Jumla
ya ajali 17 zimeripotiwa mkoani Morogoro katika kipindi cha sikuku ya
EID katika ajari hizo kuna baadhi zimesababisha vifo na nyingine
zimesababisha majeruhi.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile ametaja ajari
zilizosababisha vifo kuwa ni ajari ya pikipiki ambayo ilitokea Agosti 20
saa 1.00 asubuhi katika eneo la Michenga Ifakara katika barabara ya
Mlimba ambapo amemtaja Inocent Njoka (29) mfanyakazi wa Taasisi ya Afya
Ifakara aligonga kalavati na kupinduka na kusababisha kifo.
Kamanda Shilogile amesema chanzo acha ajari ni mwendokasi wa mwendesha pikipiki hiyo.
Aidha
kamanda ametaja ajari nyingine kuwa ni ajari ya gari iliyotokea Agosti
20 majira ya saa 4.30 asubuhi katika kijiji cha Msowero tarafa ya mikumi
katika barabara ya Mikumi Ifakara gari ikiendeshwa na dereva
asiyefahamika jina ilimgonga mwendesha baiskel ambaye jina lake
halikufahamika mwenye umri unaokadiliwa kuwa ni miaka 45-50 na
kusababisha kifo cha mwendesha baiskel.
Kamanda
Shilogile amesema uchunguzi zaidi wa ajari hiyo unaendelea ili
kumkamata mtu aliyesababisha ajari hiyo na kuwa chanzo cha ajari hiyo ni
mwendokasi wa gari hiyo.
No comments:
Post a Comment