WANAWAKE wengi hasa waishio nchi zinazoendelea wamekuwa
wakipanga uzazi kwa kutumia dawa wanazopewa na ushauri wa namna ya
kuzitumia.
Lengo la ushauri huo ni kuepuka kuzaa bila mpangilio huku wakiaminishwa kuwa dawa hizo zinawasaidia.
Dawa hizo licha kuwapatia madhara, lakini wengi wao wamekuwa wakikaa
kimya na kuugulia madhara wanayoyapata, tena bila kujaza fomu ambazo
baadhi ya watumiaji wamedai kuwa hawafahamu lolote kuhusiana nazo.
Mbali na shirika hilo kutetea uhai nchini, pia huwa linazunguka barani
Afrika kueleza na kutetea madhara yatokanayo na dawa hizo, utoaji
mimba, elimu kwa vijana, usafi wa roho na mambo mengine.
Katika utafiti niliofanya mkoani Mbeya na vitongoji vyake, ukiandaliwa
na kudhaminiwa na Shirika la Kutetea Uhai wa Binadamu Tanzania
(PROLIFE), niligundua kuwapo kwa wanawake wengi ambao wamepata madhara
baada ya matumizi ya dawa hizo.
Kabla sijaendelea na namna utafiti ulivyofanyika na madhara
waliyoyapata, nianze kwa kueleza aina ya dawa na vidhibiti mimba
vitumiwavyo.
Kuna aina tano ya vidhibiti mimba, nazo ni vidonge vya majira
vitumiavyo chachu za bandia za projestorini na estrojeni
zilizotengenezwa katika maabara ambapo mwanamke humeza kila siku.
Zipo aina mbalimbali za vidonge, majina ya vidonge hutegemea aina na kiwango cha chachu zilizowekwa.
Vidonge vyenye chachu ya estrojeni pekee huitwa vidonge na vidonge
vyenye mchanganyiko wa chachu ya estrojeni na projestini huitwa vidonge
mchanganyiko.
Vidonge vyenye chachu aina ya projestini pekee huitwa: Progestorene Only Pills (POP) au Low Dose Pill au Mini Pill.
Leo hii vidhibiti mimba vingi vimetengenezwa kwa chachu hii pekee
ambayo ni morning After Pills, RU486, Emmergency Contraceptives.
Aina ya pili ni vipandikizi ambapo mashirika yanayoendeleza njia za
kisasa za kupanga uzazi wanasifia vipandikizi, kama ni njia nzuri na
salama kwa wanawake wanaotumia.
Mashirika hayo yanadai kuwa, njia hii ni rahisi kwani inaondoa ile
adha ya kumeza vidonge kila siku, zoezi ambalo baadhi ya watumiaji
husahau.
Hii ni chachu au homoni iitwayo ‘levonorgestrel’ inayowekwa katika
vifuko 6. Baada ya kuwekwa, huanza kufanya kazi saa 24 hadi miaka 5.
Kila kifuko huwekwa mg 36 za chachu ya ‘crystalline levonorgestrel’ na
kila kimoja kina urefu wa mm 34 na upana wa mm 2.4. Kiasi cha mg 30 ya
projestini husambazwa katika damu kila siku.
Aina ya tatu ni kondomu inayotumika kwa mwanaume na mwanamke pia. Kwa kawaida kifaa hiki hubana kufuatana na umbile la mtu.
Kondomu zimegawanyika katika aina tatu; ya kwanza ni zile
zilizotengenezwa kwa utumbo wa kondoo zinazosemekana kuwa hazina uwezo
mkubwa zikitumika kama kidhibiti mimba.
Aina ya pili ni zile zilizotengenezwa kutokana na mpira wa latex.
Watengenezaji wanazisifia kuwa na ubora mkubwa zinapotumika au kama
kidhibiti mimba au kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa maambukizo ya
magonjwa ya zinaa ikiwemi virusi vya ukimwi (VVU).
Aina ya tatu ni kondomu zilizotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mpira na vitu vingine ziitwazo “polyurethane.”
Soko la kondomu limepata umaarufu zaidi kuanzia miaka ya 1980 kufuatia kuzuka na kuenea kwa janga la ukimwi.
Aina ya nne ya vidhibiti mimba ni kitanzi. Hiki ni kifaa kidogo cha
plastiki chenye vinyuzi mwishoni, ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba
kupitia uke.
Mtumiaji anaweza kugusa nyuzi hizo kama anataka kujua kitanzi alichoweka bado kipo.
Baadhi ya wanawake ambao nilipata kuzungumza nao baada ya Mkurugenzi
wa Prolife, Emil Hagamu kutoa mafundisho, walieleza madhara na kusema
kuwa mwanzo hawakujua wanaumwa nini, na matatizo yao yanatokana na nini.
Scola Yusuph alieleza: “Mimi nilitumia vidonge, lakini nikawa natoa
harufu mbaya katika sehemu zangu za siri na nilipimwa nikaambiwa nina
fangasi.”
Naye Agness Raphaely anasema baada ya kutumia sindano aina ya depo
provera akawa hajisikii hamu ya tendo la ndoa japo kabla ya kutumia
alikuwa akifurahia.
Zawadi Kilembe ameeleza kuwa, alichoma sindano Januari 13 mwaka huu na akaanza kupata siku zake mfululizo hadi Aprili 17.
Anasema alikuwa anaumwa sana kila siku hadi kufikia kulazwa, na kusema
madhara mengine aliyopata ni kukonda, kichefuchefu, kichwa kuuma,
kuumwa tumbo na chembe moyo.
Katika tafiti ya kwanza iliyoshirikisha zaidi ya wanawake 350,
wanawake 150 kati yao walieleza madhara waliyoyapata kutokana na dawa
hizo.
Tafiti hii pia iliendelea hadi Mbeya vijijini ambako nilibahatika
kukutana na wanawake wa Kanisa la Moravian katika Kijiji cha Igoma,
ambao wanaeleza matatizo wanayoyapata baada ya kutumia dawa za uzazi wa
mpango.
Elizabeth Brayson anasema baada ya kutumia vidonge alipata matatizo ya kuumwa kichwa na kutoka damu mfululizo.
Anasema baada ya kupata shida hiyo, aliamua kwenda hospitali na
kushauriwa abadilishe na kuweka vipandikizi maarufu vya vijiti.
Imelda Mwakilasa anasema baada ya kuchoma sindano moja alikosa hamu ya
tendo la ndoa hali iliyosababisha kuwa na mgogoro wa mara kwa mara na
mumewe, na ilimchukua miaka minne na alipata kizunguzungu na kichwa
kuuma, kiasi kwamba hata alipokunywa dawa kilikuwa hakiponi.
Hao ni baadhi tu ya wanawake ambao wameumizwa na matumizi ya dawa hizo.
Mkurugenzi wa Prolife, Hagamu, anaeleza dhima nzima ya shirika hilo na
kusema kuwa ni kulinda, kutetea na kudumisha uhai wa binadamu, kutetea
hadhi na heshima yao kwani vidhibiti mimba vinaharibu hekalu la Mungu.
Dhima nyingine ni kufundisha njia za uzazi wa mpango kupitia maumbile
ya mwanamke, elimu ya usafi wa moyo, na kutengeneza taifa la mtetezi wa
uhai.
Habari na Happiness Mnale wa Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment