Na Shakoor Jongo
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Bongo
Beats cha StarTV, Sauda Mwilima (pichani) amepata pigo baada ya mtoto
aliyejifungua Juni 12, mwaka huu kuwa siyo riziki yake.
Chanzo chetu
cha habari ambacho ni rafiki wa karibu wa mtangazi huyo, kikizungumza na
Ijumaa kilisema Sauda alipata uchungu wa kujifungua mishale ya jioni.
Kiliongeza kuwa, baada ya kupatwa na hali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi iliyopo Kinondoni B jijini Dar ambapo iligundulika kwamba mtoto alifia tumboni.
Kiliongeza kuwa, baada ya kupatwa na hali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi iliyopo Kinondoni B jijini Dar ambapo iligundulika kwamba mtoto alifia tumboni.
“Inawezekana mtoto alifia tumboni wakiwa njiani
kumleta hapa,” alisema mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo aliyeomba
hifadhi ya jina.
Sauda alipotafutwa kwa njia simu ili kusikia kauli yake kuhusiana na masahibu yaliyomkuta hakuweza kupatikana lakini mumewe, Kauli Juma ambaye yuko Afrika Kusini alikiri kutokea tatizo hilo.
Sauda alipotafutwa kwa njia simu ili kusikia kauli yake kuhusiana na masahibu yaliyomkuta hakuweza kupatikana lakini mumewe, Kauli Juma ambaye yuko Afrika Kusini alikiri kutokea tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment