EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, July 19, 2012

JOKATE, WEMA BIFU HADI KIFO



Wema Sepetu.

Jokate Mwegelo.
Hamida Hassan na Gladness Mallya
KUTOELEWANA kati ya ma-Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (No. 1) na Jokate Mwegelo (No.2) (pichani) kumeendelea kushika kasi na sasa bifu lao lina kila dalili ya kwenda hadi mwisho wa maisha yao, Amani lina shuka na ushahidi wa kutosha.
Awali bifu la wawili hao lilidaiwa kuwa chanzo chake kilitokana na Jokate kuunga uhusiano wa kimapenzi na msanii nyota wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ huku akijua wazi ana uchumba na Wema.
Uadui ulianzia hapo, Wema akalia sana kupitia vyombo vya habari, lakini mara zote Jokate amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond licha ya kwamba ushahidi wa kimazingira umekuwa ukikidhi kwamba wawili hao wanatoka pamoja.
 
Kufuatia hali hiyo, Wema na Jokate wakawa maadui wakubwa huku jamii ikiwatazama kwa macho ya chongo kuhusu uhusiano wao kuharibiwa na kitu mapenzi.
Juni 2012, baadhi ya wadau wakiwatumia waandishi wa habari wa Global Publishers, waliandaa mchakato wa kuwaweka chini wawili hao ili kuwapatanisha hata kwa kutumia vitabu vya Mungu ambavyo vina vipengere vinavyoelekeza binadamu kusameheana.
Mpango huo ulianza kwa Jokate kuitwa kwenye ofisi za Global zilizopo, Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam lakini bila kuambiwa anachoitiwa.
Lengo lilikuwa kwamba akikubali kupatana na mwenzake, Wema naye angeitwa ambapo mazingira yalionesha kupatikana kwake ni rahisi kuliko Jokate.

ALICHOKUWA AKIJIBU JOKATE
Pamoja na kupigiwa simu wakati mwingine akitumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu ‘SMS’, Jokate akawa anapiga danadana kwa kutoa udhuru wa kawaida.
“Nitakuja, kuna mambo nayaweka sawa kwanza, nikishayakamilisha nitakuja, kuna nini kwani?”
Paparazi: Kuna mambo ya kuzungumza ya kawaida lakini.
Jokate: Oke, nitakuja jamani.
Hata hivyo, mpango wa Jokate kufika Global ulishindikana baada ya kuendelea kudai kuna mambo anayaweka sawa kwanza.
 
Ndipo paparazi aliyepewa jukumu la kumsaka staa huyo na kumfikisha ofisi za Global kisha aitwe Wema alipoamua kumuwekea wazi modo huyo kuhusu kuwepo kwa mpango wa kuwapatanisha yeye na Wema.
Aidha, paparazi alimgeukia Wema ambapo alimpigia simu na kumwelezea ‘ei tu zedi’ kuhusu zoezi la kupatanishwa na hasimu wake Jokate.

JOKATE AFUNGUKA
“Mimi sitaki kabisa, sitaki kabisa kupatanishwa kwani sina kisirani na huyo mtu (Wema) wala sitaki na siwezi kushindana naye.”

MSIKIE WEMA NAYE
Wema naye, bila kujua Jokate amejibu nini, aliwaka kama moto wa kifuu akisema:
“Siwezi kupatana na Jokate kwa sababu simpendi huyo mtoto hata kabla hajaniibia Diamond wangu. Hata wakiwepo watu wa kutupatanisha, mimi siwezi kumsamehe.
“Nilimsamehe Jack (Wolper) kwa sababu watu walikuwa wanatuchonganisha na lile bifu langu na yeye lilikuwa la kisichana tu.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate