EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, May 3, 2015

MAPOKEZI YA JK AKIPOWASILI KUHUDHURIA SHEREHE ZA MEI MOSI 2015 JIJINI MWANZA

 Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Sumve Mhe Richard Ndassa  alipowasili katika uwanja wa ndege wa
Mwanza tayari kwa sherehe za Mei Mosi Ijumaa
 Rais Kikwete akisalimiana na  Jaji Robert Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa sherehe za Mei Mosi Ijumaa
  RAis Kikwete akisalimiana na Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Joaquina De Mello
 Rais akilakiwa na Jaji wa Mahakama Kuu

 Rais Kikwete akisalimiana na mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza  Askofu Chalres Sekelwa 
 Rais Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza
 Rais Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza
 RAis Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Cocacola Mwanza, Bw. Christopher Gachuma
 Rais Kikwete akisalimiana na Dr. Faisal H.H. Issa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza
 Rais Kikwete akilakiwa na kikundi cha kwaya
 Ngoma za utamaduni
 Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni
 Rais Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza
 Rais Kikwete akipokea risala ya Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza
 Rais Kikwete akiongea na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza
 Rais Kikwete akiongea na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza
Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa  Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza

MTOTO WA FAMILIA YA KIFALME UINGEREZA ATOLEWA HOSPITALI

Mtoto wa kike wa Prince William na Kate Middleton aliyezaliwa jana.
Prince William na Kate Middleton wakiwa wamembeba binti yao.
Prince William na Kate Middleton wakitoka Hospitali ya St Mary jijini London.
Prince William na Kate Middleton wakiwaaga watu waliofika hospitali wakati wakielekea Ikulu ya Kensington.
 Prince William akiwa amembeba mtoto wao wa kwanza, Prince George eneo hilo la hospitali.
Bado haijafahamika ni jina gani atapewa mtoto huyu.
MTOTO wa kike katika familia ya kifalme ya Uingereza ya Prince William na Kate Middleton aliyezaliwa jana ametolewa hospitali na kupelekwa nyumbani kwenye Ikulu ya Kensington.
Mtoto huyo wa kike ambaye ni wa pili katika familia hiyo alizaliwa jana Jumamosi katika Hospitali ya St Mary jijini London.
Familia hiyo mpaka sasa bado haijaamua mtoto huyo apewe jina gani.
Mtoto huyo ataendelea kubaki katika Ikulu ya Kensington ambapo leo anatarajiwa kutembelewa na Malkia wa Uingereza, Prince Charles na familia ya Kate.

Saturday, May 2, 2015

SHOO YA ZARI ALL WHITE PARTY YAFUNIKA JIJINI DAR

Diamond akiwachengua mashabiki kwa wimbo wake wa Nasema Nawe aliomshirikisha Malkia wa Taarab, Khadija Kopa.
Malkia wa Taarab nchini, Khadija Kopa akiimba sambamba na Diamond Wimbo wa Nasema Nawe.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shetta akiwarusha mashabiki waliofika katika Usiku wa Zari All White Party.
Diamond na Nay wa Mitego wakiimba ngoma yao ya Muziki Gani.
Mashabiki wakijiachia.
Diamond Platnumz akizikonga nyoyo za mashabiki.
Ray Kigosi na Mama Rolaa nao ndani.
Diamond akicheza na mashabiki wake.
Nyomi iliyohudhuria shoo hiyo.
Diamond Platnumz akimbusu mpenzi wake Zari katika usiku wa Zari All White Party ndani ya Mlimani City.
Zari na Diamond katika pozi ndani ya Mlimani City.
Zari na Diamond wakati wakiingia ukumbini.
Wasanii wa Yamoto Band wakiwa wametulia tayari kwa shoo ya usiku wa kuamkia leo.
Mpiga Picha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos (kati) akipozi na watangazaji Sauda Mwilima wa Star TV(kulia) na Khadija Shaibu 'Dida' wa Times FM.
Wanausalama wakiwaondoa baadhi ya watu waliokosa tiketi.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo mashabiki wa Diamond.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS, MUSA MATEJA / GPL)

HUSNA MAULID AFUKUZWA MSIBANI


Aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid.
Imelda mtema
ALIYEKUWA mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid hivi karibuni amedaiwa kufukuzwa kwenye msiba mmoja maeneo ya Mbezi mara baada ya kuonekana akijipiga picha (selfie) na kujichukua video akiwa ghorofani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Husna akiwa msibani hapo, kwa sababu anazozijua mwenyewe, alipanda ghorofani kwenye nyumba hiyo yenye msiba na kuanza kujipiga picha hizo kitendo ambacho kilionekana kuwakera wafiwa.
“Alipanda ghorofani akaanza kufanya mambo hayo ya kujipiga picha utadhani tupo kwenye sherehe,” kilisema chanzo hicho na kuendelea:Mara baada ya tukio hilo la ajabu, wafiwa wakaamua kumfuata Husna kulekule ghorofani na kumwambia ashuke na aondoke zake, akaondoka. Husna alipopigiwa simu, alijibu: “Siyo kweli, wananichafua tu.”

KIGOGO MPYA WA WOLPER ANASWA

Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe akiwa na Jimmy Mgaya anayedaiwa kuwa ni bwanake.
Mwandishi wetu
Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Jacqueline Wolper na Jimmy Mgaya wakipozi kimahaba.
Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.

“Kama mtakumbuka kuna siku gazeti lenu (Risasi Jumamosi) mliandika kuwa Wema (Sepetu) na Wolper walilewa chakari kwenye pati ya ‘bethidei’ ya Petit Man, basi huyo kigogo ndiye aliyewafanyia kufuru na ile pati ilifanyika nyumbani kwake, Kinondoni-Manyanya (Dar),” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia ambazo gazeti hili linazishikilia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, gazeti hili lilimtwangia simu Wolper na kumsomea mashitaka yake juu ya mwanaume huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy.

WEMA, ZARI WATOANA JASHO

Musa mateja na Imelda Mtema
Nisheedah! Gumzo la mjini wiki hii ilikuwa ni shoo ya mchumba wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Zarinah Hassan ‘Zari’ iitwayo Zari All White Party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar na ile ya Instagram Party ambayo ilimhusu mrembo Wema Sepetu iliyofanyika jijini Mwanza ambapo nyuma ya pazia, warembo hao walitoana jasho kuhakikisha wanafunikana, Risasi Jumamosi lina stori kamili.
Staa wa Bongo movie,Wema Sepetu.
MVUTANO WAANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mvutano wa Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Diamond na Zari ambaye anammiliki Diamond kwa sasa, uliibuka Alhamisi iliyopita wakati kila mmoja akijiandaa kwenda kwenye shoo inayomhusu.
“Wema na Zari leo ni full kutoana jasho, kila mmoja anataka kuwavuta mashabiki wengi upande wake.
ZARI APEWA SAPOTI
“Zari amepata sapoti kubwa kutoka kwa mpenzi wake wa sasa Diamond kwani walikuwa wanafanya shoo pamoja hivyo alikuwa na kibarua cha kuwakusanya mashabiki wote wa Diamond waende kwenye shoo yake ili Wema asipate watu,” kilisema chanzo hicho.
UPANDE WA WEMA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kwa upande wa Wema, yeye alikuwa na kibarua kizito cha kuwakusanya marafiki zake hususan mastaa wa Bongo Movies wasiende kwa Zari na badala yake waende Mwanza kwenye Instagram Party.
Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Ni mnyukano wa aina yake, Wema alikuwa na kibarua kizito kuwashawishi Bongo Movies waikache shoo ya Zari waende Mwanza kwenye Instagram, bahati nzuri alifanikiwa kwani wasanii wengi walimuunga mkono,” kilisema chanzo hicho.

Friday, May 1, 2015

USTAA UMEWASHINDA,WAPO KAMA HAWAPO!!!


Na Hamida Hassan
Wapo mabinti ambao waliingia kwenye fani ya uigizaji kwa mbwembwe, wakawika sana kwenye vyombo vya habari na kuunyemelea ustaa lakini ghafla wakayeyuka.Walipoibukia kwenye fani walionekana watakuwa tishio na kuwafunika wale wakongwe waliokuwa wakionekana wao ndiyo wao. Sasa hivi hawajulikani wako wapi na wanafanya nini.
Skaina Ally
Skaina Ally
Huyu alikuwa tishio sana miaka ya nyuma. Umbo lake tata, uzuri wake vilimbeba, akawavutia baadhi ya wanamuziki ambao walimfanya kuwa Video Queen kwenye nyimbo zao kama vile Bob Junior aliyemtumia kwenye ‘kichupa’ chake cha Wimbo wa Kimbiji.

NAY AFUNGUKIA NDOA NA SHAMSA

Msanii wa muziki, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ameeleza kuwa endapo msanii mwenzake ambaye sasa hivi wanapika na kupakua, Shamsa Ford atamuonesha utulivu na uaminifu hataona sababu ya kutomuoa.
Msanii wa muziki, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,akipozi kimahaba na Shamsa Ford.
Nay aliyasema hayo juzikati alipokuwa akizungumzia mipango yake na Shamsa ambaye amejiweka kwake baada ya kutosana na mzazi mwenzake, Siwema. Nay alisema: “Hilo la ndoa kiukweli kabisa kama Shamsa ataonesha kutulia na kunithibitishia kuwa hatakuja kunizungua, sitaona hatari kumuoa.”

MKE WA MAFUFU ABEBA VIRAGO!

KIMENUKA! MKEwa staa wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki amenaswa akifungasha virago nyumbani kwake Mwananyamala-Hospitali na kuelekea kwa wazazi wake maeneo ya Mbagala jijini Dar akidai kuchoshwa na tabia za mumewe huyo, Ijumaa lina ‘full’ stori.
Mkewa staa wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki akiwa na mizigo yake.
Akizungumza na mapaparazi wetu, Salma alisema kwa kipindi kirefu msanii huyo amekuwa akimuonyesha tabia za ajabu ikiwemo hivi karibuni kunaswa akiwa amezungukwa na vimwana kana kwamba si mume wa mtu.“Mara nyingi akiwa anatoka kwenye shughuli za usiku huwa tunatoka wote lakini cha ajabu kuna siku alinigomea kabisa kwenda naye kwenye lile onesho la Twanga Pepeta, akarudi saa 11 alfajiri na kwenye bethidei ya mtoto wa Davina akaniambia mimi nibaki nyumbani kumbe alikuwa ana mambo yake huko kwani alirudi asubuhi saa 12.
Siku ya harusi yao.
“Nimevumilia mengi sana kwenye hii ndoa mpaka leo kuamua kuondoka. Acha nimuache na mambo yake,” alisema Salma kwa masikitiko.Alisema japo katika uhusiano wao wana miaka isiyopungua saba, walikuwa kwenye uchumba kwa miaka minne na baadaye wakafunga ndoa mwaka 2013 lakini anashindwa kukumbuka alipotoka.

BALAA LA WAJAWAZITO KUPENDA CHIPSI KUKU

Ugonjwa unaowakabili watoto waliotoka mgongo nje pamoja na vichwa vikubwa, unaelezwa kusababishwa na ukosefu wa Folic Acid mwilini, hali inayochangiwa na mama mjamzito kupenda kula chipsi kuku.Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya watoto ya Moi, Agricore Joseph alisema wanawake wengi hufikia hatua ya kujifungua watoto wenye matatizo hayo kutokana na kupenda vyakula hivyo, kitu ambacho kinaweza kuepukika.
Mtoto aliyezaliwa akiwa na kichwa kikubwa.
Dokta Agricore aliyasema hayo alipokutana na MC maarufu jijini Dar, Joyce Amina Mwakipunda ‘Mc Jojo’ na Mtangazaji wa Kipindi cha Tashtiti Zetu cha Redio Uhuru, Nuru Issa, walipofika hospitalini hapo kutoa misaada mbalimbali kama vile pampasi, mafuta, poda, maji ya kunywa, juisi ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yao ya kuzaliwa.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate