Athari ya mlipuko wa bomu mjini Tripoli
Maafisa wa usalama wa Libya wamesema mabomu mawili yaliyokuwa kwenye gari yamelipuka katikati ya mji mkuu wa Tripoli,
moja karibu na ofisi ya wizara ya mambo ya Ndani na jingine karibu na chuo cha kijeshi.
Taarifa
zinasema milipuko hiyo imeua watu wawili na kuacha wengine wanne
kujeruhiwa katika chuo cha zamani cha kijeshi cha wanawake.
Hili ni shambulio kubwa la kwanza kutokea tangu
kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar
Gaddafi mwaka jana.
Mkuu wa Usalama wa mji Tripoli amelaani
mashambulizi hayo yaliyolengwa kwa watu wanaomuunga mkono rais wa zamani
wa nchi hiyo marehemu Mummar Gaddaf.
Katika hosptali ya Al Jalaa iliyopo Tripoli,
Wesan Abu Alsoude ambaye binamu yake aliuawa amelaumu mamlaka kwa
kushindwa kuchuchukua hatua kuzuia shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment