Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Anthony Rutta amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo anaesadikiwa kuwa ni mganga wa tiba za asili kumefanikiwa baada ya taarifa kutoka kwa msamaria mwema.
Amesema baada ya hizo taarifa askari walikwenda kwenye eneo hilo ambapo baada ya upekuzi na kumuhoji, Msindi alikiri kuhifadhi mabomu hayo ambayo alikua ameyachimbia chini ya ardhi nyuma ya nyumba yake yakiwa ni mabomu manne ya kutupa kwa mkopo ndani ya mfuko.
Kamanda Rutta ameongeza kwamba utafiti uliofanywa na polisi inasemekana hayo mabomu yaliagizwa nchi jirani na lilikua limeandaliwa tukio kwenda kufanya uhalifu kwenye mnada mmoja mkoani Tabora.Via millardayo
No comments:
Post a Comment