Waigizaji wakongwe kwenye tasnia ya filamu
Bongo, Jacob Steven ’JB’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamempigia saluti
muigizaji mwenzao, Kajala Masanja kutokana na filamu fupi
aliyotengeneza ya Mbwa Mwitu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Mlimani City juzi, JB alisema kuwa
Kajala amebuni kitu cha tofauti kabisa ambacho jamii nzima mpaka watoto
wanafahamu kuhusu Mbwa Mwitu.


