EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 22, 2012

Barua: CWT-Mbeya inamtaka Mkuu wa Mkoa awaombe radhi kwa kuwakashifu walimu na CWT

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)
(Tanzania Teachers’ Union – TTU)
MKOA WA MBEYA

P.O. Box  3079, MBEYA

E-mail: ttumbeyareg@yahoo.com              

Telephone:  2502535,  Cell:  0784-830564, 0715-830564, 0764-163234     
Your Ref: ............................................                                                                                                Date: 21/8/2012 

Our Ref: CWT/MBY/MW/VOL.II/57
                                                      
MKUU WA WILAYA,
S.L.P 255,
MBEYA

     YAH: Kuwakashifu walimu na CWT wakati wa semina za sensa ya watu na makazi

Tafadhali husika na mada tajwa hapo juu.

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Mbeya kwa masikitiko sana kimepokea toka kwa walimu malalamiko juu yako kuhusiana na jinsi ulivyowakashifu wakati wa zoezi la semina za sensa ya watu na makazi. Kwa nyakati tofauti, ulipita kwenye vituo vya semina hizo ambazo wengi walikuwa walimu na kutoa kashifa dhidi ya walimu na taaluma yao pamoja na CWT. Baadhi ya kashifa ambazo ulitoa ni kama ifuatavyo:-

  1. Ulikuwa ukieleza kuwa walimu ni kada ya waliofeli mitihani na hivyo serikali inawashangaa kudai waongezewe mishahara.
  2. Ulieleza kuwa walimu wamejaa madudu kichwani.
  3. Ulieleza kuwa walimu ni manjuka yaani watu mbumbumbu wasiojua kitu chochote.
  4. Ulikuwa ukiwaeleza walimu kuwa Mukoba (Rais wa CWT) anamiliki pesa nyingi toka CWT hivyo hata akigoma na kufukuzwa kazi hatapata shida yoyote ya maisha, hivyo anawadanganya walimu wanaogoma.
  5. Ulikuwa ukieleza kuwa CWT kinawanufaisha makatibu na viongozi kuliko walimu maana wao wanatembelea magari kwa pesa zenu na hivyo ni kwa nini walimu waigomee serikali badala ya kukigomea chama chao cha CWT.
  6. Ulikuwa ukieleza kuwa washiriki wa semina hawatakiwi kuugua, kufa wala kufiwa kabla ya zoezi la sensa kuisha ila baada ya sensa wanaruhusiwa kuugua, kufa na kufiwa maana serikali haitakuwa na hasara yoyote.

Kwa mantiki hiyo, walimu wametafakari na kuona kuwa kauli hizo ulizotoa kwao tena wakiwepo washiriki wengine wasio walimu zimewadhalilisha, kuwafadhaisha na kuwafanya wadhaulike kwenye jamii na hivyo kuathirika kisaikolojia. Aidha, CWT kimeona kuwa ulikuwa na lengo la kuvuruga zoezi zima la sensa ya watu na makazi kwani uliondoa utulivu wa

washiriki wa semina na kuwafanya wajadili zaidi juu ya kauli zako zenye kila aina ya maudhi. CWT hakiwezi kuvumilia viongozi wa serikali wa aina hii wasioheshimu na kuthamini walimu waliowafundisha na waliopewa dhamana ya kuelimisha umma wa nchi hii.  Aidha, CWT kinajiuliza kama ulipoteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbeya ulitumwa kuja kuwakashifu walimu? Je, ulitumwa kuja kuwakosanisha walimu na CWT yao? Je, sera unazotekeleza kweli ni za Chama tawala au ni za kwako mwenyewe? CWT kinaamini kuwa hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kwani hakuna anayeweza kukutuma hayo. Kutokana na kashifa hizo kwa walimu na chama chao unatakiwa ufanye yafuatayo ili warudishe moyo wa kuendelea kukuamini:-

  1. Uwaombe radhi walimu ndani ya siku 7 kwa kila kituo cha semina ya sensa na makazi ya watu ulichopita na kutoa kauli hizo.
  2. Umuombe radhi Rais wa CWT mwl. Gratian Mukoba ndani ya siku 7, uliyedai amejiulimbikizia fedha za CWT.
  3. Uwaombe radhi makatibu na viongozi wa CWT ndani ya siku 7 uliodai wanajinufaisha na CWT kuliko kuwanufaisha walimu.

Nakujulisha kuwa, kama utashidnwa kufanya hayo matatu juu, CWT kitaingia kwenye hatua nyingine zaidi kwani walimu walioathirika na kauli hizo wako tayari kwa hatua yoyote itakayochukuliwa na CWT.

Nakutakia kazi njema.

Mwl. Kasuku Bilago
Katibu CWT Mkoa
Mbeya

Nakala:

    1) Waziri Mkuu
         S.L.P 980
         Dodoma

    2) Katibu Mkuu CWT
       S.L.P 61110
       Dar es Salaam
  
   3) Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
       S.L.P 4865
       Dar es Salaam

   4) Mkuu wa Mkoa
       S.L.P 754,
       Mbeya
  
   5) Makatibu CWT (W)
       Mkoa wa Mbeya
nakala hii imepatikana via blogu ya Kalulunga

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate