KWAMBA mwishoni mwa wiki iliyopita vurugu kubwa zilitokea kwenye
mkutano wa hadhara zikiwahusisha wafuasi wa Chadema na CCM zimesababisha
kifo cha mtu mmoja katika Kata ya Ndago, wilayani Iramba, mkoani
Singida hakika ni habari za kusikitisha sana.
Tunaambiwa kwamba katika vurugu hizo, wafuasi wa vyama hivyo vikuu vya siasa nchini walishambuliana kwa kutumia silaha za jadi, ikiwamo mawe wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na kusababisha kifo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV-CCM) wa kata hiyo ya Ndago, Yohana Mpinga.
Jeshi la Polisi mkoani Singida limethibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kifo cha mwenyekiti huyo wa UV-CCM na kusema kwamba linawashikilia watu 18 wa kata hiyo kwa mahojiano na watakaobainika kuhusika na ghasia hizo watafikishwa mahakamani, huku likiendelea na msako wa kuwatafuta watu wengine waliohusika katika tukio hilo.
Mpaka sasa wafuasi wa vyama hivyo bado wanatupiana lawama ambazo hazijaweza kuthibitishwa na mamlaka husika, lakini polisi wanadai kwamba baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwapo katika mkutano huo waliwarushia mawe wafuasi wa Chadema kwa madai kwamba viongozi wao waliokuwa wakihutubia mkutano huo walikuwa wakitoa kauli za kumkashifu Mbunge wao wa jimbo hilo la Iramba Magharibi, Mwingulu Nchemba (CCM).
Pamoja na kwamba hatuna mamlaka ya kutoa hukumu kuhusu upande unaopaswa kulaumiwa kwa kusababisha vurugu hizo, kwa ujumla wetu tunalazimika kulaani vurugu hizo kwa nguvu zetu zote. Vyama hivyo viwili vimekuwa na uadui na mvutano mkubwa kati yao kwa muda mrefu sasa, hivyo kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na vitendo vya kuhujumiana na kudhoofishana kisiasa ambavyo vimezaa ushindani kati yao tunaoweza kusema umevuka mipaka kwa kiwango chochote kile.
Hali inakuwa mbaya zaidi uhasama huo unapovuka mipaka kutoka uhasama wa kisiasa kati ya vyama hivyo hadi uhasama kati ya mbunge na mbunge. Sote ni mashuhuda wa uhasama kati ya wabunge hao wawili ambao ulikolezwa hivi karibuni na mbunge huyo wa Ubungo baada ya kumtuhumu bungeni mwenzake wa Iramba Magharibi kwamba ni mmoja wa watuhumiwa waliokwapua fedha za EPA.
Pamoja na kukosa ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai hayo kama alivyoamuriwa na Bunge, mbunge huyo wa Ubungo aliamua kupeleka mashtaka kwa wapigakura wa hasimu wake huyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuhutubia mkutano wa hadhara ambao ulipigwa mawe na wafuasi wa mshindani wake huyo katika Jimbo la Iramba Magharibi. Wakosoaji wa mbunge huyo walisema haikuwa wakati mwafaka wala busara kwake kumkandia hasimu wake kwenye jimbo lake hilo la Iramba Magharibi, lakini Mbunge Mnyika anadai kwamba mbunge huyo ndiye aliyeanzisha uchokozi kwa kumwaga fitina kwa wapigakura wake katika jimbo lake la Ubungo hivi karibuni na kusema hatua yake hiyo ililenga kulipiza kisasi.
Wapo watu wanaodai kwamba waliovurumisha mawe katika mkutano wa mbunge huyo wa Ubungo walitumwa na Mbunge Mwingulu Nchemba. Lakini kama tulivyosema hapo awali, hakuna tuhuma ambazo zimethibitishwa hadi hivi sasa, licha ya ukweli kwamba siyo sisi wala watu wanaotoa tuhuma kwa pande hizo mbili walio na mamlaka ya kisheria kutoa hukumu. Kwa maneno mengine, tuziachie mamlaka husika siyo tu zifanye uchunguzi ulio huru, bali pia zitoe uamuzi wa haki na usioacha shaka yoyote.
Hata hivyo, tukio hilo la Singida lazima lizifumbue macho mamlaka zote zinazohusika katika kusimamia na kuratibu shughuli za vyama vya siasa. Ndiyo maana moja ya maswali magumu yanayoulizwa kuhusu vurugu hizo za Singida ni hili: Ilikuwaje mkutano huo wa hadhara wa Chadema uliokuwa na kibali cha Jeshi la Polisi haukupewa ulinzi wa kutosha?

No comments:
Post a Comment