WAKATI baadhi ya taasisi za Kiislamu nchini zikitofautiana kuhusu
ushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi inayoanza kesho, Jeshi la
Polisi limesema litawachukulia hatua za kisheria watakaobainika
kusababisha kuvurugika kwa shughuli hiyo ya kitaifa.
Kwa nyakati
tofauti jana, taasisi hizo na polisi walitoa matamko yao, ikiwa ni siku
moja kabla ya kuanza kwa Sensa ya Watu na Makazi iliyopangwa kufanyika
kwa wiki nzima kuanzia kesho.
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa
Polisi, Paul Chagonja alisema jeshi hilo limebaini kuwa baadhi ya
taasisi na makundi ya watu yanawashawishi wananchi kutoshiriki Sensa kwa
manufaa yao binafsi.
Kwa upande wake, Jumuiya ya Taasisi za
Kiislamu Tanzania kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Sheikh Ponda Issa Ponda
alisema kuwa wataitisha maandamano ili kudhihirisha msimamo wao wa
kugoma kushiriki Sensa ya Watu na Mkazi.
Hata hivyo, Jumuiya ya
Kuendeleza Quran na Sunna Tanzania (Juqusuta), kupitia kwa Kaimu
Mwenyekiti wake, Sheikh Mohamed Said imeitaka Serikali kupuuza
wanaopinga Sensa na kutojishughulisha na vipeperushi vinavyosambazwa
kuzuia watu wasishiriki.
Katika mkutano wake na waandishi wa
habari jana, Kamishna Chagonja alisema tayari baadhi ya watu wamekamatwa
kwa tuhuma za kuvuruga mchakato wa kazi hiyo.
“Hatutawavumilia
hata kidogo watu watakaobainika kuwashawishi wananchi wasishiriki Sensa
kwa namna yoyote, iwe kwa maneno au kuwarubuni kwa fedha,” alisema.
Alionya
kuwa yeyote watakayembaini akijihusisha kwa namna yoyote ile na vitendo
vinavyoashiria kuvunjika kwa amani au kuathiri mchakato wa Sensa,
atashughulikiwa na vyombo vya dola.
Mkoa wa Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema: “Nasikitishwa na makundi haya ya watu ambayo yanahamasisha wengine wasihesabiwe. Nawataarifu kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa sababu kitendo hicho ni kinyume na sheria za takwimu.”

Alisema hadi jana,
maandalizi yote yalikuwa yameshakamilika na makarani wote walioteuliwa
kwa kazi hiyo wameshalipwa posho zao za semina.
Meya wa Manispaa
ya Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema wenyeviti wa Serikali za Serikali
Mitaa watalipwa Sh100,000 kusaidia kufanikisha Sensa.
Mwenda
alitoa kauli hiyo baada ya kuwapo kwa tishio la wenyeviti hao kugoma.
Alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa Sh50,000 na nusu nyingine
itatolewa na manispaa hiyo.
Msimamo wa Sheikh Ponda
Sheikh Ponda alisema Dar es Salaam jana kuwa maandamano hayo yatafanyika Agosti 29, mwaka huu kupinga pamoja na mambo mengine, Serikali kutumia nguvu ya ziada dhidi ya msimamo wao huo.

Awali, alisoma tamko la
Jumuiya hiyo na kuwasisitiza Waislamu kutoshiriki Sensa, huku akiitaka
Serikali kuiahirisha ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha za umma.
Alitaja
sababu nne jumuiya hiyo kugomea Sensa kuwa ni kugubikwa na propaganda
na matumizi ya mabavu na Serikali kushindwa kujenga mazingira rafiki
yakufanyika kwake.
Kuhusu maandamano, alisema yanatarajiwa
kushirikisha wakazi wa mikoa saba nchini ambayo aliitaja kuwa ni Tabora,
Mwanza, Arusha, Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na Dodoma.
Alisema Dar es Salaam, maandamano hayo yataanzia katika misikiti yote iliyopo Kariakoo kuelekea Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Juqusuta wapuuza
Makamu Mwenyekiti wa Juqusuta, Sheikh Hassan Kabeke alisema vipeperushi hivyo vinaonyesha namba za simu hivyo polisi izitumie kuwasaka wahusika akisema hizo ni ushahidi tosha wa kutiwa hatiani kwa wahusika.

Sheikh
Kabeke alisema Uislamu ni dini ya amani na kwamba kuna watu wanaoutumia
kama mtaji wa kujipatia umaarufu na kuwataka Waislamu kukataa kutumiwa
na watu kwa kivuli cha Uislamu kwa masilahi binafsi ya watu.
“Kuna
watu wamefikia hatua ya kuwataka Waislamu kufunga siku tatu baada ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumalizika kwa lengo la kuwalaani wenzao
atakaoshiriki Sensa. Nakuonyeni kuwa huu ni uzushi mkubwa...” alieleza.
Maalim Seif atoa wito
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amewataka Waislamu kushiriki Sensa na kuacha kulalamika kwani msingi wa malalamiko yao ni utengano baina yao hivyo kushindwa kufanya mambo ya maendeleo kama ilivyo kwa waumini wa dini nyingine.

Akizungumza baada ya
Ibada ya Ijumaa katika Msikiti wa Mtoro, Dar es Salaam jana, Maalim Seif
alisema Waislamu walio wengi ni wanafiki na wapo ambao wanaona haya
hata kujitambulisha mbele ya hadhira jambo ambalo haliwezi kuwasaidia
zaidi ya kuwafanya wabakie walipo.
“Mtanisamehe ila lazima niseme
jambo hili. Wengi wetu ni wanafiki, kuna ambao hawawezi hata kutamka
hadharani kuwa wao ni Waislamu,” alisema Maalim Seif na kuongeza:
“Nawaomba masheikh mwondoe hali hiyo ili kuleta tija na maendeleo ya Waislamu nchini.”
Mkoa wa Mwanza
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Mwanza jana walitoa tamko la kutokushiriki Sensa kwa madai kuwa hawajashirikishwa kikamilifu.
Mkoa wa Mwanza
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Mkoa wa Mwanza jana walitoa tamko la kutokushiriki Sensa kwa madai kuwa hawajashirikishwa kikamilifu.
Aidha,
walisema wamesikitishwa na dharau iliyofanywa na waratibu wa Sensa kwa
kuwapa posho ya Sh50,000 kwa siku zote tisa ambazo watakuwa wanafanya
kazi kwa kushirikiana nao.
Kiongozi wa wenyeviti hao, Hamisi
Shindo alisema jana katika ukumbi wa UTPC, Mwanza kwamba walifikisha
malalamiko kwa wahusika, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
“Tuliwaandikia
barua Agosti, 22 mwaka huu na kuwapelekea lakini wameshindwa kutujibu
na tulipomwuliza mkuu wa mkoa alijibu kuwa Ofisi ya Takwimu imesema
haina fedha za kuwalipa wenyeviti wa mitaa,” alisema Shindo.
Mkoa wa Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa amesema ofisi yake imekamilisha maandalizi Sensa ya Watu na Makazi na akawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wanaoandikisha .
Mkoa wa Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa amesema ofisi yake imekamilisha maandalizi Sensa ya Watu na Makazi na akawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wanaoandikisha .
Akizungumza na waandishi
wa habari jana ofisini kwake, Gallawa alionya kuwa atakayeivuruga
shughuli hiyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya
Muheza, Subira Mgalu amekuwa akihamasisha wananchi kujitokeza katika
Sensa ya Watu na Makazi kwa kupita nyumba kwa nyumba usiku. Pia amekuwa
akipita katika masoko mbalimbali yaliyopo wilayani hapa kuwahamasisha
wafanyabiashara ili wajitokeze katika kuhesabiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego amewataka wakazi wake kutambua kuwa Sensa haina uhusiano na itikadi za kidini.
Akizungumza
na wenyeviti wa mtaa na vitongoji wa Wilaya ya Tanga jana, Dendego
alisema lengo la Sensa ni kuwezesha kupatikana kwa takwimu sahihi
ambazo zitatumika kwa ajili ya kupanga maendeleo.
Wilayani Korogwe, madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, wameazimia kufuata kanuni, sheria na taratibu ili kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuhesabiwa.
Wilayani Korogwe, madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, wameazimia kufuata kanuni, sheria na taratibu ili kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuhesabiwa.
Mwenyekiti
wa Wajumbe wa Baraza la Madiwani, Sadick Kallaghe alisema madiwani kwa
kutumia nafasi zao watashirikiana kikamilifu na wananchi ili kukamilisha
mchakato huo unaotarajiwa.
Habari hii imeandikwa na Aidan Mhando, Florence Majani, Joseph Zablon Elizabeth Edward, Fidelis Butahe, Frederick Katulanda, Mashaka Kibaya, Korogwe, Raisa Saidi, Tanga na Sheilla Sezzy, Mwanza.
Habari hii imeandikwa na Aidan Mhando, Florence Majani, Joseph Zablon Elizabeth Edward, Fidelis Butahe, Frederick Katulanda, Mashaka Kibaya, Korogwe, Raisa Saidi, Tanga na Sheilla Sezzy, Mwanza.
No comments:
Post a Comment