EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, May 28, 2013

DIAMOND FT NAY WA MITEGO - MUZIKI GANI { OFFICIAL VIDEO }

HATIMAE MSHINDI WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA AKABIDHIWA KITITA CHAKE.

Siku chache baada ya Mwanafunzi wa chuo cha ualimu Kasulu mkoani Kigoma, Valerian Nickodemus (22)  kuibuka kidedea na kujishindia kitita cha Shilingi milioni 100 katika promosheni ya MAHELA iliyoendeshwa kwa mafanikio makubwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, sasa ni zamu ya Watanzania wengine kujumuika na kucheka nae baada ya kuzinduliwa tena kwa Promosheni nyingine ya Cheka Nao.
 
Promosheni hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa kampuni hiyo kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha.  Baada ya zaidi ya Watanzania 300 kunufaika kwa kujishindia fedha taslimu katika Promosheni ya MAHELA iliyomahitimishwa Aprili 24 mwaka huu, sasa zaidi ya wateja 6000 wa Vodacom watajishindia Zawadi mbali mbali kwa kipindi cha siku 60.

Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni. Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na  Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa
Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
Valerian Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela. 

Tanzania yasema vitisho M23 haviinyimi usingizi.

Dar es Salaam.
Tanzania imesema vitisho vinavyoendelea kutolewa na waasi wa M23 wanaopigana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), haviinyimi usingizi.
Hata hivyo, imetaka Jumuiya ya Kimataifa kutopuuza vitisho hivyo.
Kauli ya Tanzania inakuja huku kukiripotiwa kuwapo kwa mapigano makali baina ya vikosi vya Serikali waliopambana na waasi hao, ambao wameanzisha tena harakati ya kuliteka Jimbo la Goma na maeneo mengine ya jirani.

Mapigano hayo ni ya kwanza tangu M23, kuondoka mjini humo mwaka jana kufuatia shinikizo za kidiplomasia.

Umoja wa Mataifa (UN), umesema utaongeza kasi ya juhudi zake za kutafuta amani kwa kutuma kikosi cha wanajeshi 3,000 kujaribu kuzima mapigano hayo, ambayo yalisababisha watu 19 kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema vikosi vya Tanzania vilivyoko Congo vitaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia weledi na miongozo ya UN.

Kanali Mgawe alisema kauli zozote za vitisho vinazoendelea kutolewa na waasi hao, haziwezi kurudisha nyuma juhudi hizo.

Lwakatare amwekea DPP pingamizi

Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, amewasilisa pingamizi la awali dhidi ya maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), katika Mahakama ya Rufani.

DPP amewasilisha katika Mahakama ya Rufani maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi, akiiomba mahakama hiyo iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi huo.


Hata hivyo Lwakatare kupitia kwa jopo la mawakili wake, jana aliwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi hayo akiainisha hoja mbili, ambazo mawakili wake watazitoa wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo.
‘‘Maombi hayo ya marejeo yana dosari ambazo haziwezi kurekebishwa kwa kutokana na kushindwa kuambatanisha nakala ya mwenendo ambao ndio maombi hayo yamejengwa.’’ anadai Lwakatare.

Katika hoja ya pili anadai kuwa kiapo kinachounga mkono maombi hayo ya marejeo, kina dosari ambazo haziwezi kurekebishika kwa kuwa kimehusisha na mambo mengine yasiyohusika.

Lwakatare na Rwezaura walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kula njama na kupanga kumteka Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu.

Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu aliwafutia mashtaka hayo matatu ya ugaidi na kuwabakizia shtaka moja linaloangukia kwenye jinai ya kula njama za kutenda kosa la kumdhuru Msacky kwa kutumia sumu.

Monday, May 27, 2013

WANAUME ZAIDI YA 500 WAGOMBEA KUMUOA WASTARA.

TAKRIBAN  wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.
Wastara Juma.
Habari na Global Publishers.
Akizungumza na ‘The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.
 
“Jamani mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema Wastara.
Wastara alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure kwa sababu kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado anasikia harufu ya mumewe Sajuki.
 
“Bado harufu ya Sajuki ipo mwilini mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto wa mwenzao wanakosea sana, sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,” alisema Wastara mwenye mtoto mdogo aliyezaa na Sajuki.

KESI YA LWAKATARE YAAHIRISHWA MPAKA JUNI 10, 2013.

Wilfred Muganyizi Lwakatare (kwenye gari) akirudishwa rumande. (Picha na Maktaba Yetu)
Kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare, leo imeahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu baada ya hakimu aliyetakiwa kusiliza kesi hiyo kuwa likizo. Lwakatare anakabiliwa na kesi ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki na amerudishwa rumande mpaka tarehe tajwa.

WASHIRIKI WA BIG BROTHER 2013 (THE CHASE)

Ghana - Selly.
Angola  - Biguesas.
Botswana - Motamma.

Wanafunzi watakiwa kukataa kurubuniwa.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba, amewataka wanafunzi wa elimu ya juu kukataa kurubuniwa na watu wachache ambao hawaitakii mema Tanzania.

 Kauli hiyo aliitoa mjini hapa juzi wakati alipozindua Mpango Kazi wa Kitaifa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ambapo wameanza na vyuo vikuu vilivyopo Dodoma.
 
Alisema kumekuwapo na baadhi ya watu wanaotoka nchi za magharibi na hivyo kuwarubuni Watanzania na hivyo kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini.

“Baadhi ya watu wachache ambao wanatoka nchi za magharibi ndio wamekuwa wakituharibia amani yetu hasa pale Mtwara, watu hao wamejaribu kuandika vipeperushi hadi kuviweka rangi ili tu kuwarubuni kwa kuwa wana Mtwara hawawezi kufanya hivyo,” alisema Simba.

Aliwataka wanafunzi hao kutoshabikia mambo yasiyokuwa na msingi na badala yake wasome kwa bidii na wasijihusishe na fujo ambazo hazitawasaidia kitu.

Watoto waliozaliwa watano wafariki dunia.

WATOTO watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja wamefariki dunia. 

Aliyewazaa watoto hao ni Sophia Mgaya (28) mkazi wa Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Watoto hao waliishi kwa saa 10 tu. 

Mama yao ni mwajiriwa mpya wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika shule ya sekondari Luhawasi mjini Songea.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Benedict Ngaiza alisema watoto hao watano walizaliwa baada ya miezi minane.

Alisema watoto hao walikuwa wakiendelea vizuri ingawa wote walikuwa na uzito mdogo huku mwenye uzito mkubwa akiwa na gramu 820 na mwenye uzito mdogo akiwa na gramu 430.

Dk. Ngaiza alisema kitendo cha kuzaliwa kabla ya muda stahili kimechangia watoto hao kufariki dunia.

Watoto hao walizikwa katika makaburi ya Lilambo mjini Songea.

Brazil kufuta madeni ya Afrika.

Rais wa Brazil Dilma Rousseffalitoa matamshi yake katika mkutano wa AU nchini Ethiopia
Brazil imetangaza kuwa itafutilia mbali au kuwa na makubaliano mapya kuhusu madeni inayozidai nchi za Afrika ambayo yanakisiwa kuwa dola milioni 900.

Miongoni mwa nchi 12 zilizo kwenye orodha ya mataifa yanayodaiwa ni pamoja na Congo-Brazzaville yenye uitajiri mkubwa wa mafuta na gesi, Tanzania ambayo hivi karibuni itaanza kuchimba gesi pamoja na Zambia
Wadadisi wanahisi kuwa hii ni njia mojawapo ya Brazil kutaka kukuza uhusiano wa kiuchumi kati yake ambayo ni ya saba kwa ukubwa kiuchumi na Bara la Afrika.

Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa uhusiano wa Brazil na bara la Afrika umeongezeka mara tano katika mwongo mmoja uliopita.

Tangazo hili, lilitolewa wakati wa ziara ya tatu kwa miezi mitatu ya rais wa Brazil Dilma Rousseff,aliyehudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika nchini Ethiopia.
"takriban madeni yote huenda yakafutwa , '' alisema msemaji wa Rais Rousseff Thomas Traumann.
"ili kukuza uhusiano kati ya Afrika ni muhimu kwa sera ya kigeni ya Brazil."
Aliongeza kuwa nyingi ya madeni hayo yaliongezeka miaka ya sabini na kuwa kulikuwa na mazungumzo kuyahusu wakati huo.

NAY APANGUA SKENDO YA KUKATALIWA NA WEMA.

WIKI iliyopita tulimleta kwenu msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma aliyomshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ili umchambue ambapo mlituma maswali, hapa anajibu na kufafanua moja baada ya lingine. SHUKA NAYO…Habari na Global Publishers.
Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
PONGEZI
Nakukubali sana kaka na ngoma zako unavyochana ukweli, kaza buti utafi ka mbali. Roja, Dar, 0657888221
NAY WA MITEGO: Asante.
VIPI KUHUSU NISHA?
Nay wa Mitego uliwahi kuwadisi Bongo Movies na kusema kwamba wanawake wote wanaojiuza wanatoka kwenye tasnia hiyo, je, ilikuwaje ukatoka na Salma Jabu ‘Nisha’ kwani yeye si mmoja wa Bongo Movies? Rocky, Moshi, 0715289337
NAY WA MITEGO: Sijawahi kutoka na Nisha ni mshkaji wangu tu.
YEYE NA DIAMOND
Kwanza hongera kwa kazi zako nzuri kaka, naomba kufahamu kuhusu ule wimbo uliokuwa ukimrekebisha tabia dogo (Diamond), hivi aliyetunga ni wewe au yeye au mlikaa chini na kutunga pamoja? Siyo siri umetulia hongereni sana. Julianitha Jamushi, Dar, 0712089824
NAY WA MITEGO: Asante, Muziki Gani tumeandika pamoja.
USHAURI
Nakukubali kiukweli Nay, mistari yako imesimama kinoma kwani unawachana live, wewe usiwaogope endelea kuwachana mpaka watakapobadilika. Joseph, Dar, 0757247473
NAY WA MITEGO: Hivyo ndivyo ilivyo.

KINANA NAPE WATUA IRINGA, KUANZA ZIARA NJOMBE LEO.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE MEI 27,2013.

7 bc1433 47ad94 8bbe81 d20b2

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka.

Dar es Salaam. 
Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.


Habari zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.


                                          Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako 
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.

Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.

Matokeo ya awali

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.


HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate