EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 4, 2014

KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO


NISHA BWANA MPYA, GARI MPYA


Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kutokana na kuvuta ndinga mpya na huku akidaiwa kutoka na mwanaume mpya.
Msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Kikizungumza na Ijumaa, chanzo ambacho ni jarani wa msanii huyo kilisema licha ya Nisha kuendesha mkoko huo aina ya Toyota Harrier, sasa anatoka na mwanaume mwingine ambaye mara kadhaa wamekuwa wakimbonji pamoja.
“Sasa ana mwanaume mwingine, huenda ndiye aliyemnunulia lile gari analoendesha,” alidai jirahi huyo wa Nisha.
Nisha alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema, ni kweli ana gari lingine ila kuhusu mwanaume anayetembea naye kwa sasa ni siri yake ila atamuanika siku si nyingi kwa kuwa wana mipango mikubwa baadaye.

Thursday, April 3, 2014

HABARI NJEMA KWAKO!!

Toyota Hiluz surf,mwaka 2003..ndo imeshuka bandarini hata haijaendeshwa bado iko sokoni bei ni Tshs 20000000/= (Mil 20)...call/text or whatsapp +447758158421

SHAMSA ATESWA NA GENEVIEVE

MUIGIZAJI wa Bongo Movies, Shamsa Ford amefunguka anaumia sana na mafanikio ya waigizaji wa Nigeria kama Genevieve kwani ndoto yake ni kufanya zaidi ya wao.
Mwigizaji wa Bongo Movies, Shamsa Ford.
Shamsha alifunguka hayo wiki iliyopita na kudai kila siku wasanii wa nyumbani wamekuwa wakishindwa kufika levo za mastaa hao kwa kutokuwa na mipango endelevu.

SANDRA AONYA MASTAA WASAGAJI

MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’ amesema  kinachowaponza mastaa wengi kutopenda kuingia kwenye ndoa ni kupenda vitendo vya usagaji na ushoga.
Msanii wa filamu za Kibongo, Salma Salmini ‘Sandra’
Akipiga stori na paparazi wetu, Sandra  alisema vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri siku hadi siku kwa mastaa hususan wa filamu kwa tabia ya kupenda kuiga nchi za jirani.
“Ushoga na usagaji ni janga kwa mastaa, matokeo yake wengine hata wakibahatika kuingia katika ndoa wanashindwa kupata watoto kirahisi, hali inatisha, tubadilike,” alisema Sandra.

BABU AYUBU YAMKUTA MAZITO



STAA wa vichekesho anayeigiza sauti za watu mashuhuri nchini, Babu Ayoub ‘Mc Babu Ayoub’ amekutwa na mazito baada ya ukuta wa nyumba yake kuzolewa na mafuriko na kusababisha hasara.
Gari aina ya Toyota Carina la msanii  Babu Ayoub ‘Mc Babu Ayoub’ likiwa limeharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta
Akizungumza na Amani, Babu Ayoub alisema kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, ambapo ukuta huo uliharibu sehemu kubwa ya gari lake aina ya Toyota Carina alilokuwa ameliegesha nje.
“Mvua ilikuwa kubwa, nikiwa nimelala nilitoka nje baada ya kusikia kishindo.

WEMA AZUA TIMBWILI GLOBAL, AJIITA YEYE NI CHIZI KULIKO MACHIZI WOOTE!


Stori: Sifael Paul
HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”

WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

Wednesday, April 2, 2014

RAIS SHEIN AZUNGUMZA NA WAZIRI MATHIAS CHIKAWE IKULU ZANZIBAR LEO


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar leo. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.

UTAJIRI WA MASANJA KUFURU!

Stori: Shakoor Jongo
UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo,  Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.
HABARI MEZANI
Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.
“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

YONDANI, KASEJA WATAJWA FEDHA ZA AZAM

Kipa wa Yanga, Juma Kaseja.
Na Sweetbert Lukonge
HALI si shwari Yanga, wachezaji wa timu hiyo, kipa Juma Kaseja na beki wake, Kelvin Yondani wamekalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo na huenda wakatimuliwa baada ya kutuhumiwa kuihujumu katika mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wikiendi iliyopita.
Wachezaji hao wanadaiwa kupokea mamilioni ya fedha kutoka Azam ili wacheze chini ya kiwango.
 
Beki wa Yanga, Kelvin Yondani.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani, Yanga ilitandikwa mabao 2-1 ambayo yanadaiwa yalitokana na uzembe uliofanywa na wachezaji hao na kuiweka timu hiyo kwenye mazingira magumu ya kutetea ubingwa wake.

Tambwe: Nawasubiri Simba niende Azam FC


Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe.
Na Sweetbert Lukonge
SIKU chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Amiss Tambwe, kutangaza kuikacha timu hiyo kutokana na ndoto zake za kutaka kushiriki michuano ya kimataifa kufeli, sasa yupo mbioni kujiunga na  Azam.
Tambwe ambaye anaongoza kwa kuzifumania nyavu katika michuano ya ligi kuu msimu huu akiwa na mabao 19, amesema yupo tayari kutua klabuni hapo mara tu mipango yake itakapokamilika.
Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe (kushoto) wakishangilia moja ya  bao katika Ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa taratibu za kujiunga na Azam zimepamba moto na tayari ameshafanya nao mazungumzo kupitia kwa wakala wake.

Tuesday, April 1, 2014

NAAPA: WANANCHI HAWAJAWAHI KUTAKA KATIBA MPYA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
WABUNGE wa Bunge Maalum la Katiba wanaokutana mjini Dodoma kujadili namna ya kupata Katiba Mpya wamekuwa wakijinasibu kuwa, wanawawakilisha wananchi wa Tanzania katika kupata katiba iliyo bora.
Unaweza kuwepo uongo, lakini huu wa kuwasingizia Watanzania kuhusu kupatikana kwa Katiba Mpya ni uongo mkubwa ambao sijui wanaouanzisha wana malengo gani na taifa hili? Nikiulizwa kwa nini? Nitasema kwa kiapo kuwa, hakuna Mtanzania halisi aliyewahi kuwa na haja ya kupatikana kwa Katiba Mpya!
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
Mwenye kunihoji kuhusu Watanzania halisi ninaowazungumzia, nitamwelewesha kuwa ni wale waishio vijijini na waliopo mjini ambao wamekosa fursa ya kupata elimu bora ya kuwawezesha kujitambua.

TANZANIA NI ZAIDI YA SERIKALI 2/3

Mwenyekiti wa bunge la Katiba, Samweli sita.
NIANZE kwa kulitaja kwa fahari kubwa jina la Mwenyezi Mungu, Baba muweza wa kila jambo, kwa kutuwezesha kuwa wazima wa afya, ambao leo kwa mara nyingine, tunakutana katika ukurasa wetu huu wa kubadilishana mawazo mawili matatu.
Baada ya malumbano ya zaidi ya mwezi mzima ya jinsi gani upigaji kura utakuwa wakati wa kupitisha rasimu ya katiba katika Bunge Maalum, hatimaye ufumbuzi umepatikana kwamba sasa wajumbe watakuwa huru kuamua aina ya upigaji wake wa kura, iwe kwa siri au wazi.

LULU KATIKA SKENDO YA KUPORA BWANA WA MTU

E LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Staa Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika pozi.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate