Kitendo hicho kilimfanya ajisikie mpweke kwani hadi wazazi wake walimtaka kujitoa katika kundi hilo ili tu kunusuru maisha yake kuwa matatani.
Wakati akizungumza na mwandishi wa DarTalk, Rayuu alionekana kuumia sana kwani kiongozi huyo hakuwa na haya kutokana na umri wake kuwa mkubwa na yenye alikuwa kama mtoto wake.
Rayuu katika pozi
“Yani nikikumbuka ishu hiyo huwa naumia sana kwa sababu nilikuwa ni mdogo sana, na hadi wazazi waliamua kuambia niacheni na tasnia hiyo,” alidai.
Rayuu hata hivyo aliongeza kuwa kiongozi huyo nia yake ilikuwa kutembea ili ampe nafasi kwenye tamthilia zao ambazo zilikuwa zinafanya vizuri miaka hiyo.
“Lengo lake lilikuwa afanye mapenzi na mimi ili anipe nafasi kwenye tamthilia, na sikuwa tayari niliamua kuwambia wazazi wangu ambapo nao walikuja juu ingawa waliamua niachene na kundi hilo,” aliongeza.
Via Dar talk.
No comments:
Post a Comment