DOGO anayetisha katika muziki wa Bongofleva, Abubakar Chende ‘Dogo Janja’ juzikati alinaswa akiwa katika pozi la malavidavi na mnenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Maria Soloma, Shakoor Jongo anashuka nayo.
Mpango mzima ulichukua nafasi usiku wa Septemba 5, 2012 ndani ya Club Bilicanas wakati bendi hiyo ikitoa burudani ukumbini humo ambapo wawili hao walinaswa wakiwa wamekumbatiana ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.
Maria Soloma alipowekwa mtu kati na Over the Weekend na kutakiwa kueleza kunani kati yao, alifunguka: “Jamani hakuna chochote kati yetu, Dogo Janja ni rafiki yangu wa kawaida tu na hakuna ishu yoyote inayoendelea, nakuomba uifute hiyo picha uliyotupiga,” alisema Maria Soloma.
No comments:
Post a Comment