Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba sasa hivi mastaa wa
Tanzania, hasa wanaofanya vizuri kwenye fani ya filamu wako katika kuvuja jasho
jingi ili kupata mafanikio makubwa na kuwashinda wengine.
Vinywa vya wadau siku za karibuni vimekuwa vikiwataja mastaa
wawili kwamba ndiyo wanaoongoza kwa ukwasi au kwa lugha nyingine utajiri
mkubwa. Mastaa hao ni Jackline Wolper na Wema Sepetu ambao wako juu katika
mafanikio kwa wasanii wa kike Tanzania ya leo.
Mwaka jana mwanzoni, Aunt Ezekiel ndiye aliyeonekana kuja
juu kwa mafanikio hasa baada ya kuandikwa kwamba anamiliki pub maeneo ya
Kinondoni. Tishio lake liliingiliana na pub ya msanii mwingine aitwaye Zuwema
Mohamed au Shilole.
Hata hivyo, mwaka 2012 ulipoanza, kasi ya wasanii hao
ilikuwa imepungua kwa kiasi kikubwa huku Wolper na Wema wakibaki kuwa
washindani wakubwa hapa mjini. Kwa sasa Wolper anamiliki magari matatu, nyumba
kubwa yenye nafasi, kampuni ya filamu na inasemekana ana miradi kadhaa ambayo
humwingizia fedha.
Utajiri wa wema katika picha hapo chini.
No comments:
Post a Comment