EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 23, 2012

Nyumba 300 zabomolewa kata za Mabwepande, madale - Dar es Salaam

Picture
Nyumba takribani 300 zikiwamo za kifahari, zimebomolewa baada ya kubainika kujengwa katika maeneo mbalimbali yaliyovamiwa katika Kata ya Mabwepande na Madale wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.

Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa mashamba iliyoanza jana saa 12 asubuhi, ilifanywa na Serikali ya Wilaya ya Kinondoni chini ya ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na magari yapatayo 30 yakiwamo matingatinga manne na gari la wagonjwa.

Baada ya kuanza operesheni hiyo, kulitokea tafrani kidogo baada ya wananchi waliokuwa katika vikundi kutumia silaha za jadi kama mishale, mapanga kuwashambulia polisi, jambo lililolazimu jeshi hilo kutumia mabomu ya machozi katika kuwatawanya.

Katika operesheni hiyo iliyofanyika kwa awamu, wananchi ambao maeneo yao yalivamiwa, walikuwa wakiongoza kuonesha wavamizi na kisha kubomolewa nyumba na baadaye kuchoma moto nyumba hizo zilizokuwa zimejengwa kwenye eneo hilo ambalo lina vilima vingi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema wametumia nguvu ya wastani katika kusimamia operesheni hiyo na watu takribani 20 wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kuanzisha vurugu.

"Tulipata upinzani kidogo wakati tunaanza, jambo ambalo tulilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya na kuendelea na kazi hiyo. Kazi imefanyika vizuri na hakuna askari wala raia yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa," alisema Kamanda Kenyela ambaye katika awamu ya pili ya bomoabomoa, alitaka kusiwapo na uchomaji moyo nyumba zilizobomolewa.

Alisema katika operesheni hiyo, wamekamata mitambo ya pombe haramu ya gongo na walichobaini ni kuwa eneo hilo lilikuwa maficho ya wahalifu wa ubakaji, ukabaji na ujambazi uliokuwa ukifanyika hapo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na kuwa kazi waliyoifanya ni kuwaondoa wavamizi wapya katika eneo hilo lililovamiwa la kata za Mabwepande na Madale.

"Mgogoro wa hapa ni tofauti, zamani kulikuwa na tatizo la umilikaji wa watu zaidi ya mmoja katika eneo moja, lakini sasa kuna kundi la vijana ambao wanavamia maeneo ya watu na baadaye wanayauza, wengi wa waliobomolewa ni wale waliouziwa na wavamizi," alisema Rugimbana.

via Ziro99 blog

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate