EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, July 5, 2012

Mgomo wa madaktari wawagawa wanasheria

WANASHERIA wametoa maoni tofauti kuhusu  mgogoro wa madaktari unaoendelea nchini na Serikali inavyoushughulikia, baadhi wakidai Serikali ipo sahihi, wengine wakipinga kwa madai kuwa imeingilia mahakama.   

Wakili wa Kujitegemea, Harold Sungusia alisema kuwa kitendo cha Rais kutoa maelekezo kwa madakatari siyo tatizo, lakini maelezo yenye uamuzi ni kuingilia uhuru wa mahakama.  Julai mosi katika hotuba yake kwa taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mambo mengine alizungumzia mgogoro wa madaktari akielekeza kuwa daktari anayetaka kufanya kazi arudi kazini na asiyetaka ajiondoe mwenyewe.  Akizungumzia kauli hiyo ya Rais, Sungusia alisema: 

"Kitendo hicho ni kuingilia uhuru wa mahakama, wakati ambapo bado Mahakama Kuu haijatoa uamuzi wake kuhusu kesi iliyofunguliwa Mahakama ya Kazi na Serikali dhidi ya madaktari."  Alisema kuwa kuna mgawanyo wa madaraka katika mihimili mitatu ya taifa aliyoitaja kuwa ni Dola, Mahakama na Bunge akieleza kuwa kwa kauli hiyo ya Rais Kikwete, Serikali imetumia vibaya dhana ya uhuru wa mahakama ambayo ni moja ya misingi ya utawala bora.  

Alisema Serikali imekuwa na utaratibu wa kukosoa watu  wanaojadili jambo lolote lililo mahakamani, wakati huohuo yenyewe imekuwa ikiingilia katika utendaji wake.  “Serikali ni ya kwanza kukosoa watu wanapojadili jambo fulani kwa kisingizio kuwa lipo mahakamani. Wakati huohuo yenyewe ndiyo ya kwanza kuingialia mahakama,’’ alisema Sungusia.  Wakili huyo alisisitiza kuwa Serikali imekuwa ikiingialia uhuru wa mahakama kila mara, akitolea  mfano  kesi ya mgombea binafsi .  

Alieleza  kuwa wakati kesi ya mgombea binafsi inaendelea mahakamani, Serikali iliamua kurudi  bungeni haraka na kubadilisha kipengelea ndani ya Katiba kuzuia mgombea binafsi kuwania nafasi ya uongozi.   Naye Mwanasheria Pendael Munisi alisema Bunge linaweza kujadili jambo hilo kwa kuwa linahusisha masilahi ya umma kwa mujibu wa Ibara 63(3)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.  

‘’Ibara hiyo inaeleza kuwa Bunge linaweza kutekeza  mamlaka yake na wabunge wanaweza kumuuliza waziri yeyote, jambo lolote kama linahusu masilahi ya umma,’’alisema Munisi.  

Mwanasheria huyo alilisitiza kuwa Ibara 4 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelezea mgawanyo wa madaraka kwa mihimili yote mitatu ambapo kila mhimili utatekeleza kazi zake kwa mujibu wa katiba na  haipaswi kuingiliana katika uamuzi yake.  Hata hivyo, alisema kuwa upande mwingine mgawanyo huo wa madaraka kivitendo haupo, kwa sababu Rais anaweza kuamua jambo lolote kwa masilahi ya umma na kwamba hatua hiyo ya Rais Kikwete ni kulinda uhai wa wananchi ambao maisha yao yapo hatarini kwa mgomo huo wa madaktari.  

Alisema kuwa ili mihimili hiyo mitatu ifanye kazi bila kuingiliana kiutendaji sheria zote zinapaswa kufanyiwa marekebisho makubwa na kuondoa mkanganyiko ulipo huku akitolea mfano wa kifungu cha 64 (1)© kinachomkataza mbunge kujadili jambo lililo mahakamani wakati Ibara ya 100 na ile 63(3)(a) inaeleza uhuru wa Bunge kujadili jambo kwa masilahi ya umma.   

Naye Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alisema haoni kama Serikali imeingilia uhuru wa mahakama akiwataka  wananchi kujisomea na kujua sheria badala ya kukurupuka.  

Mwanasheria Mwandamizi Francis Kayichire alisema Serikali ipo sahihi kwa kuwa,  mahakama ikishatoa hukumu Serikali inatekeleza majukumu yake.   

Alisema mahakama ilishaeleza kuwa mgomo wa madaktari ni batili hivyo Serikali inapaswa kuchukua hatua kwa wale wanaokwenda kinyume na  mahakama. 
Imeandaliwa na Aisha Ngoma, Daniel Mwingira na Pamela Chilongola na Geofrey Nyang’oro  e&p
VIA: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate