Mshindi
wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo Bw. Amin Joseph
Maro akiingia ndani ya gari yake aina ya Ford Figo baada ya kukabidhiwa
na Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru,
hafla hiyo imefanyika jioni ya siku ya jana kwenye bustani ya Nyerere Square
mjini Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine
Tengia, wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Allan Chonjo, meneja wa bia
ya Serengeti Premium Lager sambamba na Wanahabari .
Meneja
wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bwa. Allan Chonjo akifafanua
jambo mbele ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na wadau wengine
kutoka sehemu mbalimbali waliofika kulishuhudia tukio la kukabidhiwa kwa
gari aina ya Ford Figo kwa mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini
ya Kizibo Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya
leo ndani ya bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo Bw. Amin Joseph Maro akizungumza mbele ya Wanahabari waliofika kulishuhudia tukio hilo jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma,kulia kwake ni Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia.
Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia akizungumzia furaha alionayo mbele ya Wanahabari mara baada ya mtoto wake kujishindia gari mpya kabisa aina ya Ford Figo kupitia promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment