bali mapenzi tuliyokuwa nayo juu ya mchezo wa soka ndio yalitusukuma sana kuucheza mchezo huo ''.

HAYA NDIYO MANENO ALIYOANDIKA WEMA SEPETU BAADA YA KUCHAFULIWA NA GAZETI LA FILAMU.

clip_image003            C.E.O wa kampuni ya Endless Fame Film maarufu kama Wema Sepetu ameonekana kuchukizwa na kitendo cha kuchafuliwa kwa jina lake katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini.
 
Mapema asubuhi ya siku ya jana kupitia account yake ya Instagram mwanadada Wema alitupia picha ya gazeti hilo lililo mchafulia jina kwa kumuandika kuwa "Wema Kunyongwa China Awaomba Watanzania Wamuombee".Pia dakika chache zilizopita kupitia account yake hiyohiyo ya Instagram wema amefunguka zaidi kwa kitendo hicho cha kuchafuliwa jina na kuandika hivi ...
Soma hapa chini ...

Tuesday, October 1, 2013

JACK DUSTAN MCHARUKO UGHAIBUNI.



STAA wa Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dustan ameonyesha tabia za mcharuko akiwa pande za Dubai  kwa kupiga picha katika mikao tata na mrembo mmoja aliyejulikana kwa jina la Mwajabu Juma.

Jacqueline ambaye ametimkia nchini humo hivi karibuni, amezua zogo mtandaoni baada ya wadau mbalimbali kumponda kwa kuonesha tabia chafu katika nchi za watu. Alipouulizwa kuhusu picha hiyo kuzagaa mtandaoni, hakujali:
 

“Jamani Wabongo msione jambo, sasa hii picha hapa ina ubaya gani? Mbona ni pozi tu la kawaida tu wala sioni kitu chochote ambacho kinaweza kuwashangaza,” aliandika Jacqueline. 

Ray C aja na ‘Roho Imechagua Wewe Pekee’.

BAADA ya kimya cha muda mrefu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, anatarajiwa kuibuka na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Roho Imekuchagua Wewe Pekee’, ambao upo katika hatua za mwisho za maandalizi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Ray C ambaye ameanza kujipanga kurejea upya, aliwataka mashabiki wajiandae kuendelea kupata nyimbo zake ambazo kwa asilimia kubwa zinazungumzia mapenzi.

Alisema tayari wimbo huo umefikia kwenye hatua za mwisho, hivyo muda wowote utaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio.

“Mashabiki watanielewa, nyimbo zangu ni mwendelezo wa mambo yanayohusu mapenzi, hivi ni vitu muhimu kwa binadamu,” alisema Ray C.
Msanii huyo alisema kuwa atajitahidi kufanya nyimbo nyingine kwa haraka ili aweze kuachia albamu yake ya kwanza tangu kurudi katika ‘game’.

NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI...SEHEMU YA 04.

ILIPOISHIA

“Subiri wakirudi jioni.”
“Wewe utakuwepo?”

Nililishangaa swali hilo, hakuwa akinidai mimi lakini anataka niwepo?
“Unataka niwepo?”
“Ee.”

“Kwanini?”

“Naamini utanisaidia kuzipata fedha zangu.”


“Uliwahi kuja wakagoma kukupa?”

“Siyo hivyo, ila kila nikija, nikigonga mlango huwa hawafungui.”

“Basi nitakuwepo.”

“Asante kaka. Nije saa ngapi?”

“Saa moja nitakuwa nimerudi.”


Aligeuza mkokoteni na kuondoka zake huku akisema:

“Muda huo nitakuwa nimefika kaka.”

Niliondoka kwenda kazini kuomba ruksa. Lakini wakati naondoka, mfanyakazi mwenzangu mmoja aliniuliza nakwena wapi, nikaamua kumsimulia kwa ufupi kisa changu.


“Khaa! Sasa hapo tatizo liko wapi, mbona dawa ipo rahisi sana.”

“Rahisi! Ni ipi hiyo?”

“Sikia, twende pembeni nikakusimulie,” aliniambia yule mfanyakazi mwenzangu huku akiangalia kulia na kushoto kama mabosi watatokea.


Tulikwenda kusimama pembeni, akaanza kuniambia:

“Sikiliza, kama unaishi nyumba ya namna hiyo, unachotakiwa, kila siku asubuhi na jioni au usiku unapuliza bangi ndani ya nyumba, kama ni majini, mapepo sijui nini, utaona mambo poa kabisa.”


Sikuamini maneno hayo, nikamuuliza mara mbilimbili kama ni kweli.

“Khaa! Nina mjomba angu aliwahi kuishi kwenye nyumba ya hivyo, akaenda sehemu akaelekezwa dawa ni hiyo, akaitumia, mpaka sasa anaishi kwa raha hakuna cha majini wala mapepo,” alisema.


Nilimsikiliza nikianza kuamini kwa mbali, lakini nilifika mahali nikamuuliza hiyo bangi mimi nitavuta au nitaiwasha ili itoe moshi yenyewe?

“Ukishaiwasha, utaiweka mezani au popote ndani kwako, lakini angalia isizimike ili moshi wake usambae chumba kizima au sebule nzima.”


“Hilo linawezekana,” nilimwambia nikimtumbulia macho.

Kwa sababu nilikuwa nimeshaaga, ilibidi niondoke tu na kurudi baadaye. Nilikwenda mtaani, nilitafuta bangi nikapata maeneo ya Kariakoo, nikaitia mfukoni.

CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA..SEHEMU YA 10.

ILIPOISHIA  ...NA IRENE MWAMFUPE NDAUKA.
“Mpenzi, chumba kimepatikana…”
“Wapi..?”
“Kule maeneo ya nanihi, si mbali
sana…”
“Bonge la chumba. Simenti chumba
chote, kikubwa kama uwanja wa mpira, halafu bei ya ubwete…”
“Ngoja kwanza, una maana mimi
nitaweza kuja na gari nikaegesha mahali..?”
“Mh! mh! Mwenye nyumba anaweza
kutengeneza pakingi ana nafasi kubwa…”

***
Baba Joy alikuwa amekaa kwenye
mgahawa mmoja mpya. Hauna watu wengi na uko mtaa wa pili kutoka nyumbani kwake.
Simu yake iliisha chaji na alikuwa akipigania kuchajiwa na mwenye mgahawa huo…
“Chaja ya pini ndigo ilikuwepo mzee,
sijui nani kaichukua? We Benadi…” Benadi ni mhudumu wa mgahawa huo…
“Nani kachukua chaja ya pini
ndogo..?”
“Sifahamu bosi, muulize Malinda jana
alikuwa analalamika simu yake haina chaji,” alijibu Benadi.
Baba Joy alitoka mbio hadi nyumba ya
pili baada ya mgahawa huo. Nyumba ambayo hakuna anayemjua…
“Jamani hodi…”
“Karibu,” binti mmoja, mweupe, mnene
kiasi alitoka na kumwangalia kwa tabasamu mzee huyo…
“Karibu sana…”
“Asante…”
“Shikamoo…”

AUDIO | DOWNLOAD HAPA ...Joto Hasira by Lady jaydee - remix FtSonga, ONE, Nikki Mbishi, Mkoloni.


Bomoa bomoa yatikisa Dodoma.

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Paskasi Muragili, amesema kuwa mpango wa kuwavunjia wananchi nyumba zilizojengwa katika maeneo yasiyopimwa uko pale pale.

Muragili alitangaza msimamo huo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili, akijibu malalamiko ya wakazi wa maeneo ya Kikuyu Kusini, Mkalama, Imagi, Miganga, Chinyika na Kata ya Mkonze, wanaopingana na CDA kwa kutaka kuwavunjia nyumba zao.

Kaimu mkurugenzi huyo alisema kama kweli mji wa Dodoma unatakiwa uwe jiji,   lazima ujengwe kwa ramani iliyopo ambayo imeboreshwa na si kuruhusu ujenzi holela.

Wananchi wa maeneo hayo waliilalamikia CDA kwa nadai kuwa imekuwa mwiba kwa wakazi wa Dodoma.

Ili kuonesha kukerwa na msimamo wa CDA, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kikuyu Kusini walirudisha kadi za chama hicho mbele ya diwani wao  kwa madai kuwa chama hicho hakiwajali wanyonge.

Ruguluni haina shule miaka 14

MWENYEKITI Serikali ya Mtaa Ruguluni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Saidi Mahadula, amesema mtaa huo haujawahi kuwa na shule ya msingi tangu ulipoanzishwa miaka 14 iliyopita.
Mahadula alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukijadili maendeleo na kero za mtaa huo, uliofanyika kwenye viwanja vya Dk. Halid, Makondeko.

Alisema kutokana na kukosekana kwa shule katika mtaa huo, watoto hulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata shule, jambo ambalo wakati mwingine ni hatari kutokana na baadhi yao kuwa na umri mdogo.

Aliyataja maeneo ambayo watoto hao wamekuwa wakifuata shule kuwa ni Mbezi Luis, Kibamba, Mpijimagohe na Mshikamano.
“Umefika wakati wa kuunganisha nguvu zetu na tushirikiane, ili kwa pamoja tuweze kumaliza kero inayotukabili,” alisema Mahadula.

‘Hatuamini ufufuko wa mtoto’.

JESHI la Polisi mkoani Geita limethibitisha kuonekana kwa mtoto Shabani Maulidi, anayedaiwa kufufuka baada ya miaka mitatu ya kifo chake, kilichosababishwa na kutumbukia kisimani mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamnda wa jeshi hilo, Leonard Paulo, alisema kuwa pamoja na kuthibitisha tukio la kuonekana kwa mtoto huyo akiwa hai bado serikali haiamini kama ni kweli alikufa na kufufuka.

“Mimi kama kamanda wa polisi na serikali kwa ujumla, hatuamini kama mtoto huyu alikufa na kufufuka, japo wazazi wake wanakiri hilo. Serikali haiamini vitu kama hivyo,” alisema.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita ambapo mtoto huyo alilazwa kwa matibabu, alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri na wakati wowote ataruhusiwa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli juu ya tukio hilo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali ya wilaya, ambapo kwa sasa hatua inayoendelea ni kutafuta vipimo vya vinasaba (DNA).

Katika tukio jingine, mtoto wa miezi miwili, Edga Sizya, amefariki dunia papohapo baada ya kupigwa kichwani eneo la paji la uso na baba yake mzazi, Sizya Kilulinda (35) mkazi wa Bugurula.

Serikali yazidi kuandamwa...Wadau, MCT, walaani magazeti kufungiwa.

MOTO wa wadau wa tasnia ya habari kuitaka serikali iyafungulie magazeti ya Mwananchi na Mtanzania yaliyofungiwa kwa madai ya uchochezi, umezidi kukolezwa na sasa wanataka Idara ya Habari (Maelezo) ifutwe kwa madai imepitwa na wakati.

Magazeti hayo ya kila siku yalifungiwa Septemba 27 mwaka huu, kwa kutumia sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 inayolalamikiwa, ambapo Mwananchi ilipewa adhabu ya siku 14 huku Mtanzania ikiwekwa kifungo cha siku 90.

Akizungumza za na gazeti hili jana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Dk. Joseph Matumaini, alisema kuwa serikali inapaswa kuomba radhi kwa kitendo hicho na kuyafungulia magazeti hayo haraka.

Alisema kuwa uamuzi uliofanyika ulitumia sababu zisizo na faida kwa umma wa Watanzania.

Matumaini ambaye pia ni padri wa Kanisa Katoliki aliongeza kuwa Idara ya Habari (Maelezo) imepitwa na wakati, hivyo inapaswa ifutwe.

Aliongeza kuwa hata mkurugenzi wa Maelezo naye anapaswa kujiuzulu kwa sababu hakujielekeza katika masuala ya maadili ya uandishi wa habari, sheria za uandishi na sera za habari.

Padri Matumaini alisema Maelezo si chombo cha mtu binafsi ingawa kinatumiwa vibaya na serikali. Serikali imeshindwa kuongoza wananchi inaamua kutishia demokrasia na uhuru wa habari.

“Wanahabari wote tuungane chini ya Baraza la Habari Tanzania kama Mkurugenzi huyo, Assah Mwambene, hatajiuzulu na serikali isipoomba radhi, basi sisi tuunde chombo chetu huru, Maelezo ibaki na magazeti na televisheni ya serikali.

Alihoji kuwa kama kweli magazeti hayo yaliandika habari za kusababisha upotevu wa amani, mbona tangu yasomwe hakujatokea uvunjivu wowowe wa amani.

“Maelezo wajue kuwa kazi mojawapo ya vyombo vya habari ni kusema ukweli kuhusu ajenda fulani, ajenda juu ya jambo fulani nchini si lazima iipendeze serikali,” alisema.

MCT yalaani
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelaani vikali hatua ya serikali kuyafungia magazeti ya kila siku ya Mwananchi na Mtanzania kwa tuhuma za kuchapisha habari za uchochezi na kuhatarisha amani ya nchi.

Taarifa ya MCT iliyosainiwa na Katibu wake Mtendaji Kajubi Mkajanga ilisema kuwa uamuzi uliochukuliwa na serikali ni wa kusikitisha na kinyume na demokrasia na umerudisha nyuma hatua nyingi zilizopigwa na nchi kujenga taifa la kidemokrasia linaloheshimu uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari.

“Uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi ya binadamu na nchi inayojivunia kuwa imejengwa kwenye misingi ya demokrasia na kuheshimu haki za binadamu kama Tanzania haina budi kuhakikisha kuwa haki hiyo inalindwa kwa nguvu zote.

“Vyombo vya habari vinampa mwananchi uwezo wa kuitumia haki hiyo ya kujieleza na kupata habari ambayo imeathirika kwa kufungiwa kwa magazeti hayo,” alisema.

Alisema kuwa japo taifa limepiga hatua kubwa katika kuisimamia haki hiyo ya msingi ya kujieleza na kupata habari, juhudi hizo zinafifishwa kwa kuwepo kwa sheria mbaya zinazofinya haki hiyo kama sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo inampa madaraka waziri anayehusika na maswala ya habari kuyafungia magazeti bila ya haki ya kujitetea au kukata rufaa.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate