KUNA
madai kwamba ule ‘mkoko’ wa kifahari wa staa wa maigizo Bongo,
Jacqueline Wolper aina ya BMW X6 lenye Namba za Usajili T574 BXF
linatarajiwa kuingizwa sokoni wakati wowote na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) baada ya muda aliopewa nyota huyo kulipia deni lake la
kukwepa ushuru wa shilingi milioni 70 kupita bila mwenyewe kusema
chochote.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni, umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya mnada.

Chanzo kingine kilisema kuwa
mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe, kumekuwa na usumbufu mwingi
kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo baadhi ya matajiri nao
wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la kulinunua.
“Tunashangaa sana, watu na fedha zao wanakuja hapa kulitaka gari la
Wolper, mbona kuna magari mengi yapo toka mwaka juzi (2009) hawaji
kuyanunua au kwa sababu hili ni la supastaa wa Bongo?” alihoji
mfanyakazi mmoja wa TRA akiomba jina lake lisitajwe gazetini.
Akaongeza: “Unajua tatizo liko wapi? Baadhi ya wafanyakazi wa TRA nao wamekaa mkao wa kusubiri siku ya kutajwa kwa tarehe ya kulipiga mnada gari hilo ili wasuke mipango ya kupata cha juu kutoka kwa matajiri watakawaopigia debe na kushinda,” kilisema chanzo.

Amani lilipoongea
na Wolper kuhusu gari lake hilo likitaka kujua nini kitatokea kama
hatalikomboa kwa siku alizopewa na TRA ambazo zimepita, alijibu hivi:
“Kisheria gari linatakiwa likombolewe ndani ya miezi mitatu lakini mimi niliandikisha kuwa kwa mwezi mmoja nitakuwa tayari nimemaliza kila kitu. Hata hivyo, kimsingi na mimi nilimfikisha polisi Ndama Mtoto wa Ng’ombe ambaye alisimamia ununuzi wake mwanzo hadi mwisho. Kwa hiyo kama ni kukwepa ushuru ni yeye.

Gari la Wolper lilikamatwa Juni 28, 2012
kwa madai ya kukwepa ushuru, hadi Agosti 28, mwaka huu litakuwa
limefikisha miezi mitatu ambayo ni ya kisheria lakini mwezi mmoja
aliotaka Wolper uliisha Julai 28, 2012 hivyo kutoa fursa kwa TRA
kutangaza siku ya kulipiga bei.
Wolper alilinunua gari hilo kwa shilingi milioni 250 za Kitanzania likiwa na sifa nyingi tofauti na magari mengine.
Wolper alilinunua gari hilo kwa shilingi milioni 250 za Kitanzania likiwa na sifa nyingi tofauti na magari mengine.
Sio tar 28 august ni 28 sept ndio litakua limefikisha miezi 3
ReplyDelete