MKUU
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amesema kuwa, kuna vikundi vya
watu wachache wa dini ya Kiislamu vinavyowashawishi watu wasihesabiwe
katika mkoa huo.
Gama
alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kueleza
kuwa, kukiwa kumebakia siku moja kabla ya kuanza kwa kazi hiyo, Vikundi
hivyo vipo kwenye Wilaya za Same, Mwanga, Moshi na Hai, ambapo hadi sasa
watu saba ndio waliokamatwa.
Alisema
kutokana na hali hiyo alilazimika kufanya mikutano kwenye wilaya ambazo
tatizo hilo lilionekana kuwa kubwa ili kuwahamasisha wananchi.
Alielezea
changamoto nyingine iliyopo katika Wilaya ya Hai kuwa ni wenyeviti wa
vitongoji kugomea kuwapokea wageni ambao ni makarani wa sensa kwa ajili
ya kuwatembeza kwenye maeneo yao ya kuhesabu watu.
Pia
mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, alikwishapokea malalamiko kwa wenyeviti
wa vitongoji 116 ambao wanadai serikali posho zao tangu 2009 hadi mwaka
jana.
“Ni
kweli nilipokea barua kutoka wenyeviti hao wa vitongoji,lakin maamuzi
yao yalikuwa ni ya pamoja,hivyo uamuzi wa wao kama watahudhuria au
hawatahudhuria itajulikana leo na nilitaka nipate barua ya mmoja mmoja,”
alisema Gama.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment