EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, August 21, 2012

Dk Slaa akamatwa

Dk Slaa Frederick Katulanda Bukombe  na Shija Felician, Kahama SIKU tatu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuonya kile alichokiita ajenda ovu za Chadema kutaka kuvuruga nchi, jana Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa na wabunge wawili wa chama hicho wameitiwa mbaroni na polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa kwa madai ya kufanya mkutano wa wa uchochezi katika Jimbo la Maswa Mashariki. Akituhutubia taifa katika utaratibu wake wa kila mwisho wa mwezi, Rais alionya akisema Chadema kimekuwa kikitumia fursa ya kufanya maandamano ya kidemokrasia huku wakiwa na lao jambo ambalo ni kuvuruga amani ya nchi. Wakati mjadala wa hotuba hiyo ukiwa haujatulia, jana habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Kamanda wa Polisi

Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani zilisema Dk Slaa alikamatwa mnamo saa 8: 05 asubuhi kwa madai ya kufanya mkutano katika Kijiji cha Malampaka wilayani Maswa kilichopo Jimbo la Maswa Mashariki, linaloongozwa na John Shibuda. Hata hivyo, Shibuda hajashiriki maandamano yoyote ya chama chake yanayoendelea. Wabunge waliokamatwa pamoja na Dk Slaa ni Rachel Mashishanga na Chiku Obwao ambao ni wa viti maalum.

Walikamatwa na polisi mjini Kahama baada ya polisi kuzingira Hoteli ya Pine Ridge walikokuwa wamefikia wakitokea Maswa. Kamanda Athumani alisema viongozi hao wa Chadema ambao wako kwenye mpango wao wa maandamano ya amani Kanda ya Ziwa walikamatwa wakati wakijianda kwenda Wilaya ya Bukombe kuungana na wenzao kabla ya kuelekea mkoani Kagera kuendelea na mikutano yao. Kamanda huyo alisema juzi, Dk Slaa na wabunge hao wakiwa wilayani Maswa walifanya maandamano na baadaye kufanya mkutano wa uchochezi katika Mji wa Malampaka bila kutoa taarifa Polisi na baadaye kukimbilia wilayani Kahama ambako waliungana na wenzao.

“Kawaida ukiwa na mkutano ni lazima ufike polisi na kutueleza kuwa unataka mkutano ama maandamano na sisi tutakubaliana na wewe baada ya kuridhishwa na sababu za mkutano wako,” alieleza Kamanda huyo wa Polisi. Alisema mkutano huo ulikuwa nje ya ratiba na barua yao kwa vile wakati wakitoa taarifa hawakueleza iwapo watafanya mkutano katika mji huo wa Malampaka. “Walifanya mkutano huo nje ya ratiba ya kibali chao cha kufanya  maandamano mkoani Shinyanga ambacho jeshi la polisi linacho hivyo ilikuwa kinyume cha taratibu na sheria, tulimfuata alipolala na kutaka kupata maelezo yake,” alisema Kamanda Athumani. Wakiongozwa na Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Shinyanga (RCO), Kashindye Hussen polisi waliwakamata viongozi hao wa Chadema na kuwapeleka Kituo Kikuu cha Polisi ch Wilaya hatua ambayo ilisababisha wafuasi wengi wa chama hicho kumiminika hapo kujua hatma ya viongozi hao.

 Kamanda Athumani katika maelezo yake alisema Dk Slaa na wenzake waliieleza polisi kwamba wao wakiwa viongozi wa juu walifanya mkutano wao kwa nia njema na kwamba walisimama hapo wakijua kuwa viongozi wao wa wilaya walikuwa na mawasiliano na polisi. Viongozi hao wote waliachiwa kwa dhamana na Kamanda huyo alisema jeshi lake linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasaka viongozi wa wilaya ili kujua aliyehusika kuandaa mkutano huo. Mbowe aliwaambia waandishi wa habari jana wilayani Bukombe kwamba Dk Slaa alifuatwa na ofisa wa polisi akitakiwa kufika kituoni wilayani Kahama ambako alikaa muda wa saa moja akitoa maelezo yake.

 “Polisi walikuwa wakimshutumu kwa kufanya mkutano katika eneo ambalo halikupangwa, lakini Dk Slaa aliwaeleza kuwa kazi ya kuandaa mikutano siyo yake ni ya viongozi wa Wilaya ya Maswa hatua mbayo iliwafanya kumuachia na sasa tunaendelea na safari yetu ya Mkoa wa Kagera,” alisema. Baada ya kuruhusiwa kuondoka mjini Kahama Dk Slaa aliungana na viongozi wenzake wa Chadema na jama mchana walifika katika Mji wa Kemondo mkoani Kagera ambako walipokewa na viongozi wa chama hicho wa mkoa huo na kisha kuelekea mjini Bukoba

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate