EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, October 3, 2013

Mwanamke anaswa na meno ya tembo.

JESHI la Polisi mkoani Singida, linamshikilia mwanamke, Maria Chibago (33), mkazi wa Kijiji cha Mpapa, Tarafa ya Nkonko wilayani Manyoni kwa tuhuma za kupatikana na vipande saba vya meno ya tembo, kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo limetokea juzi, majira ya saa 11:00 jioni katika Kijiji cha Mpapa.

Kwa mujibu wa Kamwela, mtuhumiwa alikuwa ameyahifadhiwa meno hayo kwenye mfuko wa sandarusi na kufukiwa ardhini katika eneo la nyumbani kwake.

Alisema upatikanaji wa nyara hizo, ulifanikiwa kutokana na taarifa za siri kutoka kwa raia wema, kwamba familia ya Maria hujihusisha na shughuli za ujangili, akiwemo mumewe.

Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, mume wa Maria, Tadei Msagala pamoja na washirika wake, baada ya kushitukia mtego wa polisi, walifanikiwa kukimbia.

KWA WANAFUNZI WOTE NA WAKAZI WA ARUSHA KESHO CLUBBING NITE..NDANI YA CLUB SAFARI ARUSHA KISONGO.


MAN CITY YAFUMULIWA NYUMBANI NA BAYERN HADI AIBU, MAN UNITED DROO, REAL YAUA 4-0.

MABINGWA wa Ulaya, Bayern Munich wameonyesha soka ya kiwango cha juu na kuifumua nyumbani Manchester City mabao 3-1 Uwanja wa Etihad.
 
Yalikuwa mabao ya wachezaji bora duniani Mfaransa Franck Ribery dakika ya , Mjerumani Thomas Muller dakika ya na Mholanzi Arjen Robben dakika ya yaliyoizamisha City katika mchezo huo wa Kundi D.
 
Makosa ya kipa Joe Hart na walinzi wake yaliigharimu City leo kabla ya Alvaro Negredo kutokea benchi kwenda kufunga bao la kufutia machozi dakika ya - huku beki wa Bayern Jerome Boateng akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Yaya Toure dakika ya.
 
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Hart, Richards, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, Aguero, Nasri/Silva dk70 na Dzeko/Negredo dk57.
Bayern Munich: Neuer, Rafinha, Boateng, Dante, Alaba, Lahm, Robben/Shaqiri dk78, Schweinsteiger/Kirchhoff dk76, Kroos, Ribery/Gotze dk85 na Muller. 
Celebration: Bayern Munich's Thomas Muller (right) celebrates with team-mates after making it 2-0
Celebration: Bayern Munich's Thomas Muller (right) celebrates with team-mates after making it 2-0
No match: Frank Ribery (right) runs the ball past City's right-back Micah Richards
No match: Frank Ribery (right) runs the ball past City's right-back Micah Richards
Turn on the style: Arjen Robben of Muenchen celebrates his team's third goal
Turn on the style: Arjen Robben of Muenchen celebrates his team's third goal
Not enough: Manchester City's Yaya Toure (right) and Bayern Munich's Toni Kroos in action
Not enough: Manchester City's Yaya Toure (right) and Bayern Munich's Toni Kroos in action
Late scare: Jerome Boateng was sent off for Bayern Munich for a late tackle on Yaya Toure
Late scare: Jerome Boateng was sent off for Bayern Munich for a late tackle on Yaya Toure

TORRES NJE WIKI TATU BAADA YA KUUMIA GOTI JUZI ROMANIA.

MSHAMBULIAJI Fernando Torres anatumai kurejea uwanjani baada ya wiki tatu, kufuatia kuumia goti juzi nchini Romania.
Torres alitolewa nje dakika za mwanzoni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Chelsea ikishinda 4-0 dhidi ya Steaua Bucharest Jumanne, lakini vipimo vimethibitisha hana maumiu makubwa.
 
Arakosa safari ya Norwich Jumapili, ambayo tayari asingecheza kwa sababu ya kutumikia adhabu kutokana na di nyekundu aliyopewa dhidi ya Tottenham.
Anatarajiwa kurudi kuichezea Hispania katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Belarus na Georgia, lakini Chelsea wanatumai kuwa naye tena mshambuliaji wao huyo kabla ya mwishoni mwa mwezi.
Knock: Fernando Torres is treated by Chelsea physios after going down to a knee injury in Steaua Bucharest
Maumivu: Fernando Torres akitibiwa na madaktari wa Chelsea baada ya kuumia goti dhidi ya Steaua Bucharest

Upelelezi waahirisha kesi mauaji ya bilionea Arusha.

WATUHUMIWA saba wa mauaji ya mfanyabiashara wa madini ya tanzanite, Erasto Msuya (43) wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa madini hayo, Joseph Damas “Chusa” na Sharif Mohamed Athuman wote wakazi wa Jiji la Arusha jana wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Moshi.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walifikishwa mahakamni hapo wakiwa katika gari maalumu la kubeba watuhumiwa majira ya saa 5:30 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye silaha, wakiwemo wa kikosi maalumu cha kutuliza ghasia (FFU).

Wakiwa katika chumba cha mahakama kilichowezesha watu wachache kuingia ndani, mwendesha mashitaka wa serikali, wakili Stella Majaliwa baada ya kutaja makosa yanayowakabili washitakiwa aliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na kutokamilika kwa upelelezi.

Wakili Stella aliieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kutokana na kesi ya mauaji ya kukusudia kinyume na kanuni namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai.

Jela miaka 30 kwa unyang’anyi wa silaha Bunda mkoani Mara

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imemhukumu Mroni Mtwena mkazi wa Mihingo wilayani hapa, kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo kuwa Safina Simfukwe na Mwendesha Mashitaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Masudi Mohamedi kuwa mnamo Septemba 9 mwaka juzi, majira ya saa 11 alfajiri huko katika Kijiji cha Mihingo, Wilaya ya Bunda, mshitakiwa aliiba sh 500,000 na simu aina ya Nokia, yenye thamani ya sh 40,000, mali ya Wegero Mesere.

Mwendesha mashitaka huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa wakati anatenda kosa hilo alitumia panga kwa kumkata mlalamikaji kwenye mkono wake wa kulia.
Alidai kuwa mlalamikaji alimtambua na kupiga yowe na wananchi walimkamata na kumfikisha polisi ambapo aliandaliwa mashitaka na kupelekwa mahakamani.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Simfukwe alisema kuwa mahakama hiyo imeridhika pasipo kuacha shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, hivyo kumtia hatiani kutumikia kifungo cha miaka 30 na kuchapwa viboko 24 ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Wednesday, October 2, 2013

UCHAFU WA WEMA, AUNT CHINA NI HUU!


LICHA ya mwaka jana kuita vyombo vya habari na kujisafisha baada ya kukaa nusu utupu jukwaani, mastaa wawili wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel wamefanya uchafu wakiwa Hong Kong, China.
Video ya aibu ya wawili hao ilivuja mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwaonesha ‘wakidendeka’ na kufanyiana vitendo  vinavyokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
 
Video hiyo inaonesha ilirekodiwa siku ya ‘bethidei’ ya Wema, Septemba 27, mwaka huu ambapo bidada huyo alikuwa akitimiza umri wa miaka 25.
Katika video hiyo waliyorekodi wakiwa China, wawili hao wanaonekana kwenye chumba wakiimba wimbo wa ‘Happy Birthday’ na baada ya kumaliza, wakasogezeana midomo na kumwagiana mabusu ya nguvu.

AIRTEL YAKABIDHI VITABU VYA MILIONI 10 SEKONDARI 4 MKOA WA DODOMA‏.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akiwakabidhi msaada wa vitabu vilivyotolewa na kampuni ya simu ya Airtel wanafunzi Mariam Hamisi na Theodory Raymond wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Dodoma wengine katika picha nyuma ni meneja mauzo Airtel - Dodoma Saidimu Ngaleson na Mkuu wa Shule hiyo Maiko Masala.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibakwe ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Augustine Senya (kulia) akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi msaada huo wa vitabu ulitolewa na Airtel kwa Sekondari tano za mkoa wa Dodoma, wengine nyuma wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Hedrick Werner Afisa masoko Airtel Kanda ya Kati na  Saidimu Ngaleson Afisa mauzo Airtel mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi (kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma, Crispin Mtesigwa (kulia) uliotolewa na Airtel kwa kwa shule hiyo jana, wengine nyuma toka kushoto ni  meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma Saidimu Ngaleson na mwalimu Helbet Ngusulwa.
Afisa Elimu Taaluma wilaya ya Chamwino mkoani Dododma Hamisi Mapoto (kulia) akipokea msaada wa vitabu kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Itisso na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi (kushoto) msaada huo umetolewa na kampuni ya simu ya Airtel, nyuma ni meneja mauzo Airtel - Dodoma Saidimu Ngaleson.

MPENZI WA PREZZO AWACHARUKIA BLOGGERS WALIOANDIKA UHUSIANO WAKE NA PREZZO, HIKI NDICHO ALICHOANDIKA KWENE IG YAKE!!!

UTAFITI WAONESHA KIFUA KIKUU(TB) KUSUMBUA VIJIJINI ZAIDI UKILINGANISHA NA MIJINI.

Mtoa mada na Mtafiti wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB)Dr Said Egwaga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha juu ya utafiti walioufanya mwaka 2011 katika wilaya 62  nchini ulibaini  kati ya watu Laki moja kuna wagonjwa wa Kifua Kikuu 295 na waliothirika zaidi ni wanaume ukilinganisha na wananwake na idadi  kubwa iko maeneo ya  Vijijini  ukilinganisha na  mijini tofauti na  walivyotarajia.
Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele nchini.Dr  Upendo Mwingira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano wa Kimataifa  cha taasisi za afya za jamii unaofanyika mkoani Arusha.

SOMA UJUMBE WA PENNY KWA MPENZI WAKE DIAMOND KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO

Juu ni ujumbe aliouandika mpenzi wa staa wa Bongofleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mungilwa ‘Penny’ kwa Diamond katika siku yake ya kuzaliwa. Penny ameandika ujumbe huo pamoja na picha hapo juu katika akaunti yake ya Instagram muda mfupi uliopita. 

TASWIRA ZA VURUGU MKOANI MBEYA


Matairi yakichomwa barabarani wakati wa maandamano ya wafanyabiashara waliokuwa wakipinga kununua mashine za (EFDs) kutoka TRA. Mashine hizo zinadaiwa kuuzwa shilingi laki nane (800,000/-).
Polisi wakituliza vurugu zilizotokea wakati wa maandamano ya kupinga mashine za EFDs.

Wanafunzi waandamana Dar.

ZAIDI ya wanafunzi 50 waliochaguliwa kujiunga  katika vyuo vikuu mbalimbali nchini kwa mwaka huu, jana waliandamana kwenda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa lengo la kukutana na Waziri Shukuru Kawambwa, baada ya kukosa mikopo.

Wakizungumza na Tanzania Daima Jumatano, wanafunzi hao walisema zaidi ya wanafunzi 200  wenye sifa za kupewa mikopo ya elimu na Bodi ya Mikopo (HELBS), wamenyimwa bila maelezo.

Walisema kuwa tangu mwisho wa wiki wamekuwa wakihangaika kujua sababu za kutopewa mikopo kutoka katika bodi hiyo bila mafanikio.

Mwanafunzi Ayoub Suleiman aliyechaguliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema kuwa wameamua kumfuata Waziri Kawambwa ili wajue ni kwa nini hawajapewa mikopo hiyo.

Alisema majibu ya wanafunzi walioomba mikopo hiyo yalitoka Septemba 27 mwaka huu, miongoni mwao hawakuwepo kwa maelezo kuwa bajeti imekwisha.

“Waliotupa majibu haya ni wafanyakazi wa mapokezi na walinzi pale bodi ya mikopo, sio wahusika wenyewe kwa kuwa kila tulipoomba kukutana na mkurugenzi, hatukupata nafasi hiyo,” alisema Suleiman.

Nyumba ya mchungaji yateketea Dar.

NYUMBA ya Mchungaji Paul Ndalama (70) wa kanisa la Anglikana imeungua moto maeneo ya Moshi wilaya ya Ilala.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala Marietha Minagi alisema tukio hilo limetokea juzi saa 12:45 katika mtaa wa Moshi katika kanisa la Anglikana.

Minagi alisema moto ulizuka ghafla kwenye nyumba yenye vyumba vitatu vya kulala, jiko, choo na bafu na kuteketeza nyumba yote pamoja na mali yote iliyokuwemo ndani.
Minagi alisema nyumba hiyo inamilikiwa na kanisa la Anglikana. Mwenye nyumba hakuwepo wakati wa tukio. Chanzo cha moto hakijafahamika.

Katika tukio jingine, mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-35 amefariki baada ya kugongwa na gari maeneo ya Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate