EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 20, 2012

Eh! Mtoto azaliwa na meno 32, mvi, nyewele kwapani kwa ujauzito uliodumu "miaka 3"

Gazeti la HabariLeo la Jumapili, Agosti 19, 2012 lina taarifa ifuatayo:

Msichana mkazi wa kijiji cha Mpasa mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa amejifungua mtoto asiye wa kawaida baada ya ujauzito wa zaidi ya miaka mitatu.

Mtoto aliyekuwa kivutio na gumzo kijijini hapo na kwingineko, alizaliwa Agosti mosi, akiwa na meno 32 ambayo ni idadi ya mtu mzima na nywele zenye mvi utosini huku mzazi Lucia Sabastiano (18) akidai kuwa hakuwahi kukutana kimwili na mwanamume yeyote maishani mwake.

Mtoto huyo ambaye alifariki dunia baada ya siku mbili, alikuwa wa kiume, huku pia akiwa na sehemu za siri zilizokomaa kama za mtu mzima ambazo zilikuwa na nywele ndefu sehemu hizo.

Maumbile mengine ambayo yalionekana kuwa ya ajabu ni pamoja na midomo kuwa myekundu, mikono na miguu yenye kucha ndefu na viungo vingine vikionekana sawa na vya mtu mzima.

Akizungumzia tukio hilo jana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpasa, Privatous Maliyatabu alisema msichana huyo ambaye alipata ujauzito huo akiwa mwanafunzi wa darasa la tano, alijifungua saa 10 alasiri nyumbani kwa mjomba wake aliyetajwa kwa jina moja la Mwelela. Maliyatabu alisema Lucia alijifungua kwa msaada wa mkunga wa jadi aliyejulikana pia kwa jina moja la Mama Pashaa, baada ya kupewa dawa ya kunywa na mganga wa jadi, Maneti Mazimba.

Kwa mujibu wa Lucia, licha ya kupata ujauzito huo, bila kukutana kimwili na mwanamume maishani mwake, alidai kutojua jinsi alivyopata ujauzito huo na kudumu nao miaka mitatu, “Nakumbuka siku moja nilisimama mlangoni mwa nyumba yetu na ghafla nikaona kama mwujiza, mwanga mkali mbele yangu na kisha kujitokeza sura ya mwanaume ambaye siwezi kuhadithia umbile lake na akatoweka na tangu hapo, nilianza kuhisi tumbo kujaa na kuhisi kiumbe kikicheza,” alidai Lucia.

Baadaye aliwaeleza wazazi wake ambao walimpeleka hospitali baada ya kuona tumbo lake linaongezeka siku hadi siku, lakini kwa nyakati tofauti Lucia alipimwa katika hospitali tofauti na kuambiwa hakuwa na ujauzito. Alisema:“Kila waliponipima waliniambia kuwa sina mimba, lakini miye nilikuwa nikihisi kitu kama mtoto kinacheza tumboni kwa kipindi chote cha miaka mitatu, hali hiyo ilizidi kunishangaza.”

Mmoja wa ndugu wa Lucia ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wana uhakika ndugu yao hajawahi kukutana na mwanamume maishani mwake na familia nzima ilishangazwa na ujauzito wake, “Lucia ni miongoni mwa watoto watatu katika tumbo la mama yetu, na amekuwa akitushangaza kwa yaliyokuwa yakimtokea tangu apate ujauzito huu, kwani mara nyingi usiku amekuwa akiweweseka, hali iliyofanya tuanze kuhangaika naye kwa waganga wa jadi baada ya hospitali kutueleza kuwa hana kitu tumboni,” alisema mwanandugu huyo aliyejitambulisha kuwa ni dada yake.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dkt. Emmanuel Mtika alisema kitaalamu ujauzito unatakiwa kuwa kati ya wiki 38 na 40 na ikizidi sana wiki 42 hadi kujifungua na kuongeza kuwa hakuna ujauzito wa miaka mitatu, “Inawezekana huyu mwanamke alikuwa na matatizo ya uvimbe tumboni kwa muda mrefu na akapata ujauzito wa muda wa kawaida ihali yeye akiamini kuwa alikuwa mjamzito kwa kipindi kirefu kumbe sivyo,” alisema Dkt. Mtika.

Alisema kinachoshangaza ni maelezo ya kudai kuwa mjamzito bila kukutana na mwanamume, kwani hakuna mwanamke anayeweza kupata ujauzito kwa hali hiyo, “Inawezekana kuna mwanamume alitaka kufanya naye mapenzi kwa nguvu, lakini hakufikia sehemu mwafaka na labda mbegu za kiume zilimwagika karibu na sehemu zake za siri na kumwingia, hapo uwezekano wa kupata ujauzito upo,” alisema Daktari.

Hata hivyo, Dkt. Mtika alisema mwanamke huyo hakwenda hospitali kubwa kupata vipimo ili kubaini tatizo lililokuwa likimsumbua kwa kipindi chote hicho.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate