Stor:Erick Evarist
BAADA ya kuigiza filamu ya Barba ya mkali wa tasnia hiyo, Hajji Adam
‘Baba Hajj’ mwanamuziki wa Bongo fleva, Maunda Zorro ametangaza rasmi
kujitosa katika fani hiyo.
Maunda ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Mkongwe, Zahiri Ally Zorro na
kaka wa mwana-Bongo Fleva Banana Zorro amesema sasa atakuwa akiigiza
filamu mara kwa mara.
“Nilikuwa kimya kwa muda mrefu kwa kuwa nilikuwa nikiipika filamu ya Room Number 13 ambayo nimeuvaa uhusika vilivyo,” alisema.
Hata hivyo, Maunda alisema pamoja na kujikita kwenye filamu hataacha muziki kwa kuwa uko ndani ya damu yake.
No comments:
Post a Comment