EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 27, 2013

TWIGA CEMENT WAMKABIDHI SARUJI MISS TANZANIA 2013, KWAAJILI YA UJENZI WA BWENI SHULE YA ALBINO BUHANGIJA

Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa (kushoto) akipokea mfano wa vocha ya kuchukulia saruji mifuko 300 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, Pascol Lesoinne (kulia)Dar es Salaam jana kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Wengine pichani ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert  Makoye na Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha Dsouza. Ujenzi wa Bweni hilo ni mradi wa Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred ambao upo mbioni kukamilika.

WANASIASA CHONDECHONDE KUCHEZEA AMANI YA NCHI,MNAOMBWA KUACHA KUTUMIA LUGHA ZA UCHOCHEZI---MH:SOPHIA SIMBA

pix_2_85b85.jpg
Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.
pix_4_e5b06.jpg
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.

MAGARI MANNE YAGONGANA NA KUSABABISHA VIFO MBEYA


          WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MAGARI MANNE KUGONGANA NA
                                                              KUSABABISHA VIFO.  
§  MNAMO TAREHE 26.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO KATIKA MTEREMKO WA PIPE LINE INYALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T.605 AXX /T.480 CAX AINA YA  SCANIA LORI LIKITOKEA NCHINI ZAMBIA KUELEKEA DAR – ES SALAAM LIKIENDESHWA NA DEREVA WILSON  MACHA, AKIWA NA TINGO WAKE JUMA S/O SALEHE WOTE WAKAZI WA DSM [AMBAO KATIKA AJALI HIYO WOTE WAMEFARIKI DUNIA] LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.548 BLY/ T.974 BVN AINA YA  SCANIA LORI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL  ARON, MIAKA 30, MBENA, MKAZI WA SINZA, KISHA GARI HILO LILILIGONGA GARI T.876 BKV/T.465 BQU AINA YA  IVECO LORI AMBALO LILIKUWA LIMEEGESHWA PEMBENI YA  BARABARA LIKIWA LIMEHARIBIKA, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMWEL  KASUSU, MIAKA 37, MJITA, MKAZI WA GONGO LA MBOTO DSM.

  AIDHA GARI HILO  T.605 AXX /T.480 CAX LIKIWA LIMEPOTEZA MWELEKEO LILIGONGANA USO KWA USO NA GARI T.255 AKV/T.272 CDZ AINA YA  SCANIA LORI LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI AMBALO LILIKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA SIXTUS S/O KAPINGA, MIAKA 35,MNGONI, MKAZI WA DSM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA MWILI WAKE KUTEKETEA KWA KUUNGUA MOTO.

  KATIKA AJALI HIYO  MAGARI MAWILI T.605 AXX /T.480 CAX  NA  T.255 AKV/T.272 CDZ  YOTE YAMEUNGUA VICHWA NA KUTEKETEA NA GARI  T.548 BLY/ T.974 BVN LILIUNGUA KIDOGO SEHEMU YA  KICHWA UPANDE WA KULIA.

  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI T.605 AXX /T.480 CAX.

  MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI NA WANANCHI.

  MIILI YA MAREHEMU WILSON  MACHA NA JUMA  SALEHE IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JITIHADA ZA KUUTOA  KATIKA GARI MWILI WA MAREHEMU  SIXTUS S/O KAPINGA PAMOJA NA KUTOA MAGARI ENEO LA TUKIO  ZINAENDELEA.  

   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.



Signed By:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

    PICHA NA MDAU W MBEYA YETU

Thursday, September 26, 2013

KATIKATI YA KUMUOZA BINTI MIAKA 14, POLISI WAIVUNJA NDOA

Binti wa miaka 14, Zubeda akiwa tayari kufunga ndoa na Hamis (35).
Stori: Gladness Mallya
NDOA iliyokuwa tayari kufungwa na shehe kati ya Hamis Ngaumba (35), mkazi wa Bangulo, Ulongoni, Gongo la Mboto, Dar na binti wa miaka 14 anayetajwa kwa jina moja la Zubeda, imesambaratishwa na polisi wa Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kutokana na umri wa bi harusi kuwa mdogo, Amani limeidaka hiyo.
Kizaazaa hicho cha aina yake kilichovuta hisia za wengi kilitokea saa 10:00 jioni, Jumapili iliyopita ambapo Shehe Bakari Mgesa wa Msikiti wa Bangulo alikuwa ameanza kutoa mawaidha ya maandalizi ya kufungisha ndoa hiyo lakini ghafla polisi na mapaparazi waliingia na shughuli kuishia hapo.

PICHA ZA AWALI ZA KWANZA ZINAZO ONESHA JINSI WESTGATE ILIVYO HARIBIWA.



Carnage: The collapse came on Monday, shortly after large explosions rang out followed by billows of smoke
Carnage: The collapse came on Monday, shortly after large explosions rang out followed by billows of smoke
Destruction: Cars are strewn among the carnage, which was caused by Kenyan soldiers who fired rocket-propelled grenades inside the complex, knocking out a support column, a government official said
Destruction: Cars are strewn among the carnage, which was caused by Kenyan soldiers who fired rocket-propelled grenades inside the complex, knocking out a support column, a government official said
Conflicting reports: A minister said the terrorists had set mattresses on fire, causing the roof to collapse
Conflicting reports: A minister said the terrorists had set mattresses on fire, causing the roof to collapse

Nyie ni watu wabaya: Mtoto wa miaka 4 awaambia magaidi

Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.



Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.


Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.


Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.


Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.


WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOSOVO.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver Hoxhaj walipokutana Mjini New York kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Hoxhai.
Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Mhe. Membe wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo. Kulia ni Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje, Bi. Tully Mwaipopo, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York na Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Waziri.

Tanzanian Minister of Defence and National Service visits South Darfur.

 At UNAMID South Darfur Headquarters: UNAMID South Darfur Chief Mr. Imtiaz Hussain briefs the minister and his delegation on the status of security situation in his area of responsibility. On the minister’s left is Member of Parliament for Mlalo Brigedier General  Hassan Ngwilizi.
 Jotting down the minutes (left) is Gen. Muazu

MAN UNITED YALIPA KISASI YAICHAPA LIVER POOL 1-0 .


 Meneja wa timu ya Manchester United, David Moyes (wa pili kulia) akiwapungia mashabiki wa timu yake kuwashukuru baada mchezo wao na Liverpool, timu yake imeibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Chicharito.

 Beki wa Manchester United, Jonny Evans, (chini) akimdhibiti mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez, wakati wa mchezo huo.

WANAUME WAMPA MAKAVU MSICHANA ALIYETANGAZA KUTAFUTA BASHA WA KUMUOA, WASEMA WANA WASIWASI NA UTIMAMU WA AKILI YAKE!



 Msichana aliyejitangaza kuwa anahitaji mume wa kumuoa hatimae amepewa makavu live na wanaume na kusema kuwa huenda akili ya bint huyo haiko sawa kwa kitendo alichokifanya.

Hii ndiyo taarifa aliyoitoa dada huyo

 Mimi ni  binti  mjasiliamali  ambaye  nimechoka  kuishi  peke  yangu  na  sasa nahitaji mwanaume  wa  ndoa  anayejiheshimu  na anayejua kupenda.Umri  wangu  ni  miaka 25, elimu  yangu  ni  form six.

 Asilimia kubwa ya wanaume ni wasumbufu  na  wana wanawake  wengi,kitu  ambacho  kwa  upande  wangu sikitaki  maana  najijua  nina  wivu....

Kwa  yeyote mwenye sifa hasa ya kuja kuwa mume mwema  ambaye  atanipenda  kwa  dhati  na  hatanisaliti  basi anijibu  kupitia  email  yangu. 

Kwa  upande  wangu  namhakikishia  kuwa  ntampenda  kwa  dhati, Sitamsaliti, ntamheshimu  na  ntawapenda  ndugu  na  jamaa  zake  wote  kwa  moyo  wangu  wote.

Mawasiliano: 
Email yangu  ni nancybast4@yahoo.com

WATU WAWILI WAKAMATWA NA MAITI YENYE MADAWA YA KULEVYA TUMBONI HUKO TABATA.

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na maiti, iliyokuwa na pipi 33 za dawa za kulevya aina ya heroin tumboni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova alitaja waliokamatwa kuwa ni Nasri Omari (36), maarufu kama Rajabu Robot na Mwanaisha Salim( 36), mkazi wa Kigogo Luhanga.
 
“Kila pipi ina urefu wa sentimita sita...tulipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa huko Tabata kuna mtu mmoja alifariki ghafla muda mfupi baada ya kutoka bafuni kuoga na tukaamua kulifuatilia tukio hilo” alisema.
Alisema makachero walifika eneo la tukio, nyumbani kwa Omari na kuhoji hatimaye kugundua uwepo wa maiti sebuleni ikiwa imelazwa chali katika godoro sakafuni huku akiwa hana nguo na amefunikwa na shuka.

WASANII MANAIKI SANGA NA IRINE UWOYA PICHA ZAO WAKIWA KWENYE MAHABA MAZITO ZAZUSHA BALAA!


 Wasanii Manaiki Sanga na Irene Uwoya wakiwa kwenye picha za mahaba huku Uwoya akigida bieeeee hadi kuche.

Wednesday, September 25, 2013

SERIKALI YAIPONGEZA TIMU YA WASICHANA AIRTEL RISING STARS.


Mkurugenzi wa masoko wa Airtel, Levi Nyakundi akiongea wakati wa hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising Stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria, hafla hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt.
Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini, Angetile Osiah akiongea wakati wa hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising Stars.
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising Stars, Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising Stars.
Wachezaji waliozawadia kwa kungar'a katika michuano ya Airtel Rising Stars pamoja na nahodha wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, Leonard Thadeo (mwisho kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Naodha wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17 Stumai Abdallah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria Jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Kaptain ya timu ya wasichana Stumi, akikabithi cheti cha kushinda kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada ya kuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria Jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Mchezaji wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dola 10,000 iliyokabidhiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka washindi wa michuano ya Airtel Rising Stars Afrika. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.

MFANYA BIASHARA ANASWA LIVE GEST NA MKE WA MTU...ALIA AMESEMA AMEKOMA.

Stori: Brighton Masalu
SHETANI anazidi kuiatamia dunia, ulimwengu unawayawaya! Jamaa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Manfree, mkazi wa Kimara Mwisho, Dar ambaye inadaiwa ni mfanyabiashara wa baa iliyopo Mbezi Mwisho (Mbezi Shamba) anadaiwa kunaswa na mke wa mtu (jina tunalo), Risasi Mchanganyiko linaibumburua.
Manfree baada ya kunaswa na mke wa mtu gesti.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lililoongeza faraja na furaha ya shetani kule kuzimu, lilijiri juzikati huko Kimara Mwisho ndani ya gesti moja (jina lipo kwenye droo zetu).
Mtuhumiwa akiomba msamaha kwa mwenye mke.
ALIYENASA AANZA KUMWAGIKA
Akizungumza kwa uchungu mkubwa, mume wa mwanamke huyo ambaye hakupenda jina lake liupambe ukurasa huu, alisema siku nyingi Manfree amekuwa akimsumbua mke wake, hali iliyokuwa ikimpa wakati mgumu mwanamme huyo mwenye mke.
“Jamaa amekuwa akimsumbua sana mke wangu, nilipokuja kuzipata taarifa hizi nilishangaa sana lakini pia niliumia kama mwanamme,” alisema mwenye mke huyo.
Mwenye mke (kushoto) akiongea na mke wa mtuhumiwa.
MAZOEA YALIPOANZA
Kwa mujibu wa mume huyo, kufahamiana kwa Manfree na mkewe kulikolea zaidi baada ya mwanamke huyo kuhitaji fremu kwa ajili ya biashara ya duka ambapo kwa kutumia uenyeji wa jamaa huyo, alionesha kutaka kumsaidia.
SINEMA YA KUNASWA ILIPOANZA
Mwanamme huyo aliendelea kusema kuwa sinema ya kunaswa kwa mwanamme huyo ilianza siku moja baada ya yeye kwenda kwenye baa ya jamaa huyo kuangalia mpira (hakuzitaja timu).
Alisema akiwa hapo baa, mara mke wake alitokea na kukaa kwenye kiti, meza nyingine. Jamaa huyo naye akaenda kukaa na mke wa jamaa na kuanza kuzungumza.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate