EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, July 28, 2014

JAJA, COUTINHO SASA KUANZA MAISHA MAPYA NDANI YA KARIAKOO

Uongozi wa Yanga umekamilisha kila kitu kuhusiana na nyumba watakayoishi washambuliaji wake Jaja na Coutinho raia wa Brazil eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Jaja na Coutinho waliouomba uongozi wa Yanga waishi Kariakoo karibu na makao makuu ya klabu yao badala ya kupelekwa kwa ‘wanene’, Masaki au Oysterbay.
JAJA&COUTINHO WAKIWA MAZOEZINI NA KIKOSI CHA YANGA...
Habari za uhakika zinasema tayari Yanga imelipa nyumba hiyo na ilikuwa katika hatua za mwisho za ukarabati.

AUNT AKERWA NA MASHOGA



KERO! Mtendea haki sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa anakerwa sana na wanaume wenye hulka za kike (mashoga).
Staa wa sinema za Kibongo Aunt Ezekiel.
Akichonga na paparazi wetu, Aunt alisema mashoga wanamstaajabisha kwa jinsi wanavyojiweka na kujishaua katika jamii kitu ambacho anaamini ni tabia mbaya ambayo mtu anaweza kuiacha mara moja.
“Mashoga hunistaajabisha sana kwa kweli, kila niwaonapo sijui  najisikiaje? Nawashangaa kweli, kwa nini wasibadilike,” alisema Aunt.

NIMEMPATA - PAM D FT MESEN SELEKTA - DOWNLOAD & KUSIKILIZA HAPA


BAHATI BUKUKU NUSU KIFO!

Stori: Oscar Ndauka
NI kweli ajali haina kinga! Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi, Ijumaa Wikienda lina undani wa mkasa mzima.
Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Muonekano wa gari hilo kwa ubavuni kulia.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

ASKOFU ATAKA USHAURI WA RAIS UHESHIMIWE


 Askofu mstaafu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Dodoma, Mhashamu Mathias Isuja.
WATANZANIA wameshauriwa kuendelea kuheshimu hadhi na mamlaka aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kwa kuthamini na kuzingatia mwongozo na ushauri mbalimbali anaoutoa kwa wananchi, kwani mamlaka hayo yanatoka kwa Mungu.
Askofu mstaafu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Dodoma, Mhashamu Mathias Isuja, amesema hayo jana katika mahubiri yake maalumu wakati wa Misa ya Jumapili katika Parokia ya Makole, Jimbo Katoliki la Dodoma. Misa hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiaskofu Jimbo la Kondoa.
Askofu Isuja, ambaye ni Askofu wa kwanza Mtanzania katika jimbo hilo, aliwataka Watanzania waombe Mungu, ili ajalie busara na hekima katika kutenda na kuamua mambo mbalimbali yahusuyo nchi, hasa kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya.

Saturday, July 26, 2014

NEW AUDIO: NIMEMPATA - PAM D MIC QUEEN FT MESEN SELECTOR

SHEKHE MKUU ATANGAZA SWALA YA IDD KITAIFA

  Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao maalumu katika Ofisi za  Mkoa wa Dar es Salaam za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) hii leo, Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo sambamba na hotuba mbalimbali inatarajiwa kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo inatarajiwa kuwa siku ya Jumatatu Julai 28 au Jumanne  Julai 29 mwaka huu.

Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa Kiislamu na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika saa 9 Alasiri katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni Rasmi wa Baraza hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.

ALICHOKISEMA LULU BAADA YA ALI KIBA KUACHIA NYIMBO MBILI MPYA

 
Ali Kiba ameachia  nyimbo mbili  kwa  mpigo ambapo response ya mashabiki ni nzuri. Sasa kupitia Instagram star wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu" amefunguka mambo mengi  sana  kuhusiana  na  Ali Kiba.......Hiki  ndicho  alichokisema:
 
"Haya sasa.....maelezo hatimaye yamepatikana....mnivumilie ni marefu Kidogo...! 

1. Pongezi kwa @officialalikiba nimesikia Mwana wa Dar es Salaam tu lkn kiukweli Mimi binafsi umenikonga moyo...! 

2. Ieleweke kwamba Mimi ni shabiki wa mziki mzuri hata ukiwa umeibwa na underground na wengi wenu mmekuwa mashaidi maana huwa na post video nikiimba miziki ya watu tofauti hata wasio mastar wakubwa...kwahyo mm sio shabiki wa mtu ni shabiki wa kazi ya mtu

ALI KIBA, DIAMOND WAFIKA PABAYA!

Na Sifael Paul/GPL
Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:

DAVINA APEWA KIPIGO KIKALI NA MUMEWE


KIBANO! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kupewa kipigo kikali na mumewe, muda mfupi baada ya kukutwa akiongea kimahaba na simu iliyodaiwa kupigwa na mwanaume mwingine.
Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa msanii huyo, Mbezi-Beach, Dar, Julai 22, mwaka huu ambapo Davina alikutwa akizungumza na mwanaume ambaye haikujulikana mara moja ni nani ndipo mumewe alipomshushia kipigo ‘hevi’.

MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kchwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa.

Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani.
Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.

YEMI, SHILOLE KUFANYA MAAJABU TAIFA


WAKATI hamu ya mashabiki kila kona kwa sasa ni Agosti 8, mwaka huu katika tamasha kubwa la kihistoria la Usiku wa Matumaini litakalofanyia Uwanja wa Taifa jijini Dar, mashabiki wengi wanatamani kuwaona wakali kibao wakipanda jukwaani na kupiga nyimbo zao kali.
Diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade
Good newz ni kwamba Zuwena Mohamed ‘Shilole’ atapanda jukwaa moja na diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade kudondosha shoo ya kihistoria.
Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu nchini.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA LEO‏

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwela ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda leo Julai 25, 2014.

BAHATI BUKUKU APATA AJALI


Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amepata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Akiongea kwa simu Bahati amesema: “Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia  iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.
“Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama.”
Taratibu za kumhamishia Bahati kutoka Hospitali ya Kongwa kuja Muhimbili zinafanywa na ndugu pamoja na marafiki.
Tunakuombea upone haraka Bahati.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate