HUKU
wadau wakiwa na shauku kubwa ya kumjua mshindi wa shindano hili la
kumsaka staa wa kike mwenye mvuto ambaye hajaolewa
‘The Ijumaa Sexiest
Girl’, hatimaye kura za wasomaji zimeamua msanii wa filamu, Jackline
Wolper kutoa mkono wa kwaheri.Mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema
alisema:
“Mtifuano ulikuwa mkali sana na hii ilitokana na ukweli
kwamba, wote waliobaki ni wakali kuanzia sura hadi maumbo yao.
Wopler
ametolewa na sasa kimbembe ni kati ya Wema na Agnes.”
Kufuatia
matokeo hayo ya Wolper kuchapa lapa, sasa wanabaki Wema na Agnes ambao
watapigiwa kura kwa wiki mbili kabla ya kumpata mshindi.
Ili kushiriki
katika hatua hii muhimu ya kumpata mshindi, andika jina la mshiriki
kisha litume kwenda namba 0786-799120.
No comments:
Post a Comment