Watu wenye silaha wemeishambulia
helikopta iliyokuwa ikibeba vifaa vya uchaguzi vitakavyotumika kwa
ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa Jumamosi nchini Libya, maafisa
wa nchi hiyo wamesema.
Helikopta hiyo ililazimishwa kutua nje ya mji wa
mashariki wa Benghazi. Taarifa ambazo hazijathitishwa zinasema mtu
mmoja amefariki.
Utambulisho
wa washambuliaji bado haujajulikana, lakini eneo la mashariki mwa Libya
limekosa utulivu kutokana na makundi yanayotafuta uhuru wa kanda hiyo.
Uchaguzi wa wabunge ni za kwanza nchini humo baada Marehemu Muammar Gaddafi kupinduliwa mwaka jana.
Habari hizi zinakuja wakati watu wenye silaha wamefunga vituo vitatu vya kuuza nje mafuta kupinga uchaguzi huo.
Watu hao wamekasirishwa kwamba eneo la magharibi
ya nchi limepewa viti 200 zaidi katika Bunge jipya ikilingalishwa na
eneo la mashariki lenye utajiri wa mafuta.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, nusu ya vituo vya Libya vya kuuza nje mafuta vimefungwa kutokana na hali hiyo.
"Helikopta iliyobeba masanduku ya kura iliruka
juu eneo la Hawari Kusini mwa Benghazi ambapo alipigwa kwa kuwa kutumia
silaha ndogo," AFP limenukuu shirika la habari Kanali Ali al-Sheikhi
likisema.
Alisema mtu mmoja aliuawa, lakini shirika la
habari la Reuters linamnukuu rasmi akisema kuwa mtu mmoja aliyekuwa
ndani ya helkopta alijeruhiwa wakati helikopta alipopigwa kombora la
kutungulia ndege.
Via BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment