Baada ya kupatana kwa muda na kuwa marafiki sasa warembo wawili Sintah na Agnes, wametibuana upya kwa madai kuwa mmoja wao bado anaendeleza kinyongo kitu ambacho kinawafanya washindwe kuelewana.
Chanzo kimoja cha habari ambacho kipo karibu na Sintah kikiongea na mwandishi wa mtandao wa DarTalk kilidai kuwa ingawa walipatana lakini bado hakuna ukaribu wowote uliopo na inaonekana kuwa kila mmoja wao hafurahii urafiki huo.
Chanzo hicho kidai kuwa siku mbili zilizopita wadada hao walikutana lakini cha anajabu hakuna walichozungumza kwani kila mmoja hataki kumsemesha mwenzake kitu ambacho kinafanya waendeleze bifu ambalo lilikuwa limezizima kwa muda.
“Hakuna urafiki wowote hapa kuna kipindi ndio walipatana lakini cha ajabu juzi wamekutana na hakuna wote wamewekeana ubishi kusalimia, sasa kwa sisi watu wazima tunajua hali inavyokua na hao wanatakiwa kukaa chini na kuzungumza si kuzungumza na waandishi eti wamekubaliana,” kilidai chanzo hicho.
Hata hivyo alipotafutwa Sintah ili kutoa la moyoni juu ya kuwekeana ukauzu alidai kuwa ni kweli walipatana lakini haoni sababu ya kuendelea kuzungumza naye kwani alichokifanya walishakimaliza.
“Jamani kwani mi nina makosa gani kama mazungumzo tulifanya na tukamaliza ubishi, sasa nizungumze naye nini tena wakati kila mmoja anafanya mambo kama anataka kuzungumza na mimi awe kitu cha maana bila hivyo tutabaki kuwa marafiki wa kujuana tu,” alidai.
Hata hivyo naye Agnes alipozungumzia ishu hiyo alidai kuwa hapendi alichomfanyia Sintah kwani walipokutana yeye alifunguka na kumsalimia lakini Sintah hakutana kujibu kwa kujiona staa.
“Sina shida na salamu yake kwani nilimpa hii lakini alishindwa kuitikia kwa sababu tu ajione staa kwa kitu gani alichokuwa nacho hadi ashindwe kuitikia salamu yangu, sihitaji kuzungumza naye tena,” alidai Agnes Masogange.
No comments:
Post a Comment