Asubuhi ya leo kumezagaa
taarifa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab wa Zanzibar, Bi. Kidude
amefariki dunia. Radio ya Zenji FM ya visiwani humo nayo ilitangaza kifo
chake. Lakini kutokana na vyanzo mbalimbali vya uhakika akiwemo mjukuu
wake, Bi. Kidude bado yupo hai.
Mo Blog: Habari zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii
kuwa mkongwe wa muziki wa jadi visiwani Zanzibar Bi. Kidude amefariki dunia si
za kweli MO BLOG imezungumza na watu wa karibu ambao wamesema kwamba Bi. Kidude
bado anavuta pumzi na amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo
visiwani humo.
Jamani habari kutoka chanzo cha uhakika zinasema Bi Kidude hajafariki yupo mahututi tu. Samahani wote niliowapotosha kwa tweet yangu.
#BiKidude is not dead. According to mjukuu wake.
Asubuhi hii Kuna habari mbaya zinasambazwa kuhusu mwimbaji Maarufu wa muziki wa taarabu Bi Kidude... Habari hizo ... m.tmi.me/wk53w
Hii si mara ya kwanza kwa Bi. Kidude kuzushiwa kuwa amefariki dunia.
No comments:
Post a Comment