MSANII, Wastara Juma, akiwa na jopo la wasanii na watu maarufu
nchini, wanatarajiwa kuzindua filamu yao mpya itakayokwenda kwa jina la
‘Sayla’.
Filamu hiyo, imepangwa kuzinduliwa katika mikoa minne ya Arusha, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wastara, aliwataja baadhi wadau na
wasanii waliocheza filamu hiyo kuwa ni pamoja na Wema Sepetu, Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji na Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM), Ester Bulaya.
Wengine ni Mbunge wa Kawe, (CHADEMA), Halima Mdee, Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, watangazaji maarufu, Maimatha Jesse,
Ephraim Kibonde na wengineo.
Aliongeza kuwa mhusika mkuu katika filamu hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Dunamic Minds ni Angela Karashani.
Wastara ambaye ni mke wa muigizaji, Juma Kilowoko ‘Sajuki’
amewashukuru Watanzania kwa msaada wao wa hali na mali na kuwataka
wamuunge mkono katika ununuzi wa filamu hiyo, ambayo mapato yake
yatakwenda katika kumsaidia Sajuki na familia yake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment