PAMOJA na sherehe za Idd el Fitry kufana katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam lakini kwa familia ya Mzee Said haikuweza kufurahia kutokana na msiba uliowapata baada ya mtoto wao mpendwa Abduhafidh said (12), kupoteza maisha katika ajali iliyotokea wiki iliyopita.
Mtoto huyo
alipoteza maisha katika ajali ya gari namba T 645 AVG alilokua
akisafiria baada ya kuacha njia na kutumbukia mtaroni saa tisa alasiri
katika barabara ya Mjimwema, Kigamboni eneo la Machava.
Gari hilo lililokua likiendeshwa na Hakini Makame (40), lilikua limebeba watoto wawili ambapo mmoja alifariki na mwingine kujeruhiwa na lilikua likitokea Feri kuelekea Ufukwe wa Mikadi.
Mwandishi wetu alishuhudia ajali hiyo ikitokea kwani gari moja lililokuwa mbele ya gari lililopinduka, lilisimama ghafla ndipo Makame alipojaribu kulikwepa na kwa bahati mbaya gari lake likatumbukia mtaroni.

Mtoto aliyejeruhiwa
alishindwa kutaja jina lake kutokana na hofu iliyomshika, alikua wa
kwanza kutoka katika gari hilo huku mwenzake akiwa amebanwa na gari na
lilipovutwa alikutwa ameshafariki dunia.
Mtoto huyo alipoona Abduhafidh amefariki alilia kwa uchungu, hali iliyofanya mashuhuda kumuonea huruma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

No comments:
Post a Comment