EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, November 4, 2013

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AIBUKA NA 'A LADY WITH CONFIDENCE', APEWA MILIONI MOJA NA DAR LIVE

Pichani juu ni malkia wa mipasho Khadija Kopa akiwa stejini katika usiku wake maalumu, huku akisindikizwa na kundi zima la TOT.
Kiongozi wa TOT, Gasper Tumaini, akiushukuru uongozi wa Dar Live kwa kuandaa usiku wa Malkia muda mfupi kabla hajapanda stejini.

NATURE APEWA TAFU JUKWAANI NA CHEKA USIKU WA MALKIA

Msanii kinara wa kundi la TMK halisi, Sir Juma Nature usiku wa kuamkia leo alipewa tafu stejini na bondia maarufu nchini Francis Cheka ambaye alipanda jukwaani kuungana nae kusalimia mashabiki wake ambao walimshangilia kwa sana. Aidha TMK walimpatia bondia huyo fulana maalumu ya kundi hilo. Picha zifuatazo zinajielezea zaidi:


Bondia Francis Cheka (kati) akiwa stejini wakati TMK Halisi wakifanya vitu vyao.

Cheka akifurahia burudani ya shoo ya TMK

MWANAHAWA JUU YA STAGE, SNURA YUKO TAYARI BACK SATGE!


Mwanahawa Ally akiwa msanii anayejitegemea, akiimba nyimbo zake maarufu katika usiku wa Malkia ndani ya Dar Live.

Msanii Snura (kati) akiwa na shabiki zake nyuma ya VIP Backstage tayari kwa kumsindikiza Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa ndani ya Dar Live.

Sunday, November 3, 2013

WANAFUNZI KIDATO CHA NNE, QT WAOMBEWA JIJINI DAR

Wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na QT wanaotegemewa kuingia kwenye mtihani kesho wakiwa kwenye misa maalumu ya maombezi iliyofanyika katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar leo.
Wanafunzi wa QT pamoja na wa mashule mbalimbali wakiomba sala maalumu ya kuwatakia kila la heri katika mitihani yao kesho.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)

Kajala awashukia wanaomsema kuhusu malezi ya mwanae, hichi ndicho alichosema

“…nawashangaa sana watu wengine mnajifanya mnajua sana kuongea kuhusu mambo yasiyo wahusu kuna mzazi yoyote anataka mwanae apotee ache mambo ya kishamba unataka mtoto avae dira kwani yeye mtu mzima kama unaona namlea mtoto wangu vibaya niachie mwenyewe zaa wa kwako mlee vizuri…”

Hayo ni maneno ya mwanadada Kajala aliyoyasema leo baada ya fans wake mbalimbali kuanza “kumponda” kuwa anamlea mtoto wake “ndivyo sivyo” hususani suala kumvalisha mtoto wake vinguo vya “wadada wa mjini”

Kajala ambaye mara nyingi anaonekana akiweka picha mbalimbali za mwanaye huyo aitwaye Paula akiwa kwenye mapozi tofauti alizidi kusisitiza kuwa mtoto huyo ni wake na ambaye hapendi anachofanya basi atafute wake.
Kauli yake hiyo ilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wake ambao baadhi yao walisema yafuatayo kumsapoti….

“…tena wakukome ma sis wanajua uchungu wako ulioubeba au au wanajua umemkuzaje mpaka kufika ... nyamafu hao wakosa akili wana low life yamaisha they av got nothing better to do Wa africa uwa tunamatatizo dunia nzima mtoto wa mwenzio anakuhusu nini ukse umuongelee kweli Education kitu kuzuri ukisoma unafikilia utaongelea kiumbe we kazi. Acheni ujinga na utumwa business za wenzenu zinakuwa zenu.. thats ma bby paullet right there and am proud she is a grown gal hun.. kay ma mdogo never give a Fuck life is unbilivable!!!! Family first...”

Matokeo darasa la saba; Ufaulu waongezeka

Dar es Salaam. 
Zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba Septemba mwaka huu, wamefaulu.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde akionyesha moja ya karatasi za majibu ya mtihani wa darasa la saba kwa waandishi wahabari Dar es Salaam jana, wakati wa kutangaza matokeo ya mtihani huo wa mwaka huu. Picha na Emmanuel Herman.

Matokeo hayo yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde aliyesema ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ikilinganishwa na mwaka jana.

Alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani huo na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250.
Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01.

Shehena pembe za ndovu zakamatwa Dar es Salaam

Dar es Salaam. 
Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.


Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .

Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.

Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.

DK MVUNGI AVAMIWA NA KUCHARANGWA MAPANGA


 
Dk. Sengondo Mvungi.
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Mvungi, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana na kukatwa mapanga maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai ya kutaka wapatie fedha. Watu hao walitimiza lengo lao hilo baada ya Dk. Mvungi kuwaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

MAKABIDHIANO YA OFISI YA TFF YALIYOFANYIKA KATIKA OFISI ZA TFF JIJINI DAR JANA


Rais wa TFF aliyemaliza muda wake, Leodegar Tenga (kulia) akimkabidhi baadhi ya nyaraka Rais Mpya, Jamal Malinzi.

  Rais wa TFF aliyemaliza muda wake, Leodegar Tenga akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano. Kushoto ni Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi.   
    Rais Mpya wa TFF, Jamal Malinzi akiongea wakati wa hafla hiyo.

ANGETILE OSIAH APIGWA CHINI UKATIBU MKUU TFF - WAMBURA AKAIMU NAFASI YAKE

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.


Jamal Malinzi
Rais

Napumzika kuigiza - Rose Ndauka

Mwigizaji Rose Ndauka amesema kuwa anapumzika kwenye tasnia ya filamu kwa mwaka mmoja kwakuwa filamu za Tanzania zinafanana sana na anataka aje na kitu kipya na tofauti.

Kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti Rose Ndauka amesema wazo hilo limetokana na tatizo la kufanya kazi zinazojirudia mara kwa mara, hali iliyomfanya aamue kujipa likizo ya muda ili kujipanga.Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuwa na utata muigizaji huyo ni mjamzito kwa sasa na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu kubwa ya yeye kusimama kwa muda.

Mke wa William Mtitu ajifungua mtoto kike.

Mwigizaji, muongozaji wa filamu na mmiliki wa kampuni wa filamu ya 5effects William Mtitu amepata bahati ya kuongeza idadi ya wanafamilia wake baada ya mke wake Jovitha Mtitu kujifungua salama mtoto wao wa kwanza kwenye hospitali ya Regency jijini Dar es salaam hivi majuzi.

Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja wa kijamii Mtitu aliandika…
“Nawashukuru madaktari wa hospital ya regency na kwa Dr mvungi wakiongozwa na Dr getu kwa kusaidia mpaka mke wangu kujifungua salama na sasa naitwa baba na mke wangu mama ,kwa kweli mungu awabaliki sana…”
Hali ya Mama na mtoto ni njema na  wanaendelea vizuri. Hongera sana Mtitu na familia yako.

Saturday, November 2, 2013

Hemed: Niacheni nitafute maisha

MWIGIZAJI  na mwanamuziki mwenye mbwembwe nchini Hemed PHD ametoa onyo kwa wanawake ‘wanaomsarandia’ wakitaka penzi lake wamwache atafute maisha kwani huu ndio wakati wake.

Hemed PHD.
Amesema kitendo cha  baadhi ya wanawake kuacha shughuli zao na kuanza kumfuatilia wakitaka awe mpenzi wao kimekuwa kikimkera sana hasa ikizingatiwa kuwa hakiendi sawa na utamaduni kwani mwanamume ndiye anayetakiwa kumfuata mwanamke.


“Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwangu kukaa na namba moja ya simu kwani nikishaona nasumbuliwa sana huwa nalazimika kubadilisha ili kuepusha usumbufu,” anasema.


Anaongeza kuwa huwa anawatosa wanawake wanaomfuatilia kwa kuwa anaamini hawamtakii mema : “Ninahisi wengine wanataka kuniharibia tu, huwezi jua labda ni mbinu tu za kutaka kunipoteza kwenye ramani.”


Hemed anasema kipaumbele chake sasa ni kazi na ndiyo maana muda mwingi amekuwa haonekani au kusikika.

ALAMA MPYA ZA UFAULU ZAPINGWA

SIKU moja baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya marekebisho katika upangaji wa viwango vya alama za matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne na sita kwa kufutwa daraja sifuri na kuwekwa daraja la tano, wadau na wasomi wameponda mfumo huo.

Wakizungumza na gazeti hili, wadau hao walisema kuwa tatizo si kushuka kwa kiwango cha ufaulu, bali uwepo wa elimu bora nchini.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema kuna mifumo miwili ya elimu nchini inayotumika, ambayo ni ule wa watu masikini na wenye nafuu ya maisha.

Alisema hali hiyo inaanzia chekechea hadi vyuo vikuu, huku akihoji wizara husika mfumo wa aina hiyo unamlenga nani, kwamba tatizo lililopo ni ubora wa elimu hasa katika shule za umma.

Bashiru alisema kwenye mifumo hiyo inayotumika, ule wa masikini upo kwenye shule nyingi za umma ambako ndiko kwenye watoto wengi wanaofeli kutokana na kukosa vifaa vya kufundishia, maabara na walimu.

“Katika shule za umma watoto wengi hawasomi, hawana maabara, sasa wizara inawatahini nini? Mageuzi yoyote ambayo yatashindwa kuondoa matabaka hayawezi kuleta elimu tunayoitaka,” alisema.

Alisema ubora wa elimu utawahusu wanafunzi hao wanaosoma shule za michepuo ya Kiingereza, kwani ndio watakaokuwa wanafaulu kwa kuwa shule zao zina mfumo mzuri unaoeleweka na viwango walivyojiwekea kama mwanafunzi hatafikia atarudia darasa ama kuachishwa shule.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate