Mkali
mwenye hit kibao kila mwaka kila akitoa na sasa ana hit moja kubwa sana
inayokwenda kwa jina la mtoto wa kariakoo prince dully sykes anatafutwa
na majamaa yanayosemekana kuwa ni wanajeshi.
Tukio ilo lilitokea juzi
katika ukumbi wa mzalendo ambapo dully ilitokea kupishana lugha na mjeda
mmoja aliekuwa kavaa kiraia na hapo ndipo mjeda yule akatishia kumtupa
dully kutoka juu ya ghorofa hiyo ya mzalendo mpaka chini, hapo ndipo
dully alipomruhusu bounsa wake kufanya kazi yake anaejulikana kwa jina
la arafat ngumi jiwe. bunsa huyo kama kawaida yake na jina lake lilivyo
akamtwanga sana jamaa huyo bila yakujua kama ni mjeda.
Akiongea na
xdeejayz arafat ngumi jiwe amesema sisi tumeamua kujihami kwani yule
jamaaa alikuwa anataka kumtupa dully kutoka ghorofani hivyo ndio
tukajihami kwa kumpiga. akaulizwa" unajuakama jamaa uliempiga ni
mwanajeshi? akasema yeye ajui ni nani? chanzo chetu cha habari kinasema
dully sykes ameamua kujificha kutokana na salam amnazozipata kama kuna
wanajeshi wanakutafuta leo siku ya pili.
No comments:
Post a Comment